Wakili Peter Madeleka umekuwa lini msafi hadi umfundishe Rais kazi?

Pole Sana Bite. Pole Sana. Watu kama hawa wanaonea watu Sana halafu wanajua kweli kujitiisha huruma mbele ya macamera. Watu wa hii kaliba ni watu wa fitna na majungu. Watu wabinafsi.

Wanaonea watu, wanaharibia watu maisha. Mungu akiwapiga kwa dhambi zao wanakuja kujiliza mbele za watu kwamba wameonewa. Wanafki Sana hawa watu.

Naandika nikiwa na hasira Sana sababu na Mimi ni mhanga wa uonevu.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Hata ile clip yake ukiiangalia na kumsikiliza huoni akigusia mifumo mingine zaidi ya kumsakama dpp tu
Anyways people change
Let's give him benefit of the doubt
 
DPP ni kweli ofisi yake ilitesa watu na ni kweli mtu ana mashataka kadhaa..wizi..kudanganya sijui kutoa taaarifa za uongo mwishoni wanawake Money laundering..

IMEUMIZA WATU SANA, kingine kuna watu walikua wanashinda kesi..Ofisi ya DPP inarudisha kesi hiyo Mahakamani Mtuhumiwa anashinda mara 3 mpaka mara 4 bado anafunguliwa kesi hiyo hiyo kwa Makosa yake yale na mashahudi wale wale. Kwanini mfanye hivi? Mnamkomoa mtu mnamtesa na kuna wanasheria Wa mashirika ya umma nao wameitumia ofisi hiyo ya DPP kutesa watu sana ..
 
Katika moja ya jambo ambalo utawala wa awamu ya tano ulifanikiwa ni kudhibiti masuala ya haki na kisheria. Mawakili wengi ni wa hovyo sana.

Sent from my HRY-LX1T using JamiiForums mobile app
 
ile clip PETER MADELEKA (awali aliitwa Inspector Peter madeleka), anasema amekuwa polisi kwa miaka zaidi ya 20. ukweli ni kwamba, jamaa pamoja na kuwa mpelelezi miaka yote hiyo akitumia CPA na sheria zingine, hajui kabisa sheria, hajui maana ya uhujumu uchumi, hajui katiba.

Anapuyanga tu kama wanavyopuyangaga polisi kwenye shughuli zao wakati kwa sasa ni wakili. kitu pekee alichonacho ni uwezo wa kuongea ila hoja za kisheria anazidiwa hata na mtoto wa law school.

Alichotakiwa kukifanya ni kufanay consultation toka wa wataalamu kadhaa wa criminal law and procedures, aandae kitu inayoeleweka, aisomee usiku kucha ndio aje kufanye ile presentation. hakika nakuambia yule jamaa kama ndio vile anashinda kesi mahakamani basi itakuwa ni kwa huruma za hakimu au kesi ni mtelezo.
 
One thing watu hawajui ni kwamba, pesa hizo zinazosemekana zinalipwa kwa dpp, hazilipwi kwake, zinalipwa kwenye account ambayo Treasury registrar ameifungua hazina, ile account haipo mikononi mwa DPP, ipo mikononi mwa msajili wa hazina. jamaa kwenye clip yake amesema ile account ni ya DPP, bila kujua kwamba tupo wengi tu tumemaliza kesi za aina ile kwa ndugu zetu, ni wanasheria na tumefanya uchunguzi wa kueleweka hadi tukathibitisha hili ninaloliongea. amekurupuka bila research, na ameaibisha sana tasnia ya sheria.
 
Naandika hapa nikiwa na maumivu binafsi juu ya clip ya wakili Peter Madeleka. Sipingani na hoja alizotoa kwa sababu nyingi zina mashiko na mjadala aliouibua unatija kwa haki jinai Tanzania...
I can read feelings zako mtoa mada ulipokuwa unaandika hii post.
 
Katika moja ya jambo ambalo utawala wa awamu ya tano ulifanikiwa ni kudhibiti masuala ya haki na kisheria. Mawakili wengi ni wa hovyo sana.

Sent from my HRY-LX1T using JamiiForums mobile app
hawasomi hawa mawakili, hata wakifunguliwa uhuru wakija na hoja kama za huyu inspector wa polisi wa zamani, hakika wanasheria wa tz watakuwa wanaonekana vilaza.
 
Naandika hapa nikiwa na maumivu binafsi juu ya clip ya wakili Peter Madeleka. Sipingani na hoja alizotoa kwa sababu nyingi zina mashiko na mjadala aliouibua unatija kwa haki jinai Tanzania...
Dah! Kwa haya uliyoandika kulikuwa na ulazima wa Awamu ya Tano iliyokuwa imeji sacrifice kutetea haki za wanyonge kumshughulikia!
 
Pole sana mleta mada. Kuna ukweli usiopingika haswa hapa Tanzania. Mtendaji akiajiriwa sehemu hata akiwa malaika akienda kazini anageuka kuwa shetani. Hata wewe Beatrice ukiajiriwa TRA leo ukianza kazi na kuishi na wenzio kazini utatenda sidekicks za kupata rushwa kama wafanyavyo wenzio.

Wakili Pmadeleka alipokuwa afisa wa upelelezi jinai police alikuwa akitenda kama wenzie wanavyotenda( Linashangaza hili limetamalaki zaidi bongo) sababu sehemu nyingi za kazi hakuna uwazi, uwajibikaji na open controls hii inafanya mtendaji inabidi asujudu kwa bosi wake na kufuata system bosi wake anayoenda nayo.

Haya aliyaibua ya makosa ya kiufundi kwenye upelelezi, uendeshaji mashtaka, plea bargaining ni masuala yanayoigusa jamii moja kwa moja kwani ni maelfu ya watu wameonewa, wamenyimwa haki, wameshtakiwa pasipo sheria kufuatwa ni wakati sasa lazima yarekebishwe. Hivi unamsumbua mtuhumiwa miaka 5 halafu unakuja kumshtaki unakosa ushahidi hii ni hasara kwa taifa.
 
Well said my friend!!!

Ofisi ya DPP wakati wa Biswalo Mganga ilikuwa ni sawasawa na ofisi ya TUME YA UTUMISHI WA UMMA chini ya Muhojiii na watu wake ambapo ofisi ya TUME YA UTUMISHI WA UMMA imekuwa ni kero kwa watumishi wa Umma ambao wanaonewa na waajiri wasiofuata sheria katika masuala ya Utumishi wa Umma uonevu na kutokufanya critical review ya rufaa na malalamiko yanayopelekwa na watumishi wa umma limekuwa ni tatizo kubwa sana kwenye ifisi ya TUME.

Ofisi yaTUME TUME YA UTUMISHI WA UMMA imekuwa ni kichaka cha waajiri ambao sio ethical kwa kuwaondoa watumishi wa umma ofisini kwa misingi ya uonevu.

Tunaomba Mh. Rais aifanyie overhaul ya uhakika hii ofisi ya umma.

Asante!!
 
Analalamikia kukaa mahabusu siku11? huyu alitakiwa kukaa miaka 11 mahabusu. pambaf!
Jino kwa jino, upanga kwa upanga.
 
Kuna kamsemo kakiswahili kanasema Mtenda Akitendewa Huhisi kuonewa
 
Alichosema Peter Madeleka kina ukweli na kinapaswa kubadilika 100%, Madhambi aliyonayo hayafuti ukweli wote aliosema. Hata hivyo ni jasiri sana kusema yale aliyosema. Ingekuwa kipindi cha mwendazake sasa hivi angekuwa Cocobeach
 
lakini pia na kuhusu wewe hatujasikia upande wake. Usije kuwa unamsingizia ilhali mtu wako alikuwa na hatia kweli.
 
Yaliyopita si ndwele alipokuwa Polisi alikuwa anatekeleza amri ya Serikali lakini leo yuko kwenye mhimili wa haki,tumsamehe kwa yaliyopita tushike hayo mazuri aliyo nayo kwa wakati huu,kumbuka Saulo kabla hajawa Paulo alikuwaje?(Matendo Sura ya 9)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…