Pre GE2025 Wakili Mwabukusi: Mwaka 2020 nilikamata masanduku manne ya kura bandia za Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kweli naungana na Mwabukusi, hiyo Sheria ni kama mtego, wake waseme vyama vyote vilishirikishwa. Nimeshangaa CHADEMA kuingia kwenye huo mtego.
vyama vilidhirikishwa Kwan uongo πŸ’
 
Kumekucha.....chama cha makundi.
1. Mbowe and Lema
2. Lissu and Heche.
3. Slaa,mdude,mwakubusi and mama kula.
4. Covid 19
Safi sana kwa kuanzia kisha ghafla bin vuuu wote wanaungana wanakuwa kitu kimoja kumkabili Ccm !
Patachimbika ! Siasa ni hesabu !!
 
Sure, kwanini nafasi zisitangazwe watu waombe kama nchi nyingine? mambo ya kijinga sn
Kenya si jirani zetu na wanatumia ushauri wako.

hata iweje asiekua wa chama tawala hapati chochote bila bihind the scene endorsement ya Kinara wa chama Tawala
Never ever πŸ’
 
Mkuu shirikisha akili yako kidogo, sahivi unajiona upo salama sababu upo CCM. Angalia maslahi ya nchi yako 50yrs to come.
Yaan Ben unishawishi na mimi ni zire
Kamwe siwezi kuambatana au kuchangamana na mtu au kundi la wanaususa au kuzira ,
ni useless kabisa hiyo maana yake you are unable to think and plan alternatives to confront the challenge ahead
 
Kabisa, halafu kwenye huo utapeli ilikuwa ni wa kujadili Nia njema ya rais ya 4R. Yaani ulikuwa ni mtego wa kienyeji kabisa.

Venus Star
Mimi nashangaa sana Comrade wangu kile unachokiongea kinanitia wasiwasi kwa namna fulani. Hivi kwenye mkutano wa vyama vya siasa hukumuona Salum Mwalimu akitoa michango yake? Hukumuona akipongeza 4R. Sasa wewe unataka, mtu fulani tu ambaye hana responsibility yoyote kwenye jamii ndiye atupatie direction!!! Sasa Slaa ni kiongozi wa kitu gani? Kwanza Slaa ameshazeeka anatakiwa akae nyumbani ale pensheni yake.
 
Nani amekuambia ana imani na huyo Salim Mwalimu? Huyo Salim Mwalimu na Mbowe hawana tofauti, wako kimaslahi zaidi. Kama mlimwita mkitegemea tutaamini ule utapela basi mmepoteza. Huyo Slaa amezeeka kuliko Joe Biden rais wa America? Kwa taarifa yako tuna imani na amachongea Slaa ambaye ni mzee, kuliko alichoongea Salim Mwalimu ambaye ni kijana.
 
Kwahiyo kuna CHADEMA "A" na CHADEMA "B"?
 

Hivi Mwabukusi ni mwanasiasa au mwanaharakati?
Naona naye siku hizi amekuwa mzee wa kufuata matukio.
 
Harakati zao hawa watu ni Sahihi lakini njia na mbinu wanazotumia ktk kufanya harakati hizi siyo sahihi.
 
Kweli naungana na Mwabukusi, hiyo Sheria ni kama mtego, wake waseme vyama vyote vilishirikishwa. Nimeshangaa CHADEMA kuingia kwenye huo mtego.

..kushirikishwa ni jambo moja.

..kusikilizwa na maoni yao kuzingatiwa ni jambo lingine.

..wananchi tumeshaamka tunaijua hiyo mbinu ya kusema wadau "walishirikishwa."

..mapendekezo na mitizamo ya Cdm inajulikana hivyo tunakwenda kuangalia kama yamezingatiwa kwenye sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…