Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Ndugu Watanzania,

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa wakili msomi Boniface Kanjunjule Mwabukusi amekamatwa na Jeshi la Polisi kule Mikumi, Morogoro akiwa pamoja na Katibu wa Kanda wa CHADEMA, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali.

Inadaiwa kuwa walikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, watu waliojitambulisha kuwa ni Askari ndio wamewakamata pasipo kutaja kosa lao na wapi wanapelekwa zaidi ya kuambiwa ni Maelekezo kutoka Juu. Pia, vifaa vyao vya mawasiliano (Simu za mkononi) vimechukuliwa.
Polisi wamekiri kuwakamata? Wanakamatwa kwa uchochezi upi?
 
Hata wafanye nini, hoja zijibiwe.....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Sisi Watanganyika wasomi wengi wetu ni kama kasuku. Tuna uwezo wa kukariri kilichosemwa tu basi, mambo mwengine ZERO au below average.
 
Yaani Tz saa zingine tuna fanya mambo ya ajabu kidogo.
Yaani mtu anaweza kua na hoja za maana na muhimu kabisa lakini badala kuziwasilisha kwa umahiri, ufasaha na hekima ili kueleweka, huanza kudhihaki na kukejeli Mihimili ya dollar au viongozi eti ndio ujasiri au uhodari.
Huko ni kukosa hoja, kupoteza muda, thamani na uelekeo wa ya hoja ya Msingi. Zaidi sana ni kuwachanganya Wananchi na kuwapoteza maboya.

Mbaya zaidi vyombo vya dollar vikifanya kazi yake wahusika huwa wadogo kama mbegu ya haradali, hutia huruma kweli kweli na zile hoja za maana huyeyuka na kutokomea kabisa. Mashabiki hutishika na kurud nyuma, kwa sauti ya kinyonge ya keyboard wanaanza ooh sijui #free nani oohh # fulani must be Free etc .....
 
Yaani Tz saa zingine tuna fanya mambo ya ajabu kidogo.
Yaani mtu anaweza kua na hoja za maana na muhimu kabisa lakini badala kuziwasilisha kwa umahiri, ufasaha na hekima ili kueleweka, huanza kudhihaki na kukejeli Mihimili ya dollar au viongozi eti ndio ujasiri au uhodari.
Huko ni kukosa hoja, kupoteza muda, thamani na uelekeo wa ya hoja ya Msingi. Zaidi sana ni kuwachanganya Wananchi na kuwapoteza maboya.

Mbaya zaidi vyombo vya dollar vikifanya kazi yake wahusika huwa wadogo kama mbegu ya haradali, hutia huruma kweli kweli na zile hoja za maana huyeyuka na kutokomea kabisa. Mashabiki hutishika na kurud nyuma, kwa sauti ya kinyonge ya keyboard wanaanza ooh sijui #free nani oohh # fulani must be Free etc .....
Weka ushahidi wa unayosema. Walimkebehi nani?
 
Hakuna jipya hapo, Adv Mwabukusi hajakamatwa peke yake, hata Mdude Nyagali, na kamanda Nyaisunga, nao pia wamekamatwa, wote wako kutuo cha polisi, Mikumi, Morogoro.

Hapa tuwekane sawa tu, hayupo yeyote kati ya waliokamatwa ambaye hakujua matokeo ya kile wanachokipigania, wanachokifanya polisi sio kuwatisha, au kuwaogopesha, ni kuwafanya wawe imara zaidi kwenye mapambano.

Nawaambia hamtaamini, ipo siku yaja, haipo mbali, Samia na ushetani wake nae pia hataamini, kile kinachoenda kutokea, hakika atajuta kwa kupuuza kusikiliza alichoshauriwa, eti anaziba masikio?

Hii Tanganyika ina wenyewe, na wenyewe ndio wamegoma rasilimali zao kutolewa bure kama sadaka, wenye Tanganyika wala sio viongozi wanaokula mishahara kwa jasho la kodi zetu, this time hili somo linaenda kufundishwa kwa vitendo..
Keyboard Warrior😂
 
Wewe ni pumbavu, na sioni umuhimu wa kukusoma, Nina kuweka pembeni for now, Tanzania sio mali ya ccm na kutofautiana kiitikadi ni haki ya kila mmoja wetu humu, President Trump alikua yupo right kuhusu hizi pithole country, Tanzania SIO ulaya!!
Tanzania sio Nchi ya kujifunzia kufanya majaribio ya kipumbavu,eti Maandamano nyoooo,katafuteni Kwa kufanyia sio Tanzania stupid.
 
Awamu hii kina Mama wamerithi mihimili kazi tunayo.
 
Back
Top Bottom