View attachment 2715570
Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwakamata Wakili Boniface Mwabukusi na Mpaluka Said Nyagali maarufu kama Mdude kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP -David Misime imesema wawili hao wamekatwa kwa mahojiano ambayo yanaendelea.
“Jeshi la Polisi kama lilivyo eleza jana tarehe 11 Agosti 2023 linawafuatilia ili liwakamate watuhumiwa walioandaa na kutoa maneno ya uchochezi, kazi hiyo inaendelea kufanyika kwa
mujibu wa sheria.
“Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata maeneo ya Mikumi Mkoani Morogoro majira ya saa nane na nusu usiku tarehe 12 Agosti 2023,” imesema taarifa hiyo.
Hayo yamejiri baada mapema asubuhi leo kuibuka taarifa kukamatwa kwa Mwabukusi na Mdude kuenea katika vyanzo mbalimbali.
Mwabukusi alikuwa mmoja wa wanasheria waliofungua kesi ya kupinga mkataba uliofumgwa kati ya serikali na Dubai.
Kukamatwa kwa Mwabukusi kumekuja muda mfupi baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi kuutangazia ulimwengu, kwamba “kuna njama za kumuangusha Rais wa Jamhuri, Dk. Samia Suluhu Hassan.”