Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Mwanasiasa kuwa mfanyabiashara sio tatizo, tatizo ni kuitumia siasa kama myaji wa biashara, hapo ndipo penye tatizo, utumwa huanzia hapo.

Nielewe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kama watu wa aina hiyo ndio wapo kwenye siasa zetu, basi tunapotezeana muda. Tumeigeuza siasa kama kijiwe cha wacheza karata.

Hatutasogea popote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ndiyo maana tupo hivi, kama tulivyo sasa; kwa sababu viongozi waliopo kwenye nafasi sioni mwenye 'moto tumboni' kuwa tofauti na marupurupu yanayo patikana kutokana na nafasi wanazo zishikilia.

Tena nizaidi ya hao tunao wazungumzia hapa.
Hawa tulio nao sasa hivi, hata utaifa wao hauna maana yoyote kwao. Mfano mzuri wa kueleza hali ya hawa ni IGA ya Dubai.
Upigaji wa kawaida tu unao tokana na nafasi za uongozi wao, huku wakijali taifa lao, hali hiyo ingeepusha waliyodhamiria kuyafanya chini ya mradi wao wa Dubai. Hawa hata kutuuza hakuwastui chochote.
 
Mwanasiasa kuwa mfanyabiashara sio tatizo, tatizo ni kuitumia siasa kama myaji wa biashara, hapo ndipo penye tatizo, utumwa huanzia hapo.

Nielewe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Duh!
Hii kazi ya kuwa 'tutor' unaiweza kweli? Naona huyo jamaa hana hata chembe ya 'concept' inayohusu siasa.
Kuliwahi kuwepo kwenye vyuo vyetu vikuu takwa la kusomwa na kila mwanafunzi katika fani zote, lililo itwa 'Developmeny Studies', naona mpango huo ulikufa wenyewe baada ya "walaji na wenye maslahi binafsi" kushika hatamu za uongozi wa nchi yetu.

Matokeo yake ndiyo kama ya huyu unayejibishana naye hapa.
 
Ubovu wa sheria za kutokuwachukulia hatua waizi ndo ya kulaumiwa
Waizi wa ela kwenye ripoti ya CAG ni waajiriwa huko serekalin na bado wanafanya kazi Mfano hapo unalaumuje wapinzani

Miaka nenda rudi CAG anasema fedha zinaibiwa we umeshaona kuna mtu kafungwa sababu hakuna sheria za kuwashughulia endeleeni kuwalaumu chadema huku nchi ikiwa inatafunwa bila huruma

Tanzania ina miaka 60 ccm wametawala kuanzia rais, spika na kuwa na wabunge wengi ila lawama za matatizo ya Tanzania anapewa mbowe na chadema haya ndo maajabu ya Tanzania
 
Ningependa sana kuuendeleza mjadala huu kati yetu, lakini nahofia itaonekana kuwa tumeiteka mada nzima kati yetu.
Tupo pamoja sana.
Nieleze tu yafuatayo, na sitarudi tena kubandika chochote.
1. Hadi sasa sijui ni nini hasa kinacho/kilicho tokea CHADEMA na kuwafanya wawe kama walionyeshewa na mvua ghafla tu, na kuyeyusha yale waliyokuwa wamekwisha watangazia waTanzania kuhusu msimamo wao juu ya chaguzi zote zinazokuja hapo mwakani na baadae 2025. Binafsi, sijui sasa hivi msiamamo wao ni upi hasa juu ya hili.

Ingesaidia sana wakajitokeza kama chama na kueleza wanakosimamia wao wakati huu.

Hizi kelele za akina Mwabukusi na sisi wengine wote kwa wakati huu ni kwa sababu hiyo ya kukosekana kwa taarifa toka CHADEMA.
2.
Kwa mwendo huu tunaokwenda nao chini ya CCM, wa kuzima kila aina ya matumaini yanayojaribu kujitokeza kuleta mabadiliko ndani ya nchi yetu, huku wakiendelea na njama zile zile za kufifisha maendeleo ya nchi yetu, hatimaye hali hiyo itazaa njia zisizokuwa za kawaida kuyapata mabadiliko hayo.
 
No adv hauko sahihi.
Chama Chochote ni taasisi kubwa kuliko wewe, na kina mtazamo mpana na mkubwa kuliko wewe.
Tuliko Toka ni mbali na nikubaya zaidi kuliko hapa tulipo, Kuna figisu, na madhira mengi ambayo wapinzani wamefanyiwa, yapo waliyoyavumilia na walionekana mabwege, ila ndo wametufikisha hapa(hata tunasema Kuna chama kikuu Cha upinzani), hakuna jambo la kijinga na la kibwege kama la 2015.
Lakini katika yote wapinzani kujitafuta,.
Ikiwa wataingia bungeni msimu huo ujao, ni rahisi kuforce serikali iingie kwenye mchakato wa katiba mpya.
Siwezi kubeza michakato ya vyama pinzani, ambavyo vipo kimkakati, alafu niungane na wazo lako adv mwambukusi, wazo lenye mihemko na hasira ndani yake, wazo lisilo na mkakati..
No no no... I love chadema, naamini mawazo ya viongozi wangu kuwa na Yana Nia njema. Leo chama kinapitia wakati mgumu Kwa sababu hatuna uwakilishi wowote bungeni(achana na hao chokolaa 19).
 
Inawezekana yuko sawa, kwa mtu anatesoma JF kila siku kila jukwaa na kuwafuatilia vzr na kwz umakini bila ushabiki ,ataona asemacho wakiki
 
Niko na wewe Chief
 
Ubovu wa sheria za kutokuwachukulia hatua waizi ndo ya kulaumiwa
Waizi wa ela kwenye ripoti ya CAG ni waajiriwa huko serekalin na bado wanafanya kazi Mfano hapo unalaumuje wapinzani
Najua mjadala nawe kwangu utakuwa mgumu sana, lakini ngoja nikuulize tu swali kuhusu haya uliyo andika hapa katika hiyo mistari miwili.
Hivi huo "ubovu wa sheria...) unao usema wewe, unaanzia wapi hasa mkuu 'Artifact'?
Hata hizo sheria nzuri zikiwepo, bila ya usimamizi mahsusi nyuma ya hizo sheria, unadhani hali itakuwa tofauti na ilivyo sasa?
Mimi ninakuomba tu uyatafakari haya ninayokuuliza, nina hakika jibu sahihi utalipata mwenyewe huko.
 
Kumbe huyu ni kichaa, mwambie akaandamane, kama ni kila kitu kinafanyika anavyotaka. mbona alishindwa kuandamana. kumbe takataka tupu.

Hawa ni wapinzani wenzako, tumia busara kutoa hoja yako...mpumbavu mkubwa kumbe!
Wewe na Mwenyekiti wako walamba asali ndiyo vichaa, jamaa mkiambiwa ukweli mnapaniki vibaya, too weak
 
So wewe unataka Mbowe, Lema, Lissu, Heche na Sugu waongoze hii nchi? hata mimi ningekuwa usalama wa taifa nisingekubali kamwe hao wahuni wapewe nchi
 
Kumbe huyu ni kichaa, mwambie akaandamane, kama ni kila kitu kinafanyika anavyotaka. mbona alishindwa kuandamana. kumbe takataka tupu.

Hawa ni wapinzani wenzako, tumia busara kutoa hoja yako...mpumbavu mkubwa kumbe!
Huyu jamaa nilimdharau mapema sana nilivyomuona ana Arrogance ya kimalaya.

Nawapa heko akina Mbowe kuwashitukia mapema nakuwatupa kwa dustbin!!
 
Ukweli ni mchungu
Tulisema hakuna opposition Tz
Vyama vyote ni vikundi vya porojo
Kama opposition ipo maswala makuu muhimu wameshindwa kutafuta suluhu kutwa barabarani kama wakimbiza mwenge. Wanachowaza ni ‘siku tukichukua nchi wote watalipa gharama’ wanawaza uongozi tuuu.
Ukimya wao ni kuwapuuza wenye nchi ambao ni walipa kodi.
Cha kushangaza ni ukimya na kelele miiingi..
Ukimya upo kwenye:
Uuzwaji wa Bandari
Uuzwaji sijui iwekezaji KIA
Teuzi zisizo na msingi wala manufaa kwa Taifa

Mgomo baridi wa maandamano
Safari za mkulu
Ubadhirifu wa mali za Umma
Ufusadi uliopitiliza……

Kelele sasa miiiingi
Nyumba ya mwenyekiti
Utajiri wa Mwenyekiti
Endeleeni na join the nini sijui
Operesheni aka mbio za Mwenge
Wajinga ndio waliwao

Hii ni bs of the highest order!

Dr Slaa na mapungufu yake Taifa linamhitaji sana kuliko upinzani
 
TZ kungekuwa na Ugumu kama unavyopotray hapa hao akina Mbowe, Lissu, Lema, na wengineo wangekimbilia kurudi hapa kama mifugo baada tu ja Jiwe kufariki? Si wangebaki tu huko Dubai, Ubelgiji, Canada na kwingineko mnakowaaminisha wajinga kwamba ni kuzuri sana? Walirudi na kusifia sana hapa home, waende hapo tu jirani Rwanda wakatukane hayo matusi yao wanayotukana sasa waone kitachowapata, you guys akili zenu za mbuzi, mabingwa wa kusahau, kwa akili hizi CCM itatawala miaka 100 ijayo TZ!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…