Ni kweli anachosema Adv. Mwabukusi, siasa zetu kwa kiasi kikubwa zimegeuzwa kuwa ajira, na wala sio kuwatumikia wananchi kama walivyozoea kutudanganya.
Ndio maana unawaona wale wanawake 19 bado wako bungeni mpaka leo bila aibu yoyote, wanakula bure kodi za watanganyika, huku ajabu wakiwa bungeni nao wanajidai kulaani upotevu wa fedha serikalini, wao hawajioni!..
Huku wengine nao wameshasahau kama msimamo wa chama chao ni kutoshiriki uchaguzi, mpaka Katiba Mpya ipatikane, wao wameshaanza kusema watahakikisha wanawaondoa wabunge wa CCM majimboni mwao, hii kauli ni sawa na tusi kwa mtu mwenye spirit ya Adv. Mwabukusi.
Wapiga kura tunageuzwa mtaji wa wanasiasa bila kujua, sometime tuna siasa za kisanii sana, za kupitisha muda ili wale na familia zao, kwa wale walioupata utajiri kupitia siasa, kamwe hawawezi kuuacha uchaguzi upite mpaka waisubiri Katiba Mpya ipatikane.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app