Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Wakili Mwabukusi: Wapinzani hawana afadhali yoyote na CCM, ni wabaya kuliko hata CCM

Wewe huku unalipwa mshahara, unataka wanaume wenzako wakupiganie bure

Na-nikusaidie wanasiasa wote ni wafanyabiashara sababu huwezi pata mda wa kwenda majimboni huko kama wewe ni mwajiriwa mfano angalia mbowe, boniphase, heche wote hawa wana-biashara zao

Huwezi kuwa mwajiriwa huku unafanya siasa sababu hakuna mwajiri atakayekupa ruhusa za kila mara kwenda kufanya mikutano ya siasa huku kazi zinakusubiria mara umekaa korokoroni wanasiasa wote ni wafanyabiashara kama hulikua hulijui
Mwanasiasa kuwa mfanyabiashara sio tatizo, tatizo ni kuitumia siasa kama myaji wa biashara, hapo ndipo penye tatizo, utumwa huanzia hapo.

Nielewe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kama watu wa aina hiyo ndio wapo kwenye siasa zetu, basi tunapotezeana muda. Tumeigeuza siasa kama kijiwe cha wacheza karata.

Hatutasogea popote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ndiyo maana tupo hivi, kama tulivyo sasa; kwa sababu viongozi waliopo kwenye nafasi sioni mwenye 'moto tumboni' kuwa tofauti na marupurupu yanayo patikana kutokana na nafasi wanazo zishikilia.

Tena nizaidi ya hao tunao wazungumzia hapa.
Hawa tulio nao sasa hivi, hata utaifa wao hauna maana yoyote kwao. Mfano mzuri wa kueleza hali ya hawa ni IGA ya Dubai.
Upigaji wa kawaida tu unao tokana na nafasi za uongozi wao, huku wakijali taifa lao, hali hiyo ingeepusha waliyodhamiria kuyafanya chini ya mradi wao wa Dubai. Hawa hata kutuuza hakuwastui chochote.
 
Mwanasiasa kuwa mfanyabiashara sio tatizo, tatizo ni kuitumia siasa kama myaji wa biashara, hapo ndipo penye tatizo, utumwa huanzia hapo.

Nielewe.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Duh!
Hii kazi ya kuwa 'tutor' unaiweza kweli? Naona huyo jamaa hana hata chembe ya 'concept' inayohusu siasa.
Kuliwahi kuwepo kwenye vyuo vyetu vikuu takwa la kusomwa na kila mwanafunzi katika fani zote, lililo itwa 'Developmeny Studies', naona mpango huo ulikufa wenyewe baada ya "walaji na wenye maslahi binafsi" kushika hatamu za uongozi wa nchi yetu.

Matokeo yake ndiyo kama ya huyu unayejibishana naye hapa.
 
Ubovu wa sheria za kutokuwachukulia hatua waizi ndo ya kulaumiwa
Waizi wa ela kwenye ripoti ya CAG ni waajiriwa huko serekalin na bado wanafanya kazi Mfano hapo unalaumuje wapinzani

Miaka nenda rudi CAG anasema fedha zinaibiwa we umeshaona kuna mtu kafungwa sababu hakuna sheria za kuwashughulia endeleeni kuwalaumu chadema huku nchi ikiwa inatafunwa bila huruma

Tanzania ina miaka 60 ccm wametawala kuanzia rais, spika na kuwa na wabunge wengi ila lawama za matatizo ya Tanzania anapewa mbowe na chadema haya ndo maajabu ya Tanzania
 
Inaonekana njia ya kuwaondoa watanzania kwenye huu mkwamo ni kuanzisha chama kipya [ maoni ya wengi humu ndani].

Lakini nionavyo, hicho chama kipya hata kama kitaanzishwa, kiwe kutokea Mbeya au Sumbawanga, kama bado mazingira yanayozunguka siasa zetu yataendelea kubaki kama yalivyo sasa, basi tusitegemee badiliko lolote.

Hicho chama kitaanzishwa, kitakutana na hizi sheria mbovu za uchaguzi, matokeo yake nacho kitakuwa "neutralised" kama ambavyo tunaona Chadema imekuwa neutralised kwa sasa.

Lazima kwanza tuufumue mfumo wa siasa zetu, sheria kandamizi zote ziondolewe, how? hilo swali namuachia kila mmoja ajiulize, wala sio kwa Samia kupeleka muswada bungeni, yale ni maigizo matupu.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ningependa sana kuuendeleza mjadala huu kati yetu, lakini nahofia itaonekana kuwa tumeiteka mada nzima kati yetu.
Tupo pamoja sana.
Nieleze tu yafuatayo, na sitarudi tena kubandika chochote.
1. Hadi sasa sijui ni nini hasa kinacho/kilicho tokea CHADEMA na kuwafanya wawe kama walionyeshewa na mvua ghafla tu, na kuyeyusha yale waliyokuwa wamekwisha watangazia waTanzania kuhusu msimamo wao juu ya chaguzi zote zinazokuja hapo mwakani na baadae 2025. Binafsi, sijui sasa hivi msiamamo wao ni upi hasa juu ya hili.

Ingesaidia sana wakajitokeza kama chama na kueleza wanakosimamia wao wakati huu.

Hizi kelele za akina Mwabukusi na sisi wengine wote kwa wakati huu ni kwa sababu hiyo ya kukosekana kwa taarifa toka CHADEMA.
2.
Kwa mwendo huu tunaokwenda nao chini ya CCM, wa kuzima kila aina ya matumaini yanayojaribu kujitokeza kuleta mabadiliko ndani ya nchi yetu, huku wakiendelea na njama zile zile za kufifisha maendeleo ya nchi yetu, hatimaye hali hiyo itazaa njia zisizokuwa za kawaida kuyapata mabadiliko hayo.
 
No adv hauko sahihi.
Chama Chochote ni taasisi kubwa kuliko wewe, na kina mtazamo mpana na mkubwa kuliko wewe.
Tuliko Toka ni mbali na nikubaya zaidi kuliko hapa tulipo, Kuna figisu, na madhira mengi ambayo wapinzani wamefanyiwa, yapo waliyoyavumilia na walionekana mabwege, ila ndo wametufikisha hapa(hata tunasema Kuna chama kikuu Cha upinzani), hakuna jambo la kijinga na la kibwege kama la 2015.
Lakini katika yote wapinzani kujitafuta,.
Ikiwa wataingia bungeni msimu huo ujao, ni rahisi kuforce serikali iingie kwenye mchakato wa katiba mpya.
Siwezi kubeza michakato ya vyama pinzani, ambavyo vipo kimkakati, alafu niungane na wazo lako adv mwambukusi, wazo lenye mihemko na hasira ndani yake, wazo lisilo na mkakati..
No no no... I love chadema, naamini mawazo ya viongozi wangu kuwa na Yana Nia njema. Leo chama kinapitia wakati mgumu Kwa sababu hatuna uwakilishi wowote bungeni(achana na hao chokolaa 19).
 
HAKUNA TOFAUTI KATI YA CCM NA WAPINZANI, NI WALEWALE" MWABUKUSI

Upinzani na CCM hawana tofauti, kitendo cha kutaka kuingia kwenye uchaguzi bila katiba mpya ni kwa sababu ya maslahi binafsi na sio maslahi ya Taifa, ndio maana kuna chawa wa chama tawala na huku upinzani nako kuna machawa huku kwetu kwenye upinzani

Hakuna mtu yuko tayari kumwambia kiongozi wake kwamba anayoyafanya hayako sawa, hatuna hata mgambo lakini nakuhakikishia sisi wapinzani ni wabaya kuliko hawa walioko madarakani, tunaogopana kuambiana ukweli, sisi na CCM hatuna tofauti kabisa.

Najiuliza kwanini wapinzani tunashindwa kuonyesha msimamo?

kwanini twende kushiriki uchaguzi bila katiba mpya?

Nilishasema kuna biashara ya Demokrasia inafanyika hapa nchini"

Chanzo : Jambo Tv
Inawezekana yuko sawa, kwa mtu anatesoma JF kila siku kila jukwaa na kuwafuatilia vzr na kwz umakini bila ushabiki ,ataona asemacho wakiki
 
Ningependa sana kuuendeleza mjadala huu kati yetu, lakini nahofia itaonekana kuwa tumeiteka mada nzima kati yetu.
Tupo pamoja sana.
Nieleze tu yafuatayo, na sitarudi tena kubandika chochote.
1. Hadi sasa sijui ni nini hasa kinacho/kilicho tokea CHADEMA na kuwafanya wawe kama walionyeshewa na mvua ghafla tu, na kuyeyusha yale waliyokuwa wamekwisha watangazia waTanzania kuhusu msimamo wao juu ya chaguzi zote zinazokuja hapo mwakani na baadae 2025. Binafsi, sijui sasa hivi msiamamo wao ni upi hasa juu ya hili.

Ingesaidia sana wakajitokeza kama chama na kueleza wanakosimamia wao wakati huu.

Hizi kelele za akina Mwabukusi na sisi wengine wote kwa wakati huu ni kwa sababu hiyo ya kukosekana kwa taarifa toka CHADEMA.
2.
Kwa mwendo huu tunaokwenda nao chini ya CCM, wa kuzima kila aina ya matumaini yanayojaribu kujitokeza kuleta mabadiliko ndani ya nchi yetu, huku wakiendelea na njama zile zile za kufifisha maendeleo ya nchi yetu, hatimaye hali hiyo itazaa njia zisizokuwa za kawaida kuyapata mabadiliko hayo.
Niko na wewe Chief
 
Ubovu wa sheria za kutokuwachukulia hatua waizi ndo ya kulaumiwa
Waizi wa ela kwenye ripoti ya CAG ni waajiriwa huko serekalin na bado wanafanya kazi Mfano hapo unalaumuje wapinzani
Najua mjadala nawe kwangu utakuwa mgumu sana, lakini ngoja nikuulize tu swali kuhusu haya uliyo andika hapa katika hiyo mistari miwili.
Hivi huo "ubovu wa sheria...) unao usema wewe, unaanzia wapi hasa mkuu 'Artifact'?
Hata hizo sheria nzuri zikiwepo, bila ya usimamizi mahsusi nyuma ya hizo sheria, unadhani hali itakuwa tofauti na ilivyo sasa?
Mimi ninakuomba tu uyatafakari haya ninayokuuliza, nina hakika jibu sahihi utalipata mwenyewe huko.
 
Kumbe huyu ni kichaa, mwambie akaandamane, kama ni kila kitu kinafanyika anavyotaka. mbona alishindwa kuandamana. kumbe takataka tupu.

Hawa ni wapinzani wenzako, tumia busara kutoa hoja yako...mpumbavu mkubwa kumbe!
Wewe na Mwenyekiti wako walamba asali ndiyo vichaa, jamaa mkiambiwa ukweli mnapaniki vibaya, too weak
 
Tunaungana kwenye kushiriki chaguzi za haki, sio hizo za kwenda kupotezeana muda kisha kupewa viti viwili vitatu vya hisani ili kuhada umma na dunia kuwa Kuna demokrasia.

Ni hivi, tumechoka kuongozwa na chama hiki hiki miaka yote tena kwa shuruti. Tunataka chaguzi za haki anayeshinda ashinde kihalali, na sio kupotezea wanaume muda wao kwenye mistari ya kura, wakati mnalazimisha kuongoza kizazi kilichowachoka. Serekali inaweza kuundwa na watanzania wengine, sio lazima ccm bila ridhaa ya umma.
So wewe unataka Mbowe, Lema, Lissu, Heche na Sugu waongoze hii nchi? hata mimi ningekuwa usalama wa taifa nisingekubali kamwe hao wahuni wapewe nchi
 
Kumbe huyu ni kichaa, mwambie akaandamane, kama ni kila kitu kinafanyika anavyotaka. mbona alishindwa kuandamana. kumbe takataka tupu.

Hawa ni wapinzani wenzako, tumia busara kutoa hoja yako...mpumbavu mkubwa kumbe!
Huyu jamaa nilimdharau mapema sana nilivyomuona ana Arrogance ya kimalaya.

Nawapa heko akina Mbowe kuwashitukia mapema nakuwatupa kwa dustbin!!
 
Slaa anamdanganya sana huyu jamaa
Kwenye maisha hamnaga short-cut hasa kwenye mambo yanayohusu itikadi kama siasa

Kama anajiamini aanzishe chama chake asitake kutumia watu kama mgongo wa kufikia malengo yake maisha sio marahisi hivyo yaani chadema waache agenda zake wamfuate yeye mbona ni kituko na kichekesho
Ukweli ni mchungu
Tulisema hakuna opposition Tz
Vyama vyote ni vikundi vya porojo
Kama opposition ipo maswala makuu muhimu wameshindwa kutafuta suluhu kutwa barabarani kama wakimbiza mwenge. Wanachowaza ni ‘siku tukichukua nchi wote watalipa gharama’ wanawaza uongozi tuuu.
Ukimya wao ni kuwapuuza wenye nchi ambao ni walipa kodi.
Cha kushangaza ni ukimya na kelele miiingi..
Ukimya upo kwenye:
Uuzwaji wa Bandari
Uuzwaji sijui iwekezaji KIA
Teuzi zisizo na msingi wala manufaa kwa Taifa

Mgomo baridi wa maandamano
Safari za mkulu
Ubadhirifu wa mali za Umma
Ufusadi uliopitiliza……

Kelele sasa miiiingi
Nyumba ya mwenyekiti
Utajiri wa Mwenyekiti
Endeleeni na join the nini sijui
Operesheni aka mbio za Mwenge
Wajinga ndio waliwao

Hii ni bs of the highest order!

Dr Slaa na mapungufu yake Taifa linamhitaji sana kuliko upinzani
 
Vyama vya Upinzani vilivyosajiliwa vipo 19 kama sijakosea, WHY Chadema????

Ninachokiona hapa yeye (Mwabukusi) ndiye mwenye tamaa. Mnapokuwa vitani kwanini uanze kuwashambulia wenzako badala ya adui?? Yeye (Mwabukusi) ndiye anaetumiwa na wapenda madaraka wa CCM kuwashambulia Wapizani.

Chama Makini kama Chadema hakiwezi kuweka rehani maisha ya Watz kisa madaraka. Siku ikiwadia Watz wakaamua wenyewe kuyaweka maisha yao rehani kwa Ukombozi wa Nchi Yao sawa, hapo Chadema watakuwa tayari kuwaunga mkono.

Kingine ni kwamba siku Watz watakapoacha UNAFIKI basi wataweza kuwapata Viongozi wenye Mapinduzi ya FIKRA watakao waongoza kwenye Ukombozi wa kweli wa Nchi yao.
TZ kungekuwa na Ugumu kama unavyopotray hapa hao akina Mbowe, Lissu, Lema, na wengineo wangekimbilia kurudi hapa kama mifugo baada tu ja Jiwe kufariki? Si wangebaki tu huko Dubai, Ubelgiji, Canada na kwingineko mnakowaaminisha wajinga kwamba ni kuzuri sana? Walirudi na kusifia sana hapa home, waende hapo tu jirani Rwanda wakatukane hayo matusi yao wanayotukana sasa waone kitachowapata, you guys akili zenu za mbuzi, mabingwa wa kusahau, kwa akili hizi CCM itatawala miaka 100 ijayo TZ!
 
Back
Top Bottom