Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

20230812_185442.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya taarifa iliyotolewa august 11 2023 likiwaonya wanaofanya uchochezi kwa lengo la kuiangusha serikali jeshi limedaiwa kuwakamata watu wawili wanadaiwa kufanya vitendo hivyo.

Watu hao ni Boniphasi Mabukusi na Saidi Nyangali au Mdude. Na mahojiano zaidi na watuhumiwa hayo yanaendelea
Aidha limesema litaendelea kufuatilia na kuwakamata watuhumiwa zaidi.
Screenshot_20230812-191715_1691857068908.jpg
 
Baada ya taarifa iliyotolewa august 11 2023 likiwaonya wanaofanya uchochezi kwa lengo la kuiangusha serikali jeshi limedaiwa kuwakamata watu wawili wanadaiwa kufanya vitendo hivyo...
Hao wawili ndio wanatishia kumwangusha Mama?😅😅😅
 
Bongo kwa kubuni Dili za upigaji hawajambo maadamu per diem zinaingia hadi kamakamata iishe mtu ashamaliza kupaua
 
Namwaga pombe chini kumkumbuka hayati Chuma John Pombe Magufuli, kama kuna mungu basi amuhifadhi mahala pema.
 
Watu badala wajitafutie wao na familia zao, wako busy kujifanya wana uchungu na nchi ambayo watakufa na kuiacha
 
1691857636470.jpg


Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama Mdude kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP -David Misime imesema wawili hao wamekatwa kwa mahojiano ambayo yanaendelea.

“Jeshi la Polisi kama lilivyo eleza jana tarehe 11 Agosti 2023 linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa
mujibu wa sheria.

“Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata maeneo ya Mikumi Mkoani Morogoro majira ya saa nane na nusu usiku tarehe 12 Agosti 2023,” imesema taarifa hiyo.

Hayo yamejiri baada mapema asubuhi leo kuibuka taarifa kukamatwa kwa Mwabukusi na Mdude kuenea katika vyanzo mbalimbali.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofumgwa kati ya serikali na Dubai.

Kukamatwa kwa Mwabukusi kumekuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.”
 
Baada ya taarifa iliyotolewa august 11 2023 likiwaonya wanaofanya uchochezi kwa lengo la kuiangusha serikali jeshi limedaiwa kuwakamata watu wawili wanadaiwa kufanya vitendo hivyo.

Watu hao ni Boniphasi Mabukusi na Saidi Nyangali au Mdude. Na mahojiano zaidi na watuhumiwa hayo yanaendelea
Aidha limesema litaendelea kufuatilia na kuwakamata watuhumiwa zaidi.View attachment 2715543
Tukutane Kisutu, japo mhimili hauna meno ya msumeno.
 
Back
Top Bottom