Yaani Tz saa zingine tuna fanya mambo ya ajabu kidogo.
Yaani mtu anaweza kua na hoja za maana na muhimu kabisa lakini badala kuziwasilisha kwa umahiri, ufasaha na hekima ili kueleweka, huanza kudhihaki na kukejeli Mihimili ya dollar au viongozi eti ndio ujasiri au uhodari.
Huko ni kukosa hoja, kupoteza muda, thamani na uelekeo wa ya hoja ya Msingi. Zaidi sana ni kuwachanganya Wananchi na kuwapoteza maboya.
Mbaya zaidi vyombo vya dollar vikifanya kazi yake wahusika huwa wadogo kama mbegu ya haradali, hutia huruma kweli kweli na zile hoja za maana huyeyuka na kutokomea kabisa. Mashabiki hutishika na kurud nyuma, kwa sauti ya kinyonge ya keyboard wanaanza ooh sijui #free nani oohh # fulani must be Free etc .....