Wakili Msomi: Yanga wamefanya uzembe kwa Feisal

Wakili Msomi: Yanga wamefanya uzembe kwa Feisal

Mchezaji yoyote yule, duniani kote, saa yoyote ile anaweza kuamua kuvunja mkataba wake na klabu yake ikiwa atataka kufanya hivyo ili kuwa huru, kikubwa ajiandae kulipa gharama ya kufidia huo mkataba.
 
Issue sio kuvunja mkataba, swala ni utaratibu wa kuvunja watu wana twist story mimi mwanzo nlikua upande wa Feisal ila nmefatilia nmegundua kuna sehemu haipo sawa
Yule ameajiriwa. Kwani Yanga mtu hatakiwi kujiuzulu? Kalipa mishahara mitatu ya notisi, Kalipa hela alopewa kama manunuzi. Hataki kuchezea yanga. Uzuri yanga imekiri kwamba kaandika barua. Ulitaka afanyeje?
 
Wana Yanga mwacheni Fei Toto aende zake huko Azam. Yanga ni kubwa sana kuliko Fei Toto.
 
Utaratibu wa kuvunja mkataba haupo upande mmoja pia sheria za FIFA zinaruhusu kuvunja msimu ukiwa umeisha sio kati kati ya msimu hii kitu wasipo kaa kuongea Feisal hatacheza mpaka mwisho wa msimu
Iyo sheria ya FIFA ni kifungu gani kinachosema mpaka msimu uishe?huu ni msimu wa dirisha dogo TFF washatangaza timu zisajili.
Yanga watapoteza muda tu wabaki na iyo hela milioni 100 watafute mashine nyingine,akuna namna Yanga watambakisha Fei akuna.
 
Kwanza anapaswa aelewe kuwa Neymar hakuwalipa Barca gharama za pesa walizomsaini bali aliwalipa Barca pesa kulingana na thamani waliyomuwekea endapo kama kuna klabu itamuhitaji(release clause/buyout clause)
Kwenye mkataba wa Yanga na fei toto. Yanga wameweka release clause ambayo inamtaka mchezaji kurudisha signing fee na mshahara wa miezi mitatu
 
Shwaini wengi wanajua pesa aliyorudisha fei ni yake kumbe ni kama anawarudishia Yanga pesa yao (signing fee),Yanga wakiridhia kupokea ile pesa basi itabidi wataje pesa yao kukubali kuvunja mkataba,kama ilivyo kwa wachezaji na makocha tunavyosikiaga fifa imewataka iwalipe kwa kuvunjiwa mikataba na ni hivyo kwa wachezaji,fei akae chini na Yanga wamtajie kiasi wanachotaka awalipe asepe sio aamke tu asubuhi akadeposit pesa kwenye acc ya Yanga eti ndio kavunja mkataba!
Any contract should have consideration. Sasa ukisema awarudishie halafu wataje tena hela yao huoni kama inakuwa siyo sahihi
 
Kweli huijui sheria, na hata vipengele vya kisheria kwenye mikataba huvijui pia maana yake.

Hapo suala sio lazima mpaka viongozi wa Yanga SC wakae na Azam ndio waongee biashara, muhimu ni kama umeweka kipengele kwenye mkataba wa mchezaji wako kinachomruhusu kuondoka aki deposit kiasi fulani cha pesa, basi hapo umejibana mwenyewe.

Mchezaji ataondoka wakati wowote akiamua, muhimu aweke pesa mliyotaka kwenye akaunti yenu, hapa suala la Yanga SC kuongea na Azam linakuwa halina maana tena, halipo, kwasababu mchezaji ameshavunja mkataba na Yanga SC kwa kuweka mzigo kwenye akaunti, huyu sasa ni sawa na mchezaji huru.
Huyu jamaa anaonekana ni mweupe kabisa kichwan, yeye hajui Kama mchezaji anaweza kuvunja mkataba na timu yake akawa huru?? Then akatafuta timu yeye akiwa mchezaji huru?

Shida shule za kata nchi hii zimekuwa nyingi mno

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Feisal yuko sahihi kwa 100% kisheria.
Ameamua kuvunja mkataba na Yanga kwa kulipa gharama yote inayotamkwa na mkataba wake. Hakuna tena suala la kukaa mezani, kukubaliana au kupatana. Mkataba wa Feisal imetamka yote na wote umefuatwa. Feisal kwa sasa ni mchezaji huru, ana uhuru wote wa kwenda klabu yoyote hata bure. Na Yanga kwa sasa hawahusiki chochote na Feisal.
Basi na aende huko Azam fc
 
Bro ayo ni maoni yako, lakini kwani huonagi wachezaji wengi wakivunja mkataba na timu zao na kubaki wachezaji huru. Klabu inabidi iwe na ustadi wa kumbana mchezaji kwa kutokumpa uwezo wa kuuvunja mkataba kitu ambacho yanga wameshindwa kufanya. Mbona Dejan kavunja mkataba na simba akawa free agent saiv yuko tim nyngne. Ndomana yanga wanaitwa utopolo, hawana hata ustadi wa kutengeneza vizuri mikataba. Lakini shida hio sio kwa yanga tu hata tim nyngne bongo. Shida ni Elimuu!!!
Dejan akidai Simba Kuna vipengele wamekiuka
 
Kweli huijui sheria, na hata vipengele vya kisheria kwenye mikataba huvijui pia maana yake.

Hapo suala sio lazima mpaka viongozi wa Yanga SC wakae na Azam ndio waongee biashara, muhimu ni kama umeweka kipengele kwenye mkataba wa mchezaji wako kinachomruhusu kuondoka aki deposit kiasi fulani cha pesa, basi hapo umejibana mwenyewe.

Mchezaji ataondoka wakati wowote akiamua, muhimu aweke pesa mliyotaka kwenye akaunti yenu, hapa suala la Yanga SC kuongea na Azam linakuwa halina maana tena, halipo, kwasababu mchezaji ameshavunja mkataba na Yanga SC kwa kuweka mzigo kwenye akaunti, huyu sasa ni sawa na mchezaji huru.
Sawasawa
 
Back
Top Bottom