Pamoja na ukweli kwamba hakuna Mtu yeyote aliyehukumiwa kunyongwa na Mahakama za Tanzania ambaye atanyongwa , kutokana na "ucha mungu wa marais" wa nchi hii na kushindwa kusaini vifo vya waliohukumiwa kunyongwa , lakini binafsi sioni uhalali wowote wa Mahabusu kuchanganywa na Wafungwa .
Pamoja na ukweli kwamba lengo la Mamlaka kumchanganya Mbowe na waliohukumiwa kunyongwa ni mbinu ya kizamani na ya kishamba ya Kumtisha Mwamba Mbowe asiyetishika , lakini sioni uhalali wa Kisheria kwa Mahabusu kuchanganywa na Wafungwa , ni vema sheria za nchi zikaheshimiwa kidogo , hii ni kwa sababu WHAT GOES AROUND COMES AROUND .
Tunaomba Wanasheria waliopo hapa jf watutolee ufafanuzi wa Jambo hili