Pre GE2025 Wakili Mwabukusi: Mwaka 2020 nilikamata masanduku manne ya kura bandia za Rais

Pre GE2025 Wakili Mwabukusi: Mwaka 2020 nilikamata masanduku manne ya kura bandia za Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Cdm ni imani sio sura ya hao wasaka maslahi. Kwa taarifa yako hata hiyo Mbowe mwenyewe hatuna imani naye, ndio itakuwa huyo Salim Mwalimu? Tuna imani na Lisu, sio hao wajanjawajanja.
Kwa hiyo unaweka imani kwa watu siyo kwenye taasisi? Je, CHADEMA na LIssu nani ni mkubwa?
 
Mimi nashangaa sana Comrade wangu kile unachokiongea kinanitia wasiwasi kwa namna fulani. Hivi kwenye mkutano wa vyama vya siasa hukumuona Salum Mwalimu akitoa michango yake? Hukumuona akipongeza 4R. Sasa wewe unataka, mtu fulani tu ambaye hana responsibility yoyote kwenye jamii ndiye atupatie direction!!! Sasa Slaa ni kiongozi wa kitu gani? Kwanza Slaa ameshazeeka anatakiwa akae nyumbani ale pensheni yake.

..Salum Mwalimu alikosoa utekelezaji wa 4R.

..hakuna mtu anaweza kusema Reconciliation ni jambo baya.

..Hoja ni kama kuna reconciliation kweli, au ni blabla.

.
 
Fuatilia yanayojiri kwenye mkutano wa waandishi wa Habari wa Dkt. Slaa, Mdude na Wakili Mwabukusi.

Mabadiliko ya Sheria yanayotaka kufanyika yanapasaswa kuendana na mabadiliko ya katiba. Huwezi kujenga. Tunashauri kwamba katiba ibadilishwe, tazama sheria inayohusu sheria ya uchaguzi, kilichofanyika wamekopi ibara ya 74 ya Katiba ikaitwa sheria ya uchaguzi. Hakuna kilichotatuliwa, uundwaji na uhuru wa tume bado haujashughulikiwa.

Katiba ya sasa haikujadiliwa hata kwa masaa 4 kwenye kuandokwa kwake, sasa ina umri wa mtu mzima. Katiba ndio msingi wa mamlaka tunayokabidhi kwa viongozi, sasa wewe tunakupa mamlaka kwa katiba hii unakwendaje kujipa mamlaka makubwa kuliko yale tuliyokupa?

Kinachotakiwa ni kutunga sheria kukwamua mchakato wa jaji Warioba, kuna sarakasi zilipigwa bungeni enzi hizo kukwamisha mchakato huo. Hapo ndipo kwenye mkwamo. Kazi hii ukiwapa watu serious inachukua miezi 3 tu, wao wanasema kila siku kuwa muda hautoshi, katiba ya India iliandikwa miaka 2 tu na mwezi 1 na ndio katiba kubwa zaidi duniani.

Yale niliyoshuhudia mimi, wanaoratibu wizi wakura ni maafisa wa uchaguzi, na wale wanasoma nyaraka za mahakamani, niliomba scrutiny of vote, huwezi amini afisa alirudi kwenye kituo cha kupiga kura akaanza kuchoma moto kura zangu. Nikaiandikia tume ya uchaguzi kwa barua kuwa nipo mahakamani, afisa wenu anachoma kura zangu, tume ikanijibu nipo mahakamani haiwezi kuingilia. Nimejaribu kuonesha experience yangu.

Mimi jimbo langu ni dogo sana, lakini nilikamata masanduku manne ya kura bandia za Rais. Mimi niliibiwa kizembe 2015, lakini 2020 niliibiwa. Unadhani sasa hivi nikiibiwa kuna kesi itaenda mahakamani? Hapana. Itaenda Manslaughter.

Haya tena mzee wa kubarikiwa anasema nini?

Na yeye ana chama cha kuongelea au ndiyo chama chake na mdudu na mwambulukuku.

Vipi bandari wamewachana nayo? Maji marefu?
 
Chadema walishaingizwa mkenge na tapeli la siasa Mbowe!, Ni mpuuzi tu ndio angeweza kwenye ule mkutano wakipumbavu.
 
..Salum Mwalimu alikosea utekelezaji wa 4R.

..hakuna mtu anaweza kusema Reconciliation ni jambo baya.

..Hoja ni kama kuna reconciliation kweli, au ni blabla.

.
Najaribu kuwaza kwa kina kuhusu hoja yako hii. Kwako wewe Reconciliation ya kweli ni kufanya kitu gani?
Je uundwaji wa hii miswada ya sheria siyo sehemu ya maridhiano?

Kwako wewe maridhiano ni kitu gani? Je, unataka CHADEMA wagawiwe masinia ya ubwabwa wale na familia zao?
Mimi nashauri CHADEMA warekebishe kwanza mambo yaliyo ndani ya CHAMA chao waondoe Ngugunization.
 
Chadema walishaingizwa mkenge na tapeli la siasa Mbowe!, Ni mpuuzi tu ndio angeweza kwenye ule mkutano wakipumbavu.

..Chadema wasingekwenda mkutano mzima ungekuwa wa kumsifia na kumtukuza Raisi.

..Maoni ya Salum Mwalimu, Benson Kigaila, na Mzee Hashim, yaliakisi hoja na kilio cha muda mrefu cha wananchi.

..Chadema wasingeshiriki, mkutano ungekusanya maoni ya chawa peke yao.
 
Mbona huyo jamaa aliyemechisha kanzu na kibandiko za zambarau macho yake anarembuwa rembuwa, ni mbarikiwa?

Papa katupa msemo mwaka huu.
 
Najaribu kuwaza kwa kina kuhusu hoja yako hii. Kwako wewe Reconciliation ya kweli ni kufanya kitu gani?
Je uundwaji wa hii miswada ya sheria siyo sehemu ya maridhiano?

Kwako wewe maridhiano ni kitu gani? Je, unataka CHADEMA wagawiwe masinia ya ubwabwa wale na familia zao?
Mimi nashauri CHADEMA warekebishe kwanza mambo yaliyo ndani ya CHAMA chao waondoe Ngugunization.

..kama Ssh anataka maridhiano basi apeleke mswada wa tume huru ya uchaguzi ambayo wajumbe wake wanapatikana kwa haki na uwazi.

..tume ya uchaguzi yenye wajumbe wasiopitia usaili wanateuliwa moja kwa moja na Rais/ Mwenyekiti / Mgombea wa Ccm ni kunajisi reconcialition.

..pia apeleke mswada utakaowaondoa wakurugenzi wa halmashauri na makada wa Ccm kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

..La muhimu aunde Tume ya Haki, Ukweli, na Maridhiano, itakayoangazia matendo ya ukiukwaji wa haki za wananchi ktk tawala mbalimbali hapa nchini.

..Undugunization uko zaidi Ccm. Watoto wa Mwinyi, Kikwete, Pinda, Lowassa, wamezawadiwa fursa mbalimbali ktk Ccm. Wengi uwezo wao ni mdogo.
 
Then what next!, Unaausa uchaguzi afu unakubali Mambo mengine?. Hii ni mipango ya hovyohovyo.
..Chadema wasingekwenda mkutano mzima ungekuwa wa kumsifia na kumtukuza Raisi.

..Maoni ya Salum Mwalimu, Benson Kigaila, na Mzee Hashim, yaliakisi hoja na kilio cha muda mrefu cha wananchi.

..Chadema wasingeshiriki, mkutano ungekusanya maoni ya chawa peke yao.
 
Kwa hiyo unaweka imani kwa watu siyo kwenye taasisi? Je, CHADEMA na LIssu nani ni mkubwa?
Tunaimani na taasisi inayosimamia tunachokitaka, sio taasisi za kwenda kusifia utashi wa rais kwa ajenda binafsi. Lisu ni zaidi ya cdm kwakuwa ana misimamo isiyoyumba.
 
Najaribu kuwaza kwa kina kuhusu hoja yako hii. Kwako wewe Reconciliation ya kweli ni kufanya kitu gani?
Je uundwaji wa hii miswada ya sheria siyo sehemu ya maridhiano?

Kwako wewe maridhiano ni kitu gani? Je, unataka CHADEMA wagawiwe masinia ya ubwabwa wale na familia zao?
Mimi nashauri CHADEMA warekebishe kwanza mambo yaliyo ndani ya CHAMA chao waondoe Ngugunization.
hawawezi kukuelewa kabisa hao, ndio maana wapo kama walivyo hawaongezeki wala kubadilika miaka nendra miaka rudi. vyama vya juzi tu vimewapiku kila idara kuanzia mindset mpaka mipango 🐒
 
kuzira au kususa ndio uzalendrooo🐒

Tz bado sana
Ni mtu mjinga tu ataendelea kushiriki upuuzi huku akisaka sifa ya kutokuoneka hasusi. Na kwa taarifa yako kususia ni mbinu sahihi ya kutaka mambo yafanyike kwa usahihi. Tuliwahi kuwasusia makaburu wa Africa kusuni kuhakikisha haki inapatikana. Ulikuwa hujazaliwa, hivyo hujui kususia maana yake ni Nini.
 
hawawezi kukuelewa kabisa hao, ndio maana wapo kama walivyo hawaongezeki wala kubadilika miaka nendra miaka rudi. vyama vya juzi tu vimewapiku kila idara kuanzia mindset mpaka mipango 🐒
Kama ni kubadalika basi ccm wanapaswa sana kubadilika, kama Bado mnakimbiza mwenge ambao hata kizazi hiki hakioni maana yake, unaweza kugeuka mshauri wa watu kubadilika?!
 
Yaan Ben unishawishi na mimi ni zire
Kamwe siwezi kuambatana au kuchangamana na mtu au kundi la wanaususa au kuzira ,
ni useless kabisa hiyo maana yake you are unable to think and plan alternatives to confront the challenge ahead
Alternative ni machafuko au mapinduzi ya kijeshi. Lakini kuendele kushiriki chaguzi zinazosimamiwa na tume ya rais ni upuuzi kama upuuzi mwingine.
 
Hivi Mwabukusi ni mwanasiasa au mwanaharakati?
Naona naye siku hizi amekuwa mzee wa kufuata matukio.
Kuwa mwanasiasa ni kukubali kuwa kondoo wa matakwa ya ccm. Siku hizi ukionyesha kukataa kuburuzwa na ccm ww sio mwanasiasa Bali ni mwanaharakati. Kibaya zaidi ukijifanya ni mwanasiasa unaporwa haki zako, kisha unatakiwa uendelee kutulia ili kudhibitisha ww ni mwanasiasa na sio mwanaharakati! Huu kama sio ujuha ni Nini?
 
Then what next!, Unaausa uchaguzi afu unakubali Mambo mengine?. Hii ni mipango ya hovyohovyo.

..kwa uchaguzi uliotokea 2020 kuna tofauti gani kati ya aliyeshiriki na aliyesusa?

..sote tumejifunza kwa hiyo kama WAZALENDO kutengeneza mfumo wa uchaguzi utakaotoa haki sawa kwa vyama vyote.
 
Back
Top Bottom