Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 22,714
- 34,545
Yeye mwenyewe anatafunwa na karma ya kuunga mkono udhalimuMzee wa karma
Ova
Yeye mwenyewe anatafunwa na karma ya kuunga mkono udhalimuMzee wa karma
Ova
Pole Sana Bite. Pole Sana. Watu kama hawa wanaonea watu Sana halafu wanajua kweli kujitiisha huruma mbele ya macamera. Watu wa hii kaliba ni watu wa fitna na majungu. Watu wabinafsi.Nilishtuka kulisoma tweet ya Zito nikadhani nafananisha majina, mara Erick Kabendera naye akatweet. Kuiona clip na sura nabaini nimtesi wetu ndo wanamwonea huruma, nikasema nadhani Hawa akina Zitto wanajudge kulingana na wanayosikia awatafuti undani...
I can read feelings zako mtoa mada ulipokuwa unaandika hii post.Naandika hapa nikiwa na maumivu binafsi juu ya clip ya wakili Peter Madeleka. Sipingani na hoja alizotoa kwa sababu nyingi zina mashiko na mjadala aliouibua unatija kwa haki jinai Tanzania...
hawasomi hawa mawakili, hata wakifunguliwa uhuru wakija na hoja kama za huyu inspector wa polisi wa zamani, hakika wanasheria wa tz watakuwa wanaonekana vilaza.Katika moja ya jambo ambalo utawala wa awamu ya tano ulifanikiwa ni kudhibiti masuala ya haki na kisheria. Mawakili wengi ni wa hovyo sana.
Sent from my HRY-LX1T using JamiiForums mobile app
Dah! Kwa haya uliyoandika kulikuwa na ulazima wa Awamu ya Tano iliyokuwa imeji sacrifice kutetea haki za wanyonge kumshughulikia!Naandika hapa nikiwa na maumivu binafsi juu ya clip ya wakili Peter Madeleka. Sipingani na hoja alizotoa kwa sababu nyingi zina mashiko na mjadala aliouibua unatija kwa haki jinai Tanzania...
Mitano tenaKatika moja ya jambo ambalo utawala wa awamu ya tano ulifanikiwa ni kudhibiti masuala ya haki na kisheria. Mawakili wengi ni wa hovyo sana.
Sent from my HRY-LX1T using JamiiForums mobile app
Well said my friend!!!DPP ni kweli ofisi yake ilitesa watu na ni kweli mtu ana mashataka kadhaa..wizi..kudanganya sijui kutoa taaarifa za uongo mwishoni wanawake Money laundering..
IMEUMIZA WATU SANA..kingine kuna watu walikua wanashinda kesi..Ofisi ya DPP inarudisha kesi hiyo Mahakamani Mtuhumiwa anashinda mara 3 mpaka mara 4 bado anafunguliwa kesi hiyo hiyo kwa Makosa yake yale na mashahudi wale wale...Kwanini mfanye hivi??? Mnamkomoa mtu mnamtesa na kuna wanasheria Wa mashirika ya umma nao wameitumia ofisi hiyo ya DPP kutesa watu sana ..
Analalamikia kukaa mahabusu siku11? huyu alitakiwa kukaa miaka 11 mahabusu. pambaf!Mimi Ni. Muhanga wa matendo ya rushwa na ukatili aliyofanya huyu mtoto kipindi akiwa polisi. Rafiki yetu alisingiziwa kesi. Huyu bwana kipindi hicho ni askari Polisi akawa anachunguza shauri lile. Jambo la Kwanza alilolifanya ni kinyume na hotuba yake alikataa kutoa dhamana kwa huyo ndugu yetu baada ya mlalamikaji kuwalipa fedha. Ndugu yangu yule alikaa maabusu karibu siku tano uchunguzi unaendelea. Leo hii anakuja kulalamika kuwekwa mahabusu siku kumi na moja, kwanini yeye alipokuwa na dhamana yakutoa amri apendavyo hakuzingatia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ndani ya saa ishirini na nne?
Kuna kamsemo kakiswahili kanasema Mtenda Akitendewa Huhisi kuonewaKazi ya polisi ni ngumu sana kujikuta upo sahihi katika Utumishi wako wote, ni kazi yenye kuhitaji uwe na roho mbaya saa nyingine nahisi Ina laana kubwa sana.
Jamaa alijisahau kabisa kwamba nae alifanya haya maushenzi, yani ni kama DPP siku ambayo angejikuta nae yupo kwenye mikono ya DPP mwingine. Hapo ndio angepata picha namna alivyo katili.
Siku zote katili akitendewa ukatili huwa mlalamishi sana na huwa anatafuta public sympathy.
lakini pia na kuhusu wewe hatujasikia upande wake. Usije kuwa unamsingizia ilhali mtu wako alikuwa na hatia kweli.Nilishtuka kulisoma tweet ya Zito nikadhani nafananisha majina, mara Erick Kabendera naye akatweet. Kuiona clip na sura nabaini nimtesi wetu ndo wanamwonea huruma, nikasema nadhani Hawa akina Zitto wanajudge kulingana na wanayosikia awatafuti undani...
Yaliyopita si ndwele alipokuwa Polisi alikuwa anatekeleza amri ya Serikali lakini leo yuko kwenye mhimili wa haki,tumsamehe kwa yaliyopita tushike hayo mazuri aliyo nayo kwa wakati huu,kumbuka Saulo kabla hajawa Paulo alikuwaje?(Matendo Sura ya 9)Naandika hapa nikiwa na maumivu binafsi juu ya clip ya wakili Peter Madeleka. Sipingani na hoja alizotoa kwa sababu nyingi zina mashiko na mjadala aliouibua unatija kwa haki jinai Tanzania.
Kilichonisukuma kuandika ni baada yakumsikiliza akitamka haki kwenye vyombo vya habari akijitapa kwamba ameonewa na kubambikiwa kesi. Sikatai yaweza kuwa ni kweli alibambikiwa kesi ila yeye mwenyewe angeanza kujiuliza amedhulumu haki ngapi za watu akiwa polisi.
Mimi Ni. Muhanga wa matendo ya rushwa na ukatili aliyofanya huyu mtoto kipindi akiwa polisi. Rafiki yetu alisingiziwa kesi. Huyu bwana kipindi hicho ni askari Polisi akawa anachunguza shauri lile. Jambo la Kwanza alilolifanya ni kinyume na hotuba yake alikataa kutoa dhamana kwa huyo ndugu yetu baada ya mlalamikaji kuwalipa fedha. Ndugu yangu yule alikaa maabusu karibu siku tano uchunguzi unaendelea. Leo hii anakuja kulalamika kuwekwa mahabusu siku kumi na moja, kwanini yeye alipokuwa na dhamana yakutoa amri apendavyo hakuzingatia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa ndani ya saa ishirini na nne?
Hoja ya pili anasema mtuhumiwa apaswi kupelekwa mahakamani kama ushahidi bado, wewe Peter wewe leo ndio umeyajua haya?Au baada yakuwa wakili ndo umejifunza haya?
Kwanini ulipokuwa polisi ukuyatekeleza haya? Au hizo sheria umezisoma gerezani? Ndugu yangu kesi yake ilichukua mwaka na miezi miwili ninyi wapelelezi mkisema ushahidi haujakamilika na bado kesi yenyewe mlikuja kuloose interest after a lot of suffering. Nikukumbushe tu hata dhamana haukutoa bure, ninyi mlihitaji fedha. Usafi wako upo wapi?
Unatuambia mke wako amefukuzwa kazi na watoto wanateseka,pole ila kumbuka namna ambavyo ulidhulumu haki za watu. Yamkini baadhi ya wateja wako kipindi kile waliacha kusomesha wakakulipa ujira wa mwea ili kesi zao ziishe mikononi mwako. Hao watoto ambao hawakusoma kipindi hicho kwa sababu yenu yakupokea rushwa Wana tofauti gani na watoto wako?
Unapotaka Rais akusikilize nenda na mikono salama na safi si unaenda na mikono michafu. Umetoka huko na sijui lini umeanza kujitegemea lakini naamini Mali na vitu ulivyo navyo vinadhuluma ndani yake hivyo nikuombe wewe na wasomi wengine wa Tanzania. Ninyi ndio mmeliaribu Taifa, mngesimama katika haki kwa nyadhifa zenu ndogo mlizokuwa nazo wakubwa zenu wangebadilika lakini mnatenda maovu mkiwa kwenye uniform mkirudishwa uraiani mnaanza kulia lia kutaka haki. Mmetutesa sana badilikeni.
Nawaonea huruma kwa mliyopitia lakini niombe Mhe. Rais kwa watu kama Peter na kwa mwaka mmoja na kitu tuliosota kutafuta haki mikononi mwake akigoma na kujibu shit sidhani kama anayo mikono safi yakuleta hoja ukaifanyia maamuzi chuja sana. The guy is more than arrogant, much know na dharau nyingi lazima tuseme ukweli watu wabadilike. Tusipowasema na kuwakanya ndio Hawa wanapata madaraka wanatuumiza then wakipata shida wanarudi kulia lia.
Kwa vyombo vya habari, fanyeni uchunguzi kuhusu watu kama wakina Peter, iambieni jamii ukweli ili kuwafunga mdomo watu wengine wanaolia kwa ajili ya familia zao badala yakulia kwa ajili ya Taifa. Msipofundisha adabu wakina Peter tutasikitika nao Leo ila kesho wakipata madaraka watatufanya kibaya zaidi ya walichofanywa. Hawa wavaa suti si watu wakuamini wanatumia elimu zao vibaya omba usikutane nao kwenye kutafuta haki utajuta.
Leo huyu mtu ukimuuliza kesi ngapi amewahi kusaidia mtu sidhani kama utapata, the guy is after money...
Pole Peter ila tambua uliutia uchungu moyo wangu na moyo wa familia yetu ukiwa polisi ukitimiza majibu kinyume kabisa na kanuni za jeshi hilo. Omba radhi safisha mabaya ndipo ujitokeze kukemea maovu. Usitumie vyombo vya habari kama kinga yakutokusemwa, ulikosea ukatudhulumu lazima tukuseme ujifunze kuheahimu watu.
Kila la kheri wewe na familia yako.