Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Wakili Mwabukusi, Emmanuel Masonga na Mdude Nyagali wakamatwa na Polisi Mikumi wakiwa safarini kuelekea Dar es Salaam

Kwahizi hekaheka DP wenyewe wanaweza wakaona isiwe tabu wamrudishie mama bandari yake,, tatizo hapo ni pesa zote fisiemu wameshakula sasa sijui watarejesha nini au ndo kuleta Tozo ya pikipiki.
 
View attachment 2715570

Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama Mdude kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP -David Misime imesema wawili hao wamekatwa kwa mahojiano ambayo yanaendelea.

“Jeshi la Polisi kama lilivyo eleza jana tarehe 11 Agosti 2023 linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa
mujibu wa sheria.

“Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata maeneo ya Mikumi Mkoani Morogoro majira ya saa nane na nusu usiku tarehe 12 Agosti 2023,” imesema taarifa hiyo.

Hayo yamejiri baada mapema asubuhi leo kuibuka taarifa kukamatwa kwa Mwabukusi na Mdude kuenea katika vyanzo mbalimbali.

Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofumgwa kati ya serikali na Dubai.

Kukamatwa kwa Mwabukusi kumekuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.”
Kamateni hadi wauza vitumbua aisee, mtusaidia vijana wetu kupata maisha. Hamjui tu vile hii kitu inanifurahisha. Ni wakati sasa wa watanzania kufaidika na kupitia viongozi wa hovyo.
 
Wanaotete mali za Nchi wanakatwa ni kama tupo enzi za kaburu na Wazulu hii sijawahi ona...wanaotetea Mali za vizazi na vizazi mnawakamata hii laana itawafuna sana...
Kituko kweli

Ila time will tell

Ova
 
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo , Kamanda Misiime , Shukrani nyingi sana kwa Wananchi kwa kupaza sauti kuu , maana mngenyamaza watu hawa wangeweza kupotea kama Ben Saanane .

Kamanda Misiime amedai kwamba , watu hao wamekamatwa kwa tuhuma za Uchochezi , na kwamba kuna watu wengine bado wanasakwa ili waunganishwe nao.

======
Bali kwa Tafsiri ya wananchi , wanaoitwa wachochezi ni wale wote wanaopinga Mkataba duni wa kudhalilisha wa milele wa Bandari za Tanganyika tu (siyo za Zanzibar) na DP WORLD ya Waarabu wa Dubai , kwahiyo tunatarajia watu wengi zaidi kukamatwa kwa tuhuma hizi , wakiwemo wanasiasa , wanaharakati na Viongozi wa dini wanaopinga uwekezaji huu wa kitumwa .

Lengo la yote haya ni kuwatisha wananchi ili wamuachie Mwarabu Bandari zetu .

Je lengo hili litafanikiwa ?
Nashauri Mwehu Lissu asikamatwe. Na akikamatwa aletwe huku kwenye Hospitali ya Rufaa Chato, Kitengo cha Magonjwa ya Akili. Anahitaji matibabu huyu!
 
Back
Top Bottom