Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

NATAMANI LEO TUJAZE NYUZI JF ZIKIENDA
#JUSTICE FOR MWABUKUSI
#MWABUKUSI SIO MHAINI.
#FREE MWABUKUSI.
# MWABUKUSI FOR TANGANYIKA.
# MWABUKUSI KWANZA DP WORLD ISUBIRI.
Ningelifuraika sana endapo angekamatwa Lissu, maana tumechoka naye kwa kutufehedheshea viongozi wetu.
 
Pilato akamuuliza Yesu " Usingetenda kosa lolote wangekuleta kwangu?"
HII UMEWAHI KUISIKIA??

Siku mbili kabla ya sikukuu ya Krismas yaani 23/12/2011 nchini Kenya ilifunguliwa kesi maarufu na bwana Dola Indidis mwanasheria maarufu nchini Kenya aliyeishtaki nchi ya Israel kwa kumuua Yesu.

Kesi hiyo namba FOJ/001/D10/11 Wakili msomi Indidis alidai hakuipeleka kesi mahakamani kwa misingi ya kidini bali kwa misingi ya Kisheria. Alisema "Its academic thing not a theological thing". Yeye alichoangalia si unabii bali legal procedure. Pia alisisitiza ameamua kumtetea Yesu kama mtoto wa Yusufu (fundi seremala) na sio Yesu kama Masihi "I look Jesus as son of Joseph not as the Messiah"

Alipoulizwa mbona ilitabiriwa Yesu atakufa, alisema anafahamu hilo ila hoja sio Yesu kufa, hoja yake ni process iliyotumika kumuua haikuwa sawa kisheria. Alidai mahakama ilikosea kujiingiza kwenye kesi hiyo "The court should not involve itself in that crooked case."

Alisema Yesu angehukumiwa kifo kwa kufuata taratibu za kisheria kusingekuwa na shida, ila aliuawa kikatili bila kupewa haki ya kusikilizwa. Wakati Yesu anapelekwa mahakamani (kwa Pilato) tayari alishaanza kusulubiwa kabla hata hukumu haijatoka.

Huo ulikuwa ukiukwaji wa sheria maana mtuhumiwa hawezi kuadhibiwa kabla ya mahakama kujiridhisha kuwa mtu ana hatia. "no punishment could be made unless the court proved beyond the reasonable doubts that Jesus was guilt" Alisema Yesu angepata wakili wa kumtetea angeachiwa huru. Hata kama ilimpasa kufa angeuawa kwa namna nyingine.

Alidai pia Pilato hakuwa na nguvu ya kisheria ya kusikiliza ile kesi na hata yeye alikiri hilo ndio maana akawarudisha wayahudi kwa Herode. Lakini akalazimishwa kutoa hukumu kwa pressure ya mfalme Herode. "Pilate had no jurisdiction to give the judgment, he confessed, and also he confessed the innocence of Jesus"

Pia alidai Pilato alikiri Yesu kutokuwa na hatia, lakini bado alisulubiwa. Sasa kama Pilato ndio alikuwa Jaji na hakuona hatia ya Yesu kwanini bado Wayahudi walimsulubisha?

Akaongeza kuwa kitendo cha Wayahudi kumsulubisha Yesu mbele ya Jaji (Pilato) ni kujichukulia sheria mkononi na ni uvunjifu wa haki za binadamu. "Jesus was tochered in-front of Judge, that is abuse of Human rights"

Alidai misingi ya haki ilikiukwa katika kuongoza kesi (miscarriage of Justice) na Yesu hakupewa nafasi ya kusikilizwa japo alikuwa akilalamika. "Even Jesus complained but he was not given right to be heard,that is mis-courage of justice."

Alisema pia kuwa maamuzi hayakuzingatia principle of natural justice, na hukumu inapaswa kurekebishwa na Israel kuomba msamaha. "The judgment was bad in law and should be quashed"

Alitumia rejea muhimu ya kesi ya Mwai Kibaki vs Daniel Arap Moi 1999 kama refference ya kesi yake (MWAI KIBAKI Vs DANIEL TOROITICH ARAP MOI, Case Number :Civ App 172 of 1999").

Aliungwa mkono na makanisa kutoka nchi za Norway, Marekani, Israel, Uingereza, Tanzania, Afrika Kusini, Canada na Ujerumani.

Na YERICKO NYERERE.
 
Ukweli,jamaa walikuwa wanaenda kuimbua mahakama [emoji1]

Ova
 
Acha ujinga bhna Hili Jambo siyo jema aise
 

Huko Marekani unakoongelea huna lolote la kutolea mfano boss, ni bora ukae kimya. Huku mpaka speaker ana kinga ya kutoshtakiwa, huoni unatolea mfano wa giza na Nuru?
 
Kwa hiyo wamekamatwa kwa kosa la uhaini? Mbona kama ni hivo hao Uamsho waliachiwa?

Sent from my ATU-L31 using JamiiForums mobile app
 
Kama ni uonezi itageuka punde hakuna cha kudumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…