Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Wakili Peter Madeleka amekamatwa na Polisi Arusha,

Amekamatwa mara baada ya High Court Arusha kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Taarifa zaidi kukujia

========
Tweet yake ya mwisho ilikuwa .... Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha Leo tarehe 17 Julai 2023 IMEFUTA PLEA BARGAIN iliyoingiwa Kati ya DPP na PETER MADELEKA. Hata hivyo RCO ARUSHA ametuma ASKARI WANIKAMATE nikiwa Mahakamani. Bado sijatoka Kwa JAJI.

Baadhi ya kauli zake kuhusu sakata la bandari

1. Wakili Madeleka: Rais Samia nakusihi, Futa huu Mkataba wa Bandari
2. Wakili Madeleka: Dubai sio nchi kama ilivyo Zanzibar hivyo haiwezi kuingia mkataba na nchi nyingine
3. Wakili Madeleka ataka Jaji Biswalo achunguzwe suala zima la Plea Bargain
Kwamba sijaelewa kwamb imefutwa na kutakiwa kutumikia kifungo au imefutwa na SAS alipe pesa zote za plea bargain

Sijaelewa mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Madeleka kutoka Polisi alifungua kampuni yake ya UWAKILI. Halafu kumbuka Mrs Madeleka alikuwa ni Mrumishi wa IMMIGRARION Mkoa wa Arusha akiwa kitengo kinachohusiana na wahamiaji haramu.

Kesi zote ambazo Peter Madeleka alikuwa anashinda zilikuwa zinaharibiwa na mkewe ofsini. Na wahamiaji haramu wengi alikuwa anawasukuma kwa mumewe kwa ajili ya kutetewa mahakamani.

Hivyo Madeleka na mkewe walihujumu sana jeshi la Immigration Arusha hadi baadaye uongozi wa Makao Makuu ukagundua.

Kilichofuata ni mke wa Madeleka kuhamishwa kitua na hatimaye kuacha kazi Immigration.

Na hiyo ndiyo sababu kubwa ya bifu la Madeleka dhidi ya Makakkala, CG wa Immigration.

Madeleka siyo msafi hata kidogo, ndiyo maana alikubali kusaini "plea bargaining"
Hili sakata la huyu wakili nimewai kulisiki Ni tapeli mmoja mzuri San akishirikiana na mke wake

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Watu wengi wanashindwa kuelewa jambo moja, kilichotokea kwa Madeleka kukamatwa ni sawa sababu faili lake limerudishwa polisi wao warudishe kwa DPP alafu kesi iendelee pale ilipoishia.

Sasa mambo ya Tume ya kuchunguza haki jinai hapa yanaingia kwa udogo sana sababu Madeleka hajashinda kesi ya msingi bali ni ombi tu linalorudisha ile kesi ya msingi.

Kwa ufupi sana ni kwamba Madeleka ni mtuhumiwa kwa sasa, na ni mtuhumiwa kwa ile ile kesi yake ya awali ambayo kimsingi yeye mwenyewe ndio ameona sasa bora akapambane na ile kesi ya awali kwa kupinga alichokubaliana na DPP.

kwa ufupi sana jambo lake limekaa hivyo.
Kesi yake ya awali ilkuwa ipi mkuu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Madeleka kutoka Polisi alifungua kampuni yake ya UWAKILI. Halafu kumbuka Mrs Madeleka alikuwa ni Mrumishi wa IMMIGRARION Mkoa wa Arusha akiwa kitengo kinachohusiana na wahamiaji haramu.

Kesi zote ambazo Peter Madeleka alikuwa anashinda zilikuwa zinaharibiwa na mkewe ofsini. Na wahamiaji haramu wengi alikuwa anawasukuma kwa mumewe kwa ajili ya kutetewa mahakamani.

Hivyo Madeleka na mkewe walihujumu sana jeshi la Immigration Arusha hadi baadaye uongozi wa Makao Makuu ukagundua.

Kilichofuata ni mke wa Madeleka kuhamishwa kitua na hatimaye kuacha kazi Immigration.

Na hiyo ndiyo sababu kubwa ya bifu la Madeleka dhidi ya Makakkala, CG wa Immigration.

Madeleka siyo msafi hata kidogo, ndiyo maana alikubali kusaini "plea bargaining"
HV huyu wakili Ana akili timamu kwli unajuwa kbsa una kesi na mamlakalkn uishi kuokozoaa HV hz Ni akili si angetulia kuliko kujifanya kisebusebu ona SAS watakacho mfanya yaani litafungwa kisembe sana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Alianza mdude,
Kafata mdeleka,
Bado yule wakili wambeya.

List inaendelea, yote sababu ya bandari
 
Itabidi kuangalia upya vigezo vya polisi. Badala ya kuifanya kazi ya polisi kuwa ni kazi ya watu wenye uwezo mdogo wa akili iwe ni kazi ya watu wenye upeo mkubwa, weledi na watu wenye akili ya kutosha.

Mkiwa na polisi wasiojitambua wanaweza kuifanya nchi kuonekana ni ya ajabu.
Kuna mtu anajitambua mbele ya maelekezo?
 
Hatari sana juzi ripoti ya Haki Jinai aliyotoa jaji mstaafu Mohamed Othman Chande na baadaye kauli ya mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Samia Suluhu Hassan kuwa taasisi na viongozi waliopo katika mfumo wa haki jinai wabadilike bado haijaweza kuwafikia watendaji waliopo katika kuhakikisha haki ndani ya mfumo wa haki jinai Tanzania

View attachment 2690768
Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 15 July 2023 amepokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai kutoka kwa Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Othman Chande, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Taasisi zibadilike huku anazipa maelekezo ya ajabu? Kuna taasisi imejituma?
 
Itabidi kuangalia upya vigezo vya polisi. Badala ya kuifanya kazi ya polisi kuwa ni kazi ya watu wenye uwezo mdogo wa akili iwe ni kazi ya watu wenye upeo mkubwa, weledi na watu wenye akili ya kutosha.

Mkiwa na polisi wasiojitambua wanaweza kuifanya nchi kuonekana ni ya ajabu.
Pascal Mayalla naomba mkiwa huko kwenye mikutano ya chama muwe mnashare huu ujumbe,

Tanzania ni nchi yenye polisi wa ajabu na sipati picha kama hawa polisi wadogo akili zao zipo hivi je viongozi wake uwezo wao ukoje
 
alitoa elimu ya mkataba,

Kwa hiyo kosa lake ni kuelimisha wananchi wa Tanganyika juu ya mkataba, wakaona walale nae mbele. Maigizo kutoka juu yameanza sio
SIMBA wa YUDA amerudi. Itakuwa alikuwa amekaa ngoxi ya, kondoo sasa taratibu inatoka.
 
Wakili Peter Madeleka amekamatwa na Polisi Arusha,

Amekamatwa mara baada ya High Court Arusha kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Taarifa zaidi kukujia

========
Tweet yake ya mwisho ilikuwa .... Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha Leo tarehe 17 Julai 2023 IMEFUTA PLEA BARGAIN iliyoingiwa Kati ya DPP na PETER MADELEKA. Hata hivyo RCO ARUSHA ametuma ASKARI WANIKAMATE nikiwa Mahakamani. Bado sijatoka kwa JAJI.

Baadhi ya kauli zake kuhusu sakata la bandari

1. Wakili Madeleka: Rais Samia nakusihi, Futa huu Mkataba wa Bandari
2. Wakili Madeleka: Dubai sio nchi kama ilivyo Zanzibar hivyo haiwezi kuingia mkataba na nchi nyingine
3. Wakili Madeleka ataka Jaji Biswalo achunguzwe suala zima la Plea Bargain

---
Wakili wa kujitegemea nchini, Peter Madeleka amekamatwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Jumuishi cha utoaji haki baada ya kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Madeleka kabla ya kukamatwa alilazimika kung'ang'ania kwa zaidi ya dakika 30 katika chumba cha Mahakama cha Jaji Aisha Bade ambaye awali ndiye alitoa maamuzi katika kesi yake ya kupinga makubaliano ya kukiri kosa ‘Plea bargaining.’

Wakili Madeleka aliwasilisha maombi namba 80 ya mwaka 2021 kutokana na kesi aliyokuwa amefunguliwa ya uhujumu uchumi namba 40/2020.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi iliyotolea uamuzi Aprili 27 mwaka huu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, wakili Madeleka alikuhukumiwa kulipa faini ya Sh200,000 au kutumikia kifungo cha nje cha miaka mitatu.

Katika uamuzi huo, pia alilipa Sh2 milioni kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ili kuondolewa shauri hilo baada ya kulazimika kukiri makosa.

Hata hivyo wakili huyo alifungua kesi Mahakama Kuu, kupinga uamuzi wa Hakimu Mkazi Arusha, kumtia hatiani katika kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili Madeleka pia aliiomba Mahakama Kuu itoe amri ya kurejeshewe faini ya Sh200,000 aliyolipa kwa sababu mchakato mzima ulikuwa ni kinyume cha sheria.

Amesema baada ya hukumu hiyo, alilazimishwa kufanya makubaliano ya kukiri kosa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na baada ya kuachiwa alikata rufaa.

Leo mara baada ya kusomwa kwa hukumu yake na wakili huyo alibakia kwenye chumba cha mahakama hadi alipofika Wakili wake, Simon Mbwambo na wanahabari ndipo alipotoka kwenye chumba hicho na kukamatwa na polisi.

Awali Madeleka amesema kuwa Jaji Bade amekubaliana na hoja yake kuwa upande wa mashtaka kabla ya kuingia katika makubaliano ya kukiri makosa ulipaswa kuwa na ushahidi wa kosa alilotenda

“Hata hivyo, Jaji Bade ameagiza kesi hiyo kuanza upya kusikilizwa katokana na baadhi ya upungufu katika shauri hilo” amesema

Akizungumzia kuhusu kukamatwa kwa mteja wake, Wakili Simon Mbwambo, amesema hajui kosa analokabiliwa nalo wakili Madeleka.

"Sijui kosa naona polisi wamemkata na wanampeleka Ofisi ya RCO (Mkuu wa Upelelezi Mkoa Arusha) kwa mahojiano, labda wanataka kuanza upya kusikiliza kesi hii ya leo," amesema.

Polisi waliomkamata wakili Madeleka hata hivyo hawakuwa tayari kuelezea tuhuma zake na kuwataka wanahabari kufuata taratibu za kupata habari kwa kuzungumza na viongozi wa juu wa polisi.

Wakili Madeleka katika siku za karibuni amekuwa katika harakati za kupinga Makubaliano ya uwekezaji wa bandari kati ya Tanzania na Dubai na wiki iliyopita alikuwa jijini Dar es Salaam katika mkutano ulioandaliwa na Balozi mstaafu Dk Wilibroad Slaa na Wakili Boniface Mwabukusi wakielezea ubovu wa makubaliano hayo.
Warudishe pesa yake sasa ,nchi ina watu wa ajabu sana hii
 
@PMadeleka alifanya plea bargain halafu karudi kuichallenge tena kama haikuwa voluntary. Ameshinda kesi na plea bargain kufutwa so kesi inaanza upya ya kwake

Haku calculate vizuri strategy yake and he chose the wrong time to challenge this
Labda ana uhakika wa kushinda kesi kama anajua jamuhuri haina ushahidi wa kutosheleza lakini atakuwa ashaumia mpaka ije iishe
 
Back
Top Bottom