Hivi, katika kumfahamu kwako Mzee Kikwete uliwahi kumshuhudia akiweka hadharani vyanzo vyake vya mapato?
Uliwahi kumuona yeye binafsi akiweka bayana iwe mitandaoni ama magazetini, biashara zake?
Lakini si tunajua vyanzo vyake vingi tu kulingana na tetesi mitaani, ndugu na Jamaa ama vinywa vya mashabiki wake (Chawa?)??
Hata Mwigulu mwenyewe tetesi za umiliki wake wa team ya mpira, bus za usafiri mikoani na mengineyo alishawahi kusimama hadharani na kujitaja bayana?
Wengi wa wanasiasa hapa TZ hasa kutoka CCM na vyama vichache vya upinzani, wakimiliki mali na biashara kubwa ama ndogo tumeshuhudia wakiwatumia marafiki/ business partners ama ndugu kusimama badala yao,……Kwanini unadhani they go through so much trouble?
Ushauri wa Jamaa hapo juu ni wa dhahabu sana, ni ubinafsi pekee utakufanya uuone ni mbaya.
Hata huu mtifuano unaoendelea CCM huwaoni wahusika halisi wakichezesha karata zao, utawaona wachezaji wao tu.