Wakili Serikali Mulwambo: Mantiki sahihi ni kuingalia IGA dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo sheria za Tanzania

Unaposema huwezi kutumia sheria za ndani kuvunja mkataba wa kimataifa, kwa nini jaji ametoa hoja ya kufanya marekebisho kwenye vipengele vya ule mkataba, badala ya kuwapa ushindi wa moja kwa moja Jamhuri?
 
Eleza Vizuri Mkataba wa Kenya ilikuwa IGA kama Tanzania au? Na ilitupiliwa mbali Kwa muktadha upi?

Kama huo mwanya upo basi tusubirie maamuzi ya Mahakama ya Rufaa
 
Thanks 🙏🏿 very much just realized that while googling so this is the reason why they did this bogus contract. Please 🙏🏿 Tanzanian don’t accept this fake contract it’s not protecting your interest.
 
Sasa wanaokata Rufaa watakata Rufaa Ili wakasemaje tena maana uamuzi wa Majaji utakuwa huu huu.

Wao wangesubiria mikataba ya utekelezwaji ndio washitaki Mahakamani Kwa maana Mahakamani inaweza Amua vinginevyo na sio IGA.
Mbona unachangia kwa haraka bila kusoma utadhani kuku mwenye kideri,

Mahakama haiwezi kuvunja mkataba wa kimataifa, hilo tumeliweka wazi tangu tunaanza huu mkataba, sijui wewe ulikuwa wapi. Ila mahakama inaweza ikafanya kitu kiitwacho "Declaration of Rights" na kutoa ushauri wa kisheria "Advisory Opinion" ambao utapelekwa bungeni kwa ajili ya majadiliano. Mbona hili limeshawahi kufanyika huko nyuma kwenye kesi kubwa za kikatiba, ???

Halafu jambo jingine, nimelisema kwamba: ukisoma mkataba wa Vienna kuna mambo mengi sana ambayo hata mahakama yenyewe na mawakili hawayajayazingatia yanaoweza kuufanya huu mkataba uwe na walakini kisheria hata kama mahakama haitaweza kuuvunja. Sijui wewe mwenzangu shahada yako ya sheria ulisomea wapi.
 
Usipoteze mda na huyo choice variations naona ametumwa au mpumbavu sana haelimiki
 
Utambue wakina Adv. Mwabukusi wanashindana na mihimili yote ya hili taifa kwa sasa, hizo endorsement za bunge zinafanywa maalum ili kufukia mashimo yaliyosababishwa na huu mkataba wa hovyo ambao umeingiwa na serikali, na wanafanya hivyo ili kuhalalisha haramu ya serikali kwenye ule mkataba wa hovyo, ndio maana hii hukumu ya leo umekuja bila majibu kamili, jaji kutoa maelezo wakarekebishe akijua kuna sheria inakuja, badala ya kutoa order mkataba ni batili.
 
Kwa hiyo majadiliano yarudi Bungeni wakati Serikali ilishasaini IGA Sasa itabadili nini?

Nachotaka kujua wakati Serikali imepeleka Bungeni kupata ridhaa ya Bunge,Je Bunge lilikuwa na mandate ya kukataa Baadhi ya vipengele? Ndio nataka kujua maana umesema State inasaini na Bunge ku endorse.
 
Huo u hovyo wake uko sehemu zipi?
 
Mkuu acha mihemuko mbona unahama tena uhahama kabisa- achana na CCM na Tulia.
Nimeisoma hiyo Vienna Convention , mawakili wote wameitumia, majaji wameitumia kwenye hukumu yao, na wewe umeirejea sana; na kimsingi IGA inasimama juu yake na treaties zingine ulizo taja.
Kwa uelewa wangu nimesema IGA beeing a framework agreement haiwezi kutufikisha mahakamani; swali langu wewe unasemaje?
 
Eleza Vizuri Mkataba wa Kenya ilikuwa IGA kama Tanzania au? Na ilitupiliwa mbali Kwa muktadha upi?

Kama huo mwanya upo basi tusubirie maamuzi ya Mahakama ya Rufaa
Mkuu, wewe shahada yako ya sheria umesoma wapi, mbona unashindwa kuelewa mambo rahisi ?

Nimesema tokea mwanzoni, kwamba kama tutatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa, basi tutatengeneza mwanya ambao utahatarisha msingi mzima wa kuheshimu mikataba ya kimataifa. Nchi ambazo zinaona zinabanwa na mikataba zingeweza kuvunja kila zinapotaka. Kwenye sheria za kimataifa za mikataba, kanuni ni hii, "Pacta-Sunt-Servanda"

Halafu IGA maana yake nini wewe jamaaa, ???
IGA ni jina tu kama majina mengine. Mkataba wa kimataifa unaweza ukaitwa, Intergovernmental Agreement (IGA), Concordant, Memorundum of Undestanding (MOU), Bilateral Investment Treaty (BIT), Pact, Protocol, Convention, Charter, The Constitutive Act, etc Muhimu ni maudhui yaliyopo ndani ya mkataba.

Nashanga ninyi mnavyotaka kuyafanya mambo yawe magumu, ilhali IGA inaweza ikawa inahusu ulinzi, uwekezaji, kodi na mengineyo. Kuna IGA nyingi sana baina ya Marekani na UAE zinazohusu kodi. Lakini, kule nchini Marekani, IGA huwa zinasainiwa baina ya majimbo. Jimbo la California linaweza kusaini IGA na jimbo la Newyork. Huu siyo mkataba wa kimataifa.

==================================================================

Kuhusu Kenya: Chanzo kikubwa cha mgogoro ni mikataba ya uwekezaji (Investment Treaties + Concessions). Sheria za uwekezaji ziko sawa dunia nzima, na zinasimamiwa na kanuni za pamoja za Customary International Law ambazo zinalenga kutengeneza kitu kiitwacho, Fair and Equitable Treatment (FET) for Investors. Sasa iwe ni IGA/BIT/MIT/Hybrid-Treaty kama zinahusu uwekezaji kanuni zitakuwa sawa tu.

NB: You can bank on this....
 
Unaposema huwezi kutumia sheria za ndani kuvunja mkataba wa kimataifa, kwa nini jaji ametoa hoja ya kufanya marekebisho kwenye vipengele vya ule mkataba, badala ya kuwapa ushindi wa moja kwa moja Jamhuri?
Mkuu nionyeshe au nirejeshe hukumu iliposema hayo?
 
Acha upumbavu IGA is general kama haitaji TPA it’s null and void
 
Mkuu kwa kesi yetu concession contract au investment contract hazijafikiwa bado- kwa hiyo reference ya Kenya naiona kama ni irrelevant
 
Unaandika vipi mawakili kuna hoja hawakuziwasilisha vizuri, wakati jaji kwenye hukumu yake amekiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba na vinatakiwa kufanyiwa marekebisho?

Kama wasingewasilisha hoja zao vizuri, jaji angeweza kuwaelewa vipi mpaka akiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba wa hovyo wa bandari?

Usidharau kazi waliyofanya kina Adv. Mwabukusi, watanganyika tumeiona kazi yao na kuielewa.
 
Huyu mbongo haeleweki alinisumbua sana kumpa elimu nikaona shida yake sio elimu either ametumwa au ni mjinga asieelimika asante kwa kutoa elimu kuna wajinga wajuaji wengi Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…