Wakili Peter Madeleka umekuwa lini msafi hadi umfundishe Rais kazi?

Wakili Peter Madeleka umekuwa lini msafi hadi umfundishe Rais kazi?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Naandika hapa nikiwa na maumivu binafsi juu ya clip ya wakili Peter Madeleka. Sipingani na hoja alizotoa kwa sababu nyingi zina mashiko na mjadala aliouibua unatija kwa haki jinai Tanzania.

Kilichonisukuma kuandika ni baada yakumsikiliza akitamka haki kwenye vyombo vya habari akijitapa kwamba ameonewa na kubambikiwa kesi. Sikatai yaweza kuwa ni kweli alibambikiwa kesi ila yeye mwenyewe angeanza kujiuliza amedhulumu haki ngapi za watu akiwa polisi.

Mimi Ni. Muhanga wa matendo ya rushwa na ukatili aliyofanya huyu mtoto kipindi akiwa polisi. Rafiki yetu alisingiziwa kesi. Huyu bwana kipindi hicho ni askari Polisi akawa anachunguza shauri lile. Jambo la Kwanza alilolifanya ni kinyume na hotuba yake alikataa kutoa dhamana kwa huyo ndugu yetu baada ya mlalamikaji kuwalipa fedha. Ndugu yangu yule alikaa maabusu karibu siku tano uchunguzi unaendelea. Leo hii anakuja kulalamika kuwekwa mahabusu siku kumi na moja, kwanini yeye alipokuwa na dhamana yakutoa amri apendavyo hakuzingatia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ndani ya saa ishirini na nne?

Hoja ya pili anasema mtuhumiwa apaswi kupelekwa mahakamani kama ushahidi bado, wewe Peter wewe leo ndio umeyajua haya?Au baada yakuwa wakili ndo umejifunza haya?

Kwanini ulipokuwa polisi ukuyatekeleza haya? Au hizo sheria umezisoma gerezani? Ndugu yangu kesi yake ilichukua mwaka na miezi miwili ninyi wapelelezi mkisema ushahidi haujakamilika na bado kesi yenyewe mlikuja kuloose interest after a lot of suffering. Nikukumbushe tu hata dhamana haukutoa bure, ninyi mlihitaji fedha. Usafi wako upo wapi?

Unatuambia mke wako amefukuzwa kazi na watoto wanateseka,pole ila kumbuka namna ambavyo ulidhulumu haki za watu. Yamkini baadhi ya wateja wako kipindi kile waliacha kusomesha wakakulipa ujira wa mwea ili kesi zao ziishe mikononi mwako. Hao watoto ambao hawakusoma kipindi hicho kwa sababu yenu yakupokea rushwa Wana tofauti gani na watoto wako?

Unapotaka Rais akusikilize nenda na mikono salama na safi si unaenda na mikono michafu. Umetoka huko na sijui lini umeanza kujitegemea lakini naamini Mali na vitu ulivyo navyo vinadhuluma ndani yake hivyo nikuombe wewe na wasomi wengine wa Tanzania. Ninyi ndio mmeliaribu Taifa, mngesimama katika haki kwa nyadhifa zenu ndogo mlizokuwa nazo wakubwa zenu wangebadilika lakini mnatenda maovu mkiwa kwenye uniform mkirudishwa uraiani mnaanza kulia lia kutaka haki. Mmetutesa sana badilikeni.

Nawaonea huruma kwa mliyopitia lakini niombe Mhe. Rais kwa watu kama Peter na kwa mwaka mmoja na kitu tuliosota kutafuta haki mikononi mwake akigoma na kujibu shit sidhani kama anayo mikono safi yakuleta hoja ukaifanyia maamuzi chuja sana. The guy is more than arrogant, much know na dharau nyingi lazima tuseme ukweli watu wabadilike. Tusipowasema na kuwakanya ndio Hawa wanapata madaraka wanatuumiza then wakipata shida wanarudi kulia lia.

Kwa vyombo vya habari, fanyeni uchunguzi kuhusu watu kama wakina Peter, iambieni jamii ukweli ili kuwafunga mdomo watu wengine wanaolia kwa ajili ya familia zao badala yakulia kwa ajili ya Taifa. Msipofundisha adabu wakina Peter tutasikitika nao Leo ila kesho wakipata madaraka watatufanya kibaya zaidi ya walichofanywa. Hawa wavaa suti si watu wakuamini wanatumia elimu zao vibaya omba usikutane nao kwenye kutafuta haki utajuta.

Leo huyu mtu ukimuuliza kesi ngapi amewahi kusaidia mtu sidhani kama utapata, the guy is after money...

Pole Peter ila tambua uliutia uchungu moyo wangu na moyo wa familia yetu ukiwa polisi ukitimiza majibu kinyume kabisa na kanuni za jeshi hilo. Omba radhi safisha mabaya ndipo ujitokeze kukemea maovu. Usitumie vyombo vya habari kama kinga yakutokusemwa, ulikosea ukatudhulumu lazima tukuseme ujifunze kuheahimu watu.

Kila la kheri wewe na familia yako.
 
Nilisikiliza ile clip na baada yakusoma hii mada nimerudi kuisikiliza upya. Pole sana mtoa mada,pole kwa uchungu ulionao, pole kwa wale wote waliokumbana na utendaji wa wakili huyu aliyetuletea simanzi kwenye mitandao kumbe yeye mwenyewe ni zao la uvunjifu wa haki.

Nadhani ipo haja Hawa watu wanaokuja mitandaoni kulalamika kwa awamu ya sita tuwamulike vizuri,tusiwe wepesi kuwaamini na kusikitika nao. Kama huyu Bwana alikuwa anafanya kazi polisi na kweli kwenye video amekiri ni askari Polisi na mke wake yawezekana anatoka Uhamiaji ndo maana anasema walimfanya aache kazi, Hawa watu nivigumu kuwa wasafi.

Kazi ya Polisi na uhamiaji zinajulikana, kumpata mtu ambaye achukuhi rushwa Ni bahati sana.

Nimshauri Mhe. Samia Suluhu Hassan achukue taadhari kwa watu kama hawa, huyu ni mwananchi mmoja amejitokeza kuonyesha madhila waliyopitia mikononi mwa wakaili huyu kipindi yupo jeshi la Polisi, je ni wangapi amewadhulumu? Kwanini tuamini yeye amebambikiwa kesi?

Lakini niende mbali zaidi kwenye taarifa yake, makosa ya Uhamiaji yana dhamana na uhamiaji haina mamlaka kuchunguza kesi za uhujumu uchumi yawezekana huyu kiumbe wenzake polisi walimchoka nakutaka kumfukuza kazi kwa mwendelezo wa tuhuma za mtoa mada. Lakini mwisho ukiona polisi anatoka kwenye media nakumwekeza Mhe. Rais kazi tambua Kuna shida kichwani mwake.

Pole Tena mtoa mada lakini ningependa sana tupate story au profile za huyu wakili.....Kuna vitu havipo sawa
 
Kazi ya polisi ni ngumu sana kujikuta upo sahihi katika Utumishi wako wote, ni kazi yenye kuhitaji uwe na roho mbaya saa nyingine nahisi Ina laana kubwa sana.

Jamaa alijisahau kabisa kwamba nae alifanya haya maushenzi, yani ni kama DPP siku ambayo angejikuta nae yupo kwenye mikono ya DPP mwingine. Hapo ndio angepata picha namna alivyo katili.

Siku zote katili akitendewa ukatili huwa mlalamishi sana na huwa anatafuta public sympathy.
 
Nilishtuka kulisoma tweet ya Zito nikadhani nafananisha majina, mara Erick Kabendera naye akatweet. Kuiona clip na sura nabaini nimtesi wetu ndo wanamwonea huruma, nikasema nadhani Hawa akina Zitto wanajudge kulingana na wanayosikia awatafuti undani.

Inawezekana zito ni mmoja wa wahanga wa huyu mtu, Ni mtu asiyeweza kuvumilia nakusiliza, anapenda kuamini yupo sahihi wakati wote. Tulimbebembeleza jipe muda usikilize ukweli alikataa katu katu akaandika maelezo kwa namna alivyoona yyeye. Nimwombe Erick na wengine waliomsikiliza watafute kumjua huyu kiumbe ana elewa haki anayoizungumza?

Lakini pia Hawa watu wamekulia maisha ya Raha CID awajui shida, wamejiweka first class flan hivyo wakija wakitusomea vifungu vya katiba tunaamini Ni watu kweli, kutana nao kwenye kumi na nane uone ukwapuaji wao.

Nimekasirika sana kuona huyu mtu naye anahubiri haki. For the first time najilazimisha kuuzunika na wanaouzunika......huyu binadamu alitutesa sitamsau. Aombe radhi na kabla ajamtuhumu hata DPP akumbuke naye aliwahi kufanya haya ya DPP.kunyima bail, kubambikia kesi, kupokea fedha nakuweka mifuko binafsi( Bora DPP unalipa kwa control number yeye alikuwa ananunulia tofali) nk

Watu wa kariba hii tusisikitike nao, Mhe. Rais Hawa badala yakuwasikiliza elekeza wachunguzwe ujue undani wao wasitumie ofisi yako kukufundisha kazi kwakuwatupia mawe wasiohusika.....waje na mikono misafi
 
Pole sana, ila mchafu haimaanishi hawez kua msafi maan haya ndo maisha ya kitanzania. Wengi sana wana shutumiwa kwa mambo ovu mengi sana juu ya raia but mwisho wa cku watashangiliwa na kupewa sifa kedekede.
 
Nilisikiliza ile clip na baada yakusoma hii mada nimerudi kuisikiliza upya. Pole sana mtoa mada,pole kwa uchungu ulionao, pole kwa wale wote waliokumbana na utendaji wa wakili huyu aliyetuletea simanzi kwenye mitandao kumbe yeye mwenyewe ni zao la uvunjifu wa haki...

Niliposikiliza ile crip nilimuunga mkono lakini baada ya kusoma hapa nimegundua kuwa ni shetani ndie alinishawishi kuwa na huruma nae, watu kama hawa wapo wengi sana kuna mmoja sitomsahau lakini eti nae ni Jaji na kanifanya nimchukie hata aliyemchagua bure bila sababu ,

Hivi watu kama hawa kwanini Rais kwa kutumia madaraka yake asifute hicho kichaka chake cha uwakili ili watu tuwe na amani? huyu bwana na crip yake ni kama anakata rufaa na kuomba haki na ktk rufaa kuna kushinda au rufaa kutupwa hivyo Mama Rais wetu naomba mjibu huyu wakili fake kwa kufuta cheti chake cha uwakili arudi uraiani kabisaaaa akalime huko kwao usukumani kwani tumechoka nao
 
Back
Top Bottom