Wakili Msomi: Yanga wamefanya uzembe kwa Feisal

Kweli huijui sheria, na hata vipengele vya kisheria kwenye mikataba huvijui pia maana yake.

Hapo suala sio lazima mpaka viongozi wa Yanga SC wakae na Azam ndio waongee biashara, muhimu ni kama umeweka kipengele kwenye mkataba wa mchezaji wako kinachomruhusu kuondoka aki deposit kiasi fulani cha pesa, basi hapo umejibana mwenyewe.

Mchezaji ataondoka wakati wowote akiamua, muhimu aweke pesa mliyotaka kwenye akaunti yenu, hapa suala la Yanga SC kuongea na Azam linakuwa halina maana, tena halipo, kwasababu mchezaji ameshavunja mkataba na Yanga SC kwa kuweka mzigo kwenye akaunti, huyu sasa ni sawa na mchezaji huru.
Kuvunja mkataba ni makubaliano kwaiyo hata timu ikiona sio wakati muafaka wa kuvunja mkataba inaweza kukataa izo pesa na mchezaji akalazimika kutumikia mkataba wake mpaka utakapofika kikomo ndo haondoke ubaya utakuja tu mchezaji atakua ni kama analazinishwa wakati moyo wake haupo hapo
 
Neymar alienda PSG bila makubaliano kati ya PSG na Barca.
Alichofanya Neymar ni kuvunja mkataba 250 million euro. Then akawa free agent akaenda zake PSG. Yaani hata FFP haikuwa na nguvu yoyote hapa..
Neymar na barca walikubaliana kuvunja mkataba ndio barca akapokea zile pesa barca alikua na uwezo wa kuzikataa zile pesa na neymar angelazimika kubaki kutumikia mkataba wake mpaka neymar anamalizana na barca psg ilikua pembeni haiusiki na chochote. Kama hozi tetesi ni za kweli basi situation iliyopo hapa ni tofauti feisal kadeposit pesa bila kukaa mezani na kukubaliana na uongozi wa yanga kwaiyo yanga anayo nguvu kisheria kukataa izo pesa na feisal akalazimika kubaki kumaliza mkataba wake
 
Hapo sijui Sheria is kuna raia ni vilaza sana kwenye soka, umeona wapi mchezaji mwenye mkataba na timu anasajiliwa na timu nyingine bila hizo timu kukubaliana? Yaani Leo Jude Bellingham apokee pesa kutoka Man City akailipe Dortmund then awe mchezaji wa Man City bila City na Dortmund kukubaliana?
Basi wachezaji wengi sana wangesepa Kwa namna hiyo.
Una uhakika gani kama hiyo pesa Feisal alipewa na Azam? Ukiambiwa kuthibitisha hili utaweza kweli au ndiyo unafuata maneno ya mtandaoni ? Unadhani Azam ni wajinga kiasi hicho kwamba watakiri walimpatia Feisal pesa ya kuvunja mkataba?
 
Kitu ambacho hujui ni kwamba Barca pia walipeleka malalamiko FIFa kama anavyofanya Yanga.
So barca hawakukubali kabisa kitendo cha Nyemar kusepa.
 
Kuvunja mkataba ni makubaliano kwaiyo hata timu ikiona sio wakati muafaka wa kuvunja mkataba inaweza kukataa izo pesa na mchezaji akalazimika kutumikia mkataba wake mpaka utakapofika kikomo ndo haondoke ubaya utakuja tu mchezaji atakua ni kama analazinishwa wakati moyo wake haupo hapo
Kama timu ikikataa pesa inakuwa imekwenda kinyume na kipengele cha makubaliano ya mkataba, unless pawepo na exceptions kwenye hicho kipengele, jambo ambalo bado sijaliona.
 
Kuvunja mkataba ni makubaliano as long as mkataba bado haujaisha basi attempt yoyote ya kuuvunja inapaswa pande zote mbili wakubaliane yaani kabla feisal hajalipa iyo pesa inabidi akae na uongozi wa yanga wakubaliane mkataba kwanza endapo upande mmoja ukikataa kuvunja mkataba maana yake ubaki ivyo ivyo mpaka utakapofika mwisho, uwezi ukamlazimisha yanga avunje mkataba wakati msimu upo kati yupo kwenye mashindano mengi anahitaji wachezaji wake tegemeo wote.. sijui unanielewa? Ingekua kuvunja mkataba ni rahisi ivyo basi wachezaji wangekua wanadeposit release clause kwenye akaunt8 za klabu zao wanaondoka tu kimya kimya
 
Usikute viongozi wa Yanga walikubaliana na Azam dili iliposanuka wanajaribu kufunika kombe. Nchi hii usimwamini yoyote kwenye Jambo lolote.
Hiki ndicho ninachokiwaza muda wote. Uvumi wa Fei kutakiwa na Azam sio wa jana tu, una muda mrefu, lakini viongozi walikaa kimya ili kutoa mwanya kwa Fei kuhama ndipo wakurupuke kuwapoteza mashabiki. Huu ni mchongo wa viongozi wa Yanga na Azam, hakuna bahati mbaya hapo wala si uzembe. Watu wamekula pesa
 
Kitu ambacho hujui ni kwamba Barca pia walipeleka malalamiko FIFa kama anavyofanya Yanga.
So barca hawakukubali kabisa kitendo cha Nyemar kusepa.
Barca walipeleka malalamiko fifa kwamba psg wanavunja sheria ya financial fair play. Hawakupeleka malalamiko kuhusu neymar kuondoka. Neymar alitaka kuondoka ila barca akambania ndo akawa anafanya vituko baada ya lile sakata lake la kupigana na semedo mazoezini barca akachoka kuvumilia ikabidi wakae chini wamruhusu aondoke endapo akiweza kutoa release clause neymar akatoa na akaruhusiwa kuondoka
 
Una uhakika gani kama hiyo pesa Feisal alipewa na Azam? Ukiambiwa kuthibitisha hili utaweza kweli au ndiyo unafuata maneno ya mtandaoni ? Unadhani Azam ni wajinga kiasi hicho kwamba watakiri walimpatia Feisal pesa ya kuvunja mkataba?
Hili ni jepesi sana kama pesa ukifuatiliwa, kama hujui haya kaa kimya tu mkuu. Kwa mshahara uliosemwa wa Fei, hawezi kuwa na hiyo amount hivyo atalazimika kudeclare alivyoipata. Tuyaache tu hayo
 
Barca walipeleka malalamiko fifa kwamba psg wanavunja sheria ya financial fair play. Hawakupeleka malalamiko kuhusu neymar kuondoka. Neymar alitaka kuondoka ila barca akambania ndo akawa anafanya vituko baada ya lile sakata lake la kupigana na semedo mazoezini barca akachoka kuvumilia ikabidi wakae chini wamruhusu aondoke endapo akiweza kutoa release clause neymar akatoa na akaruhusiwa kuondoka
Ingekuwa rahisi hivyo wachezaji wangekuwa wanahama hovyo tu kila wakitakiwa na timu tofauti. Think
 
Hapo sijui Sheria is kuna raia ni vilaza sana kwenye soka, umeona wapi mchezaji mwenye mkataba na timu anasajiliwa na timu nyingine bila hizo timu kukubaliana? Yaani Leo Jude Bellingham apokee pesa kutoka Man City akailipe Dortmund then awe mchezaji wa Man City bila City na Dortmund kukubaliana?
Basi wachezaji wengi sana wangesepa Kwa namna hiyo.
Kilaza ni wewe , angalia the way Neymar alovyoondoka Barcelona. Neymar amenumu mkataba wake mwenyewe issue ikawa imesiha...na kulikiwa hakuna makubalianono baina Bara na PSG
 
Watu wanajua kuvunja mkataba ni rahisi tu hawajui yale ni makubaliano kama upande mmoja unaona haupo katika wakati mzuri wa kuvunja mkataba unaweza ukakataa
 
Kilaza ni wewe , angalia the way Neymar alovyoondoka Barcelona. Neymar amenumu mkataba wake mwenyewe issue ikawa imesiha...na kulikiwa hakuna makubalianono baina Bara na PSG
Wabongo tuna vichwa vigumu sana kuelewa.. neymar alimalizana na uongozi wa barca wakakubaliana wanavunja mkataba ila feisal hajamalizana na uongozi wa yanga kadeposit tu pesa bila makubaliano ya kuvunja mkataba kwaiyo yanga ana nguvu ya kiaheria kukataa izo pesa na feisal atalazimika kuendelea kutumikia mkataba wake.. hivi amuelewi au mmechagua tu kutokuelewa?
 
Umesoma mkataba wake au unabwabwaja tu?, usiendeshwe na mihemko ila angalia kipengele kipi cha mkataba kilichovunjwa au utaratibu upi ulioko kwenye mkataba sio kurukia vitu ambavyo hauna data.
Waambini viongozi wenu waweke vifungu vilivyokiukwa vilivyoko kwenye mkataba sio hizo taaraba mnazokumbatia eti utaratibu haujafuatwa, mkiulizwa vifungu mnakimbia.
Nasikitika kusema umeandika pumba nyingi huna tofauti na wengine wakurupukaji. Fuatilia kwa makini usiwe bendera fuata upepo

Barua walioandika jana Yanga imejieleza vizuri hujaifuatilia ila uko hapa kutemaashudu na unachojua ni kukurupukia mambo.
 
Barca walipeleka malalamiko fifa kwamba psg wanavunja sheria ya financial fair play. Hawakupeleka malalamiko kuhusu neymar kuondoka. Neymar alitaka kuondoka ila barca akambania ndo akawa anafanya vituko baada ya lile sakata lake la kupigana na semedo mazoezini barca akachoka kuvumilia ikabidi wakae chini wamruhusu aondoke endapo akiweza kutoa release clause neymar akatoa na akaruhusiwa kuondoka
Barca walilalamika kwa kigezo kuwa HAWAKUTARAJIA PESA WALIZOWEKA KUVUNJA MKATABA ZITALIPWA halafu pasiwepo financial irregularities. Waliweka dau kubwa mno kama kigingi, lakini kuhusu kuvunja mkataba, kipengele cha mkataba wa Neymar kilikuwa cha UNILATERAL TERMINATION OF CONTRACT. Kwa hiyo kama Neymar angemudu dau la Euro m222 kuununua mkataba, basi hakuhitaji makubaliano na klabu. Hii ndio sababu Barca walipigwa na butwaa, kwani hawakutarajia ataweza kutoa dau hilo.

Sasa miataba wa Fei kwa mujibu wa viongozi ni bilateral lijapo suala la kuuvunja, pande mbili zokae mezani kukubaliana.
 
Nasikitika kusema umeandika pumba nyingi huna tofauti na wengine wakurupukaji. Fuatilia kwa makini usiwe bendera fuata upepo

Barua walioandika jana Yanga imejieleza vizuri hujaifuatilia ila uko hapa kutemaashudu na unachojua ni kukurupukia mambo.
Yanga hawajawahi kuaminika kwenye suala la mikataba ya wachezaji, usiwe unabeba kila jambo toka yanga kama lilivyo.

Suala la Fei ni jambo la kitaaluma hivyo kama hii sio taaluma yako kaa pembeni acha watu wenye maarifa juu ya mikataba na sheria watoe maoni kisha wewe pembua upate chakula cha ubongo.
 
Barca walilalamika kwa kigezo kuwa HAWAKUTARAJIA PESA WALIZOWEKA KUVUNJA MKATABA ZITALIPWA halafu pasiwepo financial irregularities. Waliweka dau kubwa mno kama kigingi, lakini kuhusu kuvunja mkataba, kipengele cha mkataba wa Neymar kilikuwa cha UNILATERAL TERMINATION OF CONTRACT. Kwa hiyo kama Neymar angemudu dau la Euro m222 kuununua mkataba, basi hakuhitaji makubaliano na klabu. Hii ndio sababu Barca walipigwa na butwaa, kwani hawakutarajia ataweza kutoa dau hilo.

Sasa miataba wa Fei kwa mujibu wa viongozi ni bilateral lijapo suala la kuuvunja, pande mbili zokae mezani kukubaliana.
Kwaiyo barca walipeleka malalamiko dhidi ya nani uko fifa? Psg au neymar?
 
Wakili na mwanamichezo mzoefu nchini, Aloyce Komba ametoa ufafanuzi juu ya dili la Fei Toto kutua Azam akisema:
.
“Yanga wamefanya uzembe wenyewe na wasije wakathubutu kukimbilia Fifa kama walivyofanya kwa Bernard Morrison itakula kwao. Waangalie vizuri mkataba wa mchezaji unaeleza nini, watapoteza muda zaidi.”
.
“Ninachokiona Yanga walimpa mkataba Fei ambao hauna faida kwao. Unawekaje kiasi hicho cha pesa kuvunja mkataba wake wakati unaona kabisa kiwango cha mchezaji kilivyo. mchezaji hawezi kuacha pesa hasa kama mkataba wake unaruhusu kuununua ama kuuvunja.”
.
“Sioni kama Azam wamekosea na ni timu ambayo inazingatia sana masuala ya kisheria katika kuvunja mikataba ya wachezaji wao ama wanaposajili mchezaji. Azam siyo wajinga kiasi hicho wakurupuke tu kumsajili Fei Toto pasipo kuzingatia taratibu za kimkataba.
.
“Wanachotakiwa kukifanya Yanga ni kuulezea umma ama wanachama na mashabiki juu ya hilo, lakini mengine ni kuleta siasa tu kwenye mpira.”

My Take
Nawakumbusha tu Yanga kuitwa Utopolo ni maono ya ndani sana. Hii ndio maana halisi ya Utopolo
Komba ni kolo analazimisha hoja.
 
Hapo sijui Sheria is kuna raia ni vilaza sana kwenye soka, umeona wapi mchezaji mwenye mkataba na timu anasajiliwa na timu nyingine bila hizo timu kukubaliana? Yaani Leo Jude Bellingham apokee pesa kutoka Man City akailipe Dortmund then awe mchezaji wa Man City bila City na Dortmund kukubaliana?
Basi wachezaji wengi sana wangesepa Kwa namna hiyo.
Namjua Komba ni mojawapo wa mawakili kilaza. Huwa hajawahi kushinda kesi[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom