Wakili Robert Amsterdam ni nani?

Wakili Robert Amsterdam ni nani?

Sasa hii itawasaidiaje kwenye kampeni zenu ili muibuke washindi pasipo kuiba kura kama ilivyo desturi yenu. Wewe ulitaka umchagulie wakili.

This is very shallow and inept.
 
Hata mimi ninashangaa busara za Lissu kwenye jambo hili. Vile vile huenda aliwahi kufanya naye kazi ACACIA kwa hiyo wote wameikosa ACACIA. Ajenda kubwa ya Lisu inaonekana ni kuhusu mikataba ya mikataba na kushitakiwa tu.
 
Asante akseh... na asidhani tumeshau kuwa rafiki mkubwa wa acasia na makampuni mengi ya madini yaliyokuwa yakiibia nchi hii sote tunajua ni CCM na viongozi wake, mfani karamagi alisaini mkataba haramu hotelini london na sote tunajua, na uyu mjinga anatuaminisha kuwa ni TL.
Sincerely ukweli tunaujua
Wakati Lissu anawapambania Watanzania wanaonyanyaswa na makampuni ya madini duniani kule Nyamongo na serikali ikipambana naye tokea wakati wa Mkapa ili kuyalinda makampuni hayo, huyo mnayempigia chapuo kuwa mzalendo alikuwepo baraza LA mawaziri.

Ndio maana mauongo yenu dhidi ya Lissu ukiyazungumzia pale Tarime watu wanaweza kukutwanga marungu.

Nani nchi hii kawapigania RAIA dhidi ya makampuni ya madini yanayoiba na viongozi wa serikali zaidi ya Lissu nchi hii?

CCM labda muyadanganye mazwazwa kama yale mliyoyakusanya uwanjani Jana jukwaani maana hayafuatilii mambo ya nchi hii kwa kusoma historia
 
Sehemu moja umeandika...
"As shameful and criminal as Robert Amsterdam's behavior is in supporting a violent political front for a convicted criminal and mass murderer, at least Amsterdam admits he is doing so because he is a paid lobbyist. Unfortunately, it appears he has also constructed a network of faux "third party independent voices" he uses to lend his message credibility his status as a paid lobbyist cannot.”

Mahala pengine imeandikwa...
"Amsterdam's clients are hopeless causes, guilty of such overt criminality there really is no defense. And while it may be noble to defend such men, adhering to the best traditions and values of the West, Robert Amsterdam goes well beyond this, abusing this responsibility in order to carry out specific political objectives on behalf of the globalists with whom he consorts".

Wasomao na wahafamu
 
Baada ya taarifa za kuwepo kwa Tweet yenye barua ya wazi toka kwa raia wa Canada Bw. Robert Amsterdam, nimelazimika kujielemisha ili kujua huyu mtu ni nani, thanks to Google search. Niliyosoma kuhusu huyu mtu yamenishitua.

Kwa kifupi imeelezwa kwamba Bw Amsterdam ni wakili wa kimataifa anayejihusisha na kesi za kisiasa, mikataba ya madini, haki za binadamu, uakilishi wa kisheria wa makubwa duniani, n.k.

Kati ya kesi maarufu alizowahi kuzisimamia wakili Amsterdam ni zile zilizo wahusisha tajiri Mikhail Khodorkovsky wa Urusi na bilionea Thaksin Shinawatra wa Thailand. Wote hawa walishitakiwa nchini mwao kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kuonyesha nia ya kupindua serikali za nchi zao. Ni wazi kwamba Rais Putin wa Urusi hakuchelewa kumsweka ndani tajiri huyo wa mafuta.

Kwenye kichwa cha habari "A lesson in Intellectual dishonesty and International meddling" mwandishi wa habari Tony Cartalucci anaelezea Wakili Robert Amsterdam kama mtetezi wa majambazi (convicted criminals) hida ya serikali kwa kutumia agenda za Uhuru wa kisiasa.

Wakili Amsterdam pia ameshiriki kwenye kesi za mikataba ya madini katika nchi za kiafrika. Kama raia wa Canada sitashangaa nikisikia kwamba pia alihusika kusimamia makampuni kama Acasia kwenye kesi mbali mbali za kuishitaki Tanzania kwenye mahakama za kimaifa.

Huyu ndiye mtu ambaye Tindu Lissu amemkodisha kusimamia kwenye shughuli zake za kisiasa. Swali linakuja akilini ni kwamba Bwana Lissu amempa ahadi gani ikiwa atakupa Rais?

Huyu mtu anahesabu za political goes gani kwa Tanzania kama ilivyokuwa huko kwenye mataifa mengine? Hakuna chembe ya ukweli kwamba mkataba wa Bw Lissu na Amsterdam unahusu kutuma ya kisiasa.

Andiko la mwandishi Tony kuhusu Intellectual dishonesty and International meddling linatoa picha kamili ya huyu mtu. Hapo ndipo Mh. Lissu ametufikisha kama nchi.

Nadhani kuna ukweli kwamba anatumwa na wakubwa.
Kwaiyo unatakaje??
 
Baada ya taarifa za kuwepo kwa Tweet yenye barua ya wazi toka kwa raia wa Canada Bw. Robert Amsterdam, nimelazimika kujielemisha ili kujua huyu mtu ni nani, thanks to Google search. Niliyosoma kuhusu huyu mtu yamenishitua.

Kwa kifupi imeelezwa kwamba Bw Amsterdam ni wakili wa kimataifa anayejihusisha na kesi za kisiasa, mikataba ya madini, haki za binadamu, uakilishi wa kisheria wa makubwa duniani, n.k.

Kati ya kesi maarufu alizowahi kuzisimamia wakili Amsterdam ni zile zilizo wahusisha tajiri Mikhail Khodorkovsky wa Urusi na bilionea Thaksin Shinawatra wa Thailand. Wote hawa walishitakiwa nchini mwao kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kuonyesha nia ya kupindua serikali za nchi zao. Ni wazi kwamba Rais Putin wa Urusi hakuchelewa kumsweka ndani tajiri huyo wa mafuta.

Kwenye kichwa cha habari "A lesson in Intellectual dishonesty and International meddling" mwandishi wa habari Tony Cartalucci anaelezea Wakili Robert Amsterdam kama mtetezi wa majambazi (convicted criminals) hida ya serikali kwa kutumia agenda za Uhuru wa kisiasa.

Wakili Amsterdam pia ameshiriki kwenye kesi za mikataba ya madini katika nchi za kiafrika. Kama raia wa Canada sitashangaa nikisikia kwamba pia alihusika kusimamia makampuni kama Acasia kwenye kesi mbali mbali za kuishitaki Tanzania kwenye mahakama za kimaifa.

Huyu ndiye mtu ambaye Tindu Lissu amemkodisha kusimamia kwenye shughuli zake za kisiasa. Swali linakuja akilini ni kwamba Bwana Lissu amempa ahadi gani ikiwa atakupa Rais?

Huyu mtu anahesabu za political goes gani kwa Tanzania kama ilivyokuwa huko kwenye mataifa mengine? Hakuna chembe ya ukweli kwamba mkataba wa Bw Lissu na Amsterdam unahusu kutuma ya kisiasa.

Andiko la mwandishi Tony kuhusu Intellectual dishonesty and International meddling linatoa picha kamili ya huyu mtu. Hapo ndipo Mh. Lissu ametufikisha kama nchi.

Nadhani kuna ukweli kwamba anatumwa na wakubwa.
Mwandiko wako Kama wa Anna Makinda
 
WAJINA WANGU "Robert Amsterdam" USITUTISHE

Na, Robert Heriel

Kuna watu wapuuzi wanafikiri nchi hii itaogopa mtu yeyote atakaye bana maslahi ya taifa hili na watu wake. Tanzania ni nchi huru, ina watu wake na mali zake, ina utamaduni wake na sheria zake. Mtu yeyote bila kujali nafasi yake atakayedhani anaweza kuharibu nchi hii atatoboka mapema kabla hajafanikiwa.

Wajina wangu Robert Amsterdam ambaye nimemfahamu baada ya mteja wake, Tundu Lisu kurudi hapa nchini. Sikuwahi kumfahamu Wajina wangu Robert Amsterdam hapo kabla. Ninafuraha kumjua ';Bob' Mwenzangu, kwani nafahamu watu wenye majina ya Robert jinsi tulivyowatulivu, wapenda haki, werevu na wenye busara.

Robert Amsterdam ni Mwanasheria wa Kimataifa mwenye asili ya Kikanada ambaye amebobea katika fani ya sheria, na kujikita katika sheria za Kimataifa za umma(public international law), sheria za jinai ya Kimataifa(international criminal law), na Utetezi wa mambo ya kisiasa(political advocacy) Kutokana na umashuhuri wake na kushinda kesi nyingi za kimataifa anakampuni ya sheria iitwayo "Amsterdam & Partners LLP" Yenye Ofisi zake katika jiji la London, Uingereza na Washington Dc, Marekani.

Wajina wangu 'Bob' nakupongeza kwa kumtetea Ndugu yetu Tundu Lisu. Tunajua upo katika majukumu yako ya kazi. Lakini majukumu yako yasizidi mipaka na kuingilia mambo yasiyokuhusu.

Wajina wangu 'Bob' katika chaguzi zozote zinazofanyika hapa nchini kwetu kuna mambo ya msingi ambayo kama Watanzania tunayazingatia kuliko kitu chochote. Mambo hayo yanaweza kuwa yapo kisheria au yasiwepo kisheria, lakini itoshe kusema yapo;

Nitagusia machache kwa upendeleo kwa sababu wewe ni wajina wangu;

1. Amani ya nchi yetu

Watanzania ni watu wapendao amani, na hapa nimedhamiria kuzungumzia amani ya kutokuwa na vita, vurugu, kadhia, maandamano yenye mauaji, majeraha, uharibifu wa mali n.k.
Pengine tukawa hatuna amani ya kukosa mali, chakula na pesa. Lakini tunaamini amani ya kwanza ni kutokuwa na vita na matumizi ya mabavu.

2. Kulinda Muungano
Wajina wangu Bob, najua wafahamui nchi yetu ni muunganiko wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar na kuunda taifa la Tanzania. Hatupendi mtu ambaye tuna mashaka naye, ambaye atashindwa kulinda muungano. Mtu yeyote mwenye dalili za namna hiyo atapingwa, atadhibitiwa kwa heri au kwa shari. Ilimradi muungano usivunjike.

3. Uzalendo
Bob, bila kuvuka walau 70% ya uzalendo huwezi kuwa Rais wa taifa hili. Moja ya dalili za mtu Mzalendo ni kuitetea nchi hii kwa kukemea maadui zetu bila kificho. Bob wewe ni Mzungu wa Kanada, nataka nikuambie kuwa ninyi ndugu zetu wazungu mmekuwa mkitumia janja janja kutuibia mali zetu. Mnatupa 10 mnachukua 1000. Mnatuibia mali zetu kwa kile kiitwacho mikataba ya kimataifa, misaada, haki za binadamu n.k

Sasa sisi kwenye uchaguzi tunaangalia ni nani ataweza kukabiliana nanyi, nani ataweza kuhimili mikiki mikiki yenu, nani ataweza kuwatolea maneno ya shombo kama baadhi ya viongozi wa jamii za kizungu wanavyotutolea. Bob, Rejea kauli ya Bwana Donald Trump ambaye alitusimanga kwa maneno ya hovyo akiziita nchi zetu ni "shithole countries''

4. Kukomboa fikra za Watanzania.
Ndugu Amsterdam, nchi yetu ipo huru lakini bado hatupo huru kiuchumi na kiutamaduni. Na ili tuwe huru kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamadani sharti tukombolewe Kifikra. Bob, wewe unajua kile ninachozungumzia. Huwezi kuwa huru kama u mtumwa wa kifikra.

Tunamchagua Rais atakaye wakomboa Watanzania Kifikra. Rais atakayejenga fikra za watanzania kuwa wanaweza kujitegemea, wanaweza kuendesha maisha yao bila ya msaada wa wageni.
Rais atakaye waambia wananchi waache kutegemea wanasiasa, waache kutegemea mambo ya kupewa, bali wafanye kazi kwa bidii.

Hatutaki Rais anayewategemea ninyi ndugu zetu wazungu, watani wa jadi.

Ndugu wajina, mteja wako ni mtu mashuhuri hapa nchini, ni mwanasheria mzuri ambaye ninampenda, jambo pekee ambalo natamani kuliona kutoka kwake ni kuona akiwatukana ninyi watani zetu wa Jadi ambao mmetuweka kwenye kumi na nane zenu za ukoloni mamboleo.

Hatuogopi barua zako ikiwa zitagusa maslahi ya watanzania, hatutaogopa kuchukua hatua kulingana na sheria za nchi yetu pale mteja wako atakapovunja sheria za nchi hii.

Mimi namkubali sana Tundu Lisu ambaye ni mteja wako, lakini haitakuwa sababu ya yeye kututisha na ninyi watani zetu wa jadi.

Mteja wako atachaguliwa na watanzania ikiwa ataonekana na dalili zozote za mambo manne niliyoyataja hapo juu.

Kuhusu Kukatwa kwa Mteja wako.

Bob, sipendi Tundu Lisu aenguliwe na NEC, lakini kama itabainika anashirikiana na adui zetu kwa namna yoyote ile basi napendekeza akatwe mapema sana

Lisu ni Rafiki yangu, sijawahi kujificha kumtetea, kumpendekeza, kumsifia, kulaani hata siku aliyopigwa risasi. Lakini kama ataungana na ninyi watani zangu, wazungu ambao Taikon nawachukulia kama adui wa nchi yangu hakika nitapendekeza akatwe.

Ikiwa Lisu atabainika atahatarisha muungano basi aenguliwe.
Niliwahi kumsikia kipindi cha nyuma akiongea maneno yenye ukakasi ambayo bila shaka yanaukweli ndani yake, lakini ni ukweli usio na faida kwa nchi yetu zaidi ni ukweli wenye hasara ya kuleta utengano kwa nchi hii. Tunapenda ukweli, lakini ukweli wenye faida.

Ndugu Amsterdam, nilimpa mteja wako homework ambayo ingetoa muelekeo kwa wale wanaokaribia kumuamini na kutaka kumchagua. Nilimpa kazi mbili:

i. Azungumzie suala la ushoga, alikemee kwa nguvu zote.

Bob, Nchi yetu hairuhusu mambo hayo, ni kosa kisheria. Nafahamu nchi zenu sio kosa. Lakini kwetu ni kosa kubwa.
Tundu Lisu hakuwahi kuteteaa ushoga, lakini alionekana kupata kigugumizi kupinga ushoga pale alipoambiwa anazungumziaje suala la wapenzi wa jinsia moja. Lisu alikuwa na nafasi ya kuonyesha msimamo wake. Sasa kama alishindwa kipindi kile, nimempa homework kabla ya uchaguzi atoe msimamo wake. Aklishindwa majibu atayapata kwa watanzania. Mimi msimamo wangu ni kuwa nitampinga kila nipitapo nafasi ikiwa hatatoa ufafanuzi.

ii. Kuwakashifu ninyi wazungu
Nilimpa kazi ya pili kuwa, kama kweli anaipenda nchi hii basi angalau siku moja nimsikie akiwatukana ninyi, awatolee maneno ya kuudhi, kuchoma, kuteketeza. Mteja wako ameonekana kushindwa kuwasema ninyi vibaya. Hali inayonifanya nimuone kama kibaraka wenu.

Lisu ni rafiki yangu, ndugu zangu wanajua, maandiko yangu yanajieleza mara kadhaa, mchumba wangu anajua jinsi ninavyomkubali Lissu. Lakini kitu pekee wanachokijua watu hao pia kutoka kwangu ni kuwa sina unafiki.

Lisu kama utashindwa homework zangu, nakuhakikishia hutaenda popote Taikon angalipo, kama Mungu aishivyo.

Nimalize kwa kusema; Ndugu wajina wangu Robert Amsterdam, Mteja wako bado kuna mambo ameshindwa kujipapambanua. Hivyo barua zako hazitutishi kwa lolote lile.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
robertheriel99@gmail.com
 
Hakuna nchi yoyote duniani including Marekani na China ambazo haziogopi sera mbaya za nje dhidi ya nchi yao sembuse nchi maskini kama Tanzania ambayo fedha karibu 50% zinatoka nje. Tumeona nchi nyingi tu tena zenye nguvu kama Russia, China, Iraq, etc zikiathirika vibaya na sunctions kutoka nje.

Kuiangusha Tz ni rahisi mno hata baadhi ya watu binafsi wakiamua tu kufunga viwanda au biashara zao tayari nchi inayumba sembuse nchi matajiri. Lakini kwanini Robert unamsapoti magu na yote haya ya hovyo anayofanya? Natumaini wewe ni msomi flani lakini sioni unakwama wapi kuhusu uongozi mbovu wa kidikteta tulio nao, kwanini unasapoti udikteta na ukandamizi uliopo? Unafaidika nao? Basi jua kuna wengi sana wanaumia.
 
Hakuna nchi yoyote duniani including Marekani na China ambazo haziogopi sera mbaya za nje dhidi ya nchi yao sembuse nchi maskini kama Tanzania ambayo fedha karibu 50% zinatoka nje. Tumeona nchi nyingi tu tena zenye nguvu kama Russia, China, Iraq, etc zikiathirika vibaya na sunctions kutoka nje. Kuiangusha Tz ni rahisi mno hata baadhi ya watu binafsi wakiamua tu kufunga viwanda au biashara zao tayari nchi inayumba sembuse nchi matajiri. Lakini kwanini Robert unamsapoti magu na yote haya ya hovyo anayofanya? Natumaini wewe ni msomi flani lakini sioni unakwama wapi kuhusu uongozi mbovu wa kidikteta tulio nao, kwanini unasapoti udikteta na ukandamizi uliopo? Unafaidika nao? Basi jua kuna wengi sana wanaumia.
Wewe ni mmoja wa wainamia beberu?
 
Huyo Jamaa yupo na Twitter activists wana RT post yake wakitegemea Voters wako Twitter kwa taarifa tu hao washabiki wa Twitter majority sio wapiga kura, Sisi tupo kijiji kwa kijiji na leo tumeitisha harambee kanisani ya kuchangia ujenzi wa msikiti chamwino, Hii nikuonesha sisi watanzania hatuwezi kuwa seperated na mtu mmoja ambae hata familia yake haipo hapa nchini, Yeye atafute tu hata kundi la lawyers wa abroad akishindwa kuwalipa basi afunge nao ndoa mana si ndio miongoni mwa sera zake
 
Wewe ni mmoja wa wainamia beberu?
Sivyo hata kigogo na hata siwaiti mabeberu manake kama wao ni mabeberu basi akina nani ni majike? Nasema tu ni busara kushiriiana na nchi zilizoendelea badala ya kuwatukana huku tukikopa matrilioni kwao kila kukicha.
 
Msijidanganye na article zenu za kujiliwaza, mjue tu Tanzania sio kisiwa, fanyeni ujinga wenu halafu mtoke hapo muende kuomba misaada WB ndio mkumbushwe vizuri mlivyo wajinga.
 
Back
Top Bottom