Wakili Serikali Mulwambo: Mantiki sahihi ni kuingalia IGA dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo sheria za Tanzania

Mkuu Comte, haya nayaelewa na nimeshayaandika kule juu kwenye mchango wangu wa kwanza kabisa. Sijui kama uliusoma vizuri. Nimezungumzia suala zima la CAPACITY OF PARTIES and STATUS OF AN AGREEMENT. Nachokisema mimi ni hiki, kama wanasheria wetu, akiwemo Jaji hawajatumia, Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, basi kuna shida kubwa mno.

Yote tisa, huwezi kutumia sheria za ndani kuvunja mkataba wa kimataifa hasahasa ndani ya nchi inayotumia mfumo wa LEGAL DUALISM kama Tanzania. Kumekuwa na walakini mkubwa linapokuja suala la kuamua kesi zenye chembe za sheria za kimataifa. Mfano halisi, hata kesi ya Hamisi Machano ya uhaini, ilikuwa na makosa mengi mnoo.
Unaposema huwezi kutumia sheria za ndani kuvunja mkataba wa kimataifa, kwa nini jaji ametoa hoja ya kufanya marekebisho kwenye vipengele vya ule mkataba, badala ya kuwapa ushindi wa moja kwa moja Jamhuri?
 
Hata hili nalo lina walakini mkubwa. Hata katiba ya nchi nayo ni sheria kama sheria nyingine, sema tu ni sheria mama (The Mother-Law). Kiutaratibu, mikataba ya kimataifa huwa haivunjwi kupitia mahakama za ndani, kama ingakuwa inafanyika hivyo basi, mikataba mingi sana ya kimataifa ingekuwa inavunjwa kwa hila au ujanja pale ambapo nchi inahisi kubanwa.

Chini ya sheria za kimataifa za mikataba, kuna kanuni kongwe sana iitwayo "Pacta-Sunt-Servanda", ambayo hutaka nchi ziheshimu makubaliano iliyoyaingia bila ujanja-ujanja mwingine. Tukisema tunatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa basi tutakuwa tunaweka mwanya wa nchi kuvunja hii kanuni ya "Pacta-Sunt-Servanda"

Upande mwingine, Customary International Law, inasema dhahiri kwamba, suala zima la kusaini mikataba liko chini ya mamlaka ya serikali. AU, signing international treaties, falls within the prerogative of the executive. Hivyo bunge linapewa mamlaka ya kuridhia tu (Endorsing), kama mbinu ya ushirikishwaji wa wananchi, ila utiaji sahihi wa mikataba ni suala la serikali (The Executive). Ukishafahamu hili, utatambua kwamba mahakama haina uwezo wa kuvunja mikataba ya kimataifa kwasababu mamlaka yake ni ndani ya nchi tu.

Kesi za kikatiba za Rev. Christopher Mtikila, za miaka ya 90's ziliweka hizi kanuni wazi kabisa, kwamba kuna baadhi ya mambo siyo ya mahakama bali mihimili mingine. Hivyo mahakama inachoweza kufanya ni kutangaza haki na wajibu wa wahusika (Declaration of Rights) na kulishauri bunge lifanya mabadiliko muhimu. Hili niliongea majuzi na ndugu yangu Kalamu lakini nadhani hatukuelewana vizuri.

=============================================================
Sasa nirudi kwenye kesi na makosa niliyoyaona mwanzoni kabisa katika hoja tano ambazo mawakili wetu wasomi hawakuziangalia vizuri. Hata binafsi, nilishangaa kwanini mawakili wa serikali nao hawakuzizingatia vizuri hasahasa, Pre-Trail Conference (PTC):

Mosi, hoja ya kwamba Dubai siyo nchi hivyo haiwezi kusaini mikataba ya kimataifa. Wakili Mwabukusi alitumia mkataba wa kimataifa uitwao, The Monte-Video Convention, 1933 ambao unatoa vigezo vya sehemu kuitwa nchi. Hili ukiliangalia katika upande mmoja unaweza ukahisi ni sahihi, lakini katika mapana yake, lina walakini mkubwa.

Prof Hersch Lauterpatch aliandika mwaka 1958 kwenye chapisho la The International Law Commission (ILC), Commentary on International Treaties, kwamba "Treaties signed and entered by composition states/composite states, are treaties in the ordinary meaning of treaties entered by states"

Ukizingatia, State-Practice, hili linafanyika sana hapa duniani. Madola madogo (Composite States) ndani ya muungano au shirikisho huruhusiwa kusaini mikataba ya kimataifa chini ya udhamini wa dola kubwa. Mfano, Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, chini ya Ibara ya 32 (3) inasema hivi "In so far as the Lander have power to legislate, they may, with the consent of the Federal Government, conclude treaties with foreign states"

Hichi kipengele ndicho kililipa ruhusa jimbo la Bavaria la Ujerumani Magharibi, kuingia makubaliano ya kimataifa mwaka 1960 na nchi kama Austria na Switzerland kwenye utunzaji wa ziwa Constance dhidi ya uchafuzi. Hivyo hili linawezekana vizuri tu. Lakini kubwa na muhimu ni kwamba siku hizi hatutumii, The Monte-Video Convention 1933, peke yake kupima uwezo wa eneo linalojitawala kuwa dola, bali tunatumia, The Badinter Principles ambazo ziliandialiwa na European Union kwenye kuzitambua nchi huru zilizojitoa kwenye shirikisho la Yugoslavia.

Pili, kutumia sheria ya mikataba "The Law of Contract Act" kupinga mkataba wa kimataifa. Haya ni makosa makubwa mno. Mikataba yote ya kimataifa hutafasiriwa na kusomwa chini ya The Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969. Bahati mbaya kwenye ile kesi, hii sheria haikutumika, wala mawakili wa serikali hawakuitumia na sifahamu kama hata Jaji Ndunguru naye kaitumia. Kama hajautumia huu mkataba kwenye kuhukumu hii kesi, basi binafsi nasema, Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Bagosha (In Magu's Voice).

The Law of Contract Act, ingetumika endapo tu kama Tanzania/TPA ingekuwa imeshasaini HGA na DP-World. Maana, HGA ndiyo mkataba (A Contract/Concession/International Commercial Contract), bali IGA ni mkataba wa kimataifa (A Treaty). Japo, hata hapa kuna mianya mingi tu, ambayo mawakili wangeweza kupenya endapo wangepewa muda zaidi wa kujipanga.

Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.

Anyway,
Mambo ni mengi, na huyo wakili wako unayemsifia hapa naye kapuyanga vibaya. Wakina Mwabukusi walikuwa na baadhi ya hoja nzuri sana, sema tu hawakuziwakilisha vizuri mbele ya mahakama.
Eleza Vizuri Mkataba wa Kenya ilikuwa IGA kama Tanzania au? Na ilitupiliwa mbali Kwa muktadha upi?

Kama huo mwanya upo basi tusubirie maamuzi ya Mahakama ya Rufaa
 
Hata mimi nimefurahishwa sana na hichi walichokifanya ndugu zangu wakina Advocate Mwabukusi na jopo lake. Wamesema wanakata rufaa, nadhani kwenye mahakama ya rufani hata kama hawatavunja mkataba, kuna kitu muhimu ambacho mahakama inaweza kulishauri bunge likifanye au kukizingatia. Mahakama za Tanzania zishawahi kufanya hivi huko nyuma, kwa kulishauri bunge lipitie tena baadhi ya sheria ambazo zina ukakasi.
Tanzania ina BIT 21 mpaka sasa. UAE na Tanzania hatuna BIT ndiyo maana tumesaini IGA ambayo imetohoa vipengele vingi kwenye sheria ya uwekezaji. Naamini BIT itakuwa nzuri zaidi kwasababu haitakuwa ni mkataba wa upande mmoja tu, (Duty to Tanzania, Rights to Dubai). Despite their pitfall, BITs are mutual and reciprocal to say the least.

Mwarabu amefanya hivi maksudi akifahamu kabisa endapo atasaini BIT na Tanzania, basi wananchi wa Tanzania watakuwa na haki kubwa sana kwenda kuwekeza sehemu yoyote ndani ya UAE ikiwemo Dubai. Hii ndiyo tunaita akili kumkichwa.
Thanks 🙏🏿 very much just realized that while googling so this is the reason why they did this bogus contract. Please 🙏🏿 Tanzanian don’t accept this fake contract it’s not protecting your interest.
 
Sasa wanaokata Rufaa watakata Rufaa Ili wakasemaje tena maana uamuzi wa Majaji utakuwa huu huu.

Wao wangesubiria mikataba ya utekelezwaji ndio washitaki Mahakamani Kwa maana Mahakamani inaweza Amua vinginevyo na sio IGA.
Kipi!? Kumbuka hizo ni sheria za Kimataifa Zenye msingi wa Kimataifa,hakuna kitu Bunge litafanya unless Kwa sababu wamesha endorse.

Wangeenda Mahakamani mapema Kuzuia endorsement ya Bunge Ili zile sections zinazoleta ukakasiri zikajadiliwe upya n Executive na kazi hii ingefanywa na Kamati za Bunge kuishauru Serikali mapema kabisa kinyume na hapo ni kupoteza mda
Mbona unachangia kwa haraka bila kusoma utadhani kuku mwenye kideri,

Mahakama haiwezi kuvunja mkataba wa kimataifa, hilo tumeliweka wazi tangu tunaanza huu mkataba, sijui wewe ulikuwa wapi. Ila mahakama inaweza ikafanya kitu kiitwacho "Declaration of Rights" na kutoa ushauri wa kisheria "Advisory Opinion" ambao utapelekwa bungeni kwa ajili ya majadiliano. Mbona hili limeshawahi kufanyika huko nyuma kwenye kesi kubwa za kikatiba, ???

Halafu jambo jingine, nimelisema kwamba: ukisoma mkataba wa Vienna kuna mambo mengi sana ambayo hata mahakama yenyewe na mawakili hawayajayazingatia yanaoweza kuufanya huu mkataba uwe na walakini kisheria hata kama mahakama haitaweza kuuvunja. Sijui wewe mwenzangu shahada yako ya sheria ulisomea wapi.
 
Usipoteze mda na huyo choice variations naona ametumwa au mpumbavu sana haelimiki
 
Kipi!? Kumbuka hizo ni sheria za Kimataifa Zenye msingi wa Kimataifa,hakuna kitu Bunge litafanya unless Kwa sababu wamesha endorse.

Wangeenda Mahakamani mapema Kuzuia endorsement ya Bunge Ili zile sections zinazoleta ukakasiri zikajadiliwe upya n Executive na kazi hii ingefanywa na Kamati za Bunge kuishauru Serikali mapema kabisa kinyume na hapo ni kupoteza mda
Utambue wakina Adv. Mwabukusi wanashindana na mihimili yote ya hili taifa kwa sasa, hizo endorsement za bunge zinafanywa maalum ili kufukia mashimo yaliyosababishwa na huu mkataba wa hovyo ambao umeingiwa na serikali, na wanafanya hivyo ili kuhalalisha haramu ya serikali kwenye ule mkataba wa hovyo, ndio maana hii hukumu ya leo umekuja bila majibu kamili, jaji kutoa maelezo wakarekebishe akijua kuna sheria inakuja, badala ya kutoa order mkataba ni batili.
 
Mbona unachangia kwa haraka bila kusoma utadhani kuku mwenye kideri,

Mahakama haiwezi kuvunja mkataba wa kimataifa, hilo tumeliweka wazi tangu tunaanza huu mkataba, sijui wewe ulikuwa wapi. Ila mahakama inaweza ikafanya kitu kiitwacho "Declaration of Rights" na kutoa ushauri wa kisheria "Advisory Opinion" ambao utapelekwa bungeni kwa ajili ya majadiliano. Mbona hili limeshawahi kufanyika huko nyuma kwenye kesi kubwa za kikatiba, ???

Halafu jambo jingine, nimelisema kwamba: ukisoma mkataba wa Vienna kuna mambo mengi sana ambayo hata mahakama yenyewe na mawakili hawayajayazingatia yanaoweza kuufanya huu mkataba uwe na walakini kisheria hata kama mahakama haitaweza kuuvunja. Sijui wewe mwenzangu shahada yako ya sheria ulisomea wapi.
Kwa hiyo majadiliano yarudi Bungeni wakati Serikali ilishasaini IGA Sasa itabadili nini?

Nachotaka kujua wakati Serikali imepeleka Bungeni kupata ridhaa ya Bunge,Je Bunge lilikuwa na mandate ya kukataa Baadhi ya vipengele? Ndio nataka kujua maana umesema State inasaini na Bunge ku endorse.
 
Utambue wakina Adv. Mwabukusi wanashindana na mihimili yote ya hili taifa kwa sasa, hizo endorsement za bunge zinafanywa maalum ili kufukia mashimo yaliyosababishwa na huu mkataba wa hovyo ambao umeingiwa na serikali, na wanafanya hivyo ili kuhalalisha haramu ya serikali kwenye ule mkataba wa hovyo, ndio maana hii hukumu ya leo umekuja bila majibu kamili, jaji kutoa maelezo wakarekebishe akijua kuna sheria inakuja, badala ya kutoa order mkataba ni batili.
Huo u hovyo wake uko sehemu zipi?
 
Hapana siyo kweli, siyo kweli hata kidogo, tena ondoka kabisa huu uelewa.

Nimesema mwanzoni kabisa, Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ndiyo sheria inayosimamia tafasiri ya mikataba yote ya kimataifa. Mle ndani wanatoa mambo kama:

1. Maana ya mkataba wa kimataifa (Meaning of a Treaty)
2. Aina ya mikataba ya kimataifa (Types or Forms of International Treaties)
3. Wahusika wa mikataba (Subjects of International Law Capable of Making Treaties)
4. Vipengele muhimu vya mkataba (Elements and Contents of a Treaty)
5. Jinsi ya kurekebisha mikataba ya kimataifa (Modification and Amendment of Treaties)
6. Jinsi ya kuvunja mikataba ya kimataifa (Termination of International Treaties)
7. Jinsi ya kumuwajibisha mvunja mikataba (Remedies or Redress for Breach of Treaties)

Tatizo letu kubwa wanasheria wa Tanzania ni kwamba tunaliendesha hili suala kwa kukomoana, ulaghai na ushabiki. Hata msomi wa sheria kiwango cha PhD, Dr Tulia Ackson aliliongopea bunge vibaya kusema nchi imengia makubaliano siyo mkataba. Huwa nashangaa sana kwanini mpaka leo hajawajibishwa hata na wana CCM wenzake walio makini.

Mkuu acha mihemuko mbona unahama tena uhahama kabisa- achana na CCM na Tulia.
Nimeisoma hiyo Vienna Convention , mawakili wote wameitumia, majaji wameitumia kwenye hukumu yao, na wewe umeirejea sana; na kimsingi IGA inasimama juu yake na treaties zingine ulizo taja.
Kwa uelewa wangu nimesema IGA beeing a framework agreement haiwezi kutufikisha mahakamani; swali langu wewe unasemaje?
 
Eleza Vizuri Mkataba wa Kenya ilikuwa IGA kama Tanzania au? Na ilitupiliwa mbali Kwa muktadha upi?

Kama huo mwanya upo basi tusubirie maamuzi ya Mahakama ya Rufaa
Mkuu, wewe shahada yako ya sheria umesoma wapi, mbona unashindwa kuelewa mambo rahisi ?

Nimesema tokea mwanzoni, kwamba kama tutatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa, basi tutatengeneza mwanya ambao utahatarisha msingi mzima wa kuheshimu mikataba ya kimataifa. Nchi ambazo zinaona zinabanwa na mikataba zingeweza kuvunja kila zinapotaka. Kwenye sheria za kimataifa za mikataba, kanuni ni hii, "Pacta-Sunt-Servanda"

Halafu IGA maana yake nini wewe jamaaa, ???
IGA ni jina tu kama majina mengine. Mkataba wa kimataifa unaweza ukaitwa, Intergovernmental Agreement (IGA), Concordant, Memorundum of Undestanding (MOU), Bilateral Investment Treaty (BIT), Pact, Protocol, Convention, Charter, The Constitutive Act, etc Muhimu ni maudhui yaliyopo ndani ya mkataba.

Nashanga ninyi mnavyotaka kuyafanya mambo yawe magumu, ilhali IGA inaweza ikawa inahusu ulinzi, uwekezaji, kodi na mengineyo. Kuna IGA nyingi sana baina ya Marekani na UAE zinazohusu kodi. Lakini, kule nchini Marekani, IGA huwa zinasainiwa baina ya majimbo. Jimbo la California linaweza kusaini IGA na jimbo la Newyork. Huu siyo mkataba wa kimataifa.

==================================================================

Kuhusu Kenya: Chanzo kikubwa cha mgogoro ni mikataba ya uwekezaji (Investment Treaties + Concessions). Sheria za uwekezaji ziko sawa dunia nzima, na zinasimamiwa na kanuni za pamoja za Customary International Law ambazo zinalenga kutengeneza kitu kiitwacho, Fair and Equitable Treatment (FET) for Investors. Sasa iwe ni IGA/BIT/MIT/Hybrid-Treaty kama zinahusu uwekezaji kanuni zitakuwa sawa tu.

NB: You can bank on this....
 
Unaposema huwezi kutumia sheria za ndani kuvunja mkataba wa kimataifa, kwa nini jaji ametoa hoja ya kufanya marekebisho kwenye vipengele vya ule mkataba, badala ya kuwapa ushindi wa moja kwa moja Jamhuri?
Mkuu nionyeshe au nirejeshe hukumu iliposema hayo?
 
Kwa hiyo majadiliano yarudi Bungeni wakati Serikali ilishasaini IGA Sasa itabadili nini?

Nachotaka kujua wakati Serikali imepeleka Bungeni kupata ridhaa ya Bunge,Je Bunge lilikuwa na mandate ya kukataa Baadhi ya vipengele? Ndio nataka kujua maana umesema State inasaini na Bunge ku endorse.
Acha upumbavu IGA is general kama haitaji TPA it’s null and void
 
Mkuu, wewe shahada yako ya sheria umesoma wapi, mbona unashindwa kuelewa mambo rahisi ?

Nimesema tokea mwanzoni, kwamba kama tutatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa, basi tutatengeneza mwanya ambao utahatarisha msingi mzima wa kuheshimu mikataba ya kimataifa. Nchi ambazo zinaona zinabanwa na mikataba zingeweza kuvunja kila zinapotaka. Kwenye sheria za kimataifa za mikataba, kanuni ni hii, "Pacta-Sunt-Servanda"

Halafu IGA maana yake nini wewe jamaaa, ???
IGA ni jina tu kama majina mengine. Mkataba wa kimataifa unaweza ukaitwa, Intergovernmental Agreement (IGA), Concordant, Memorundum of Undestanding (MOU), Bilateral Investment Treaty (BIT), Pact, Protocol, Convention, Charter, The Constitutive Act, etc Muhimu ni maudhui yaliyopo ndani ya mkataba.

Nashanga ninyi mnavyotaka kuyafanya mambo yawe magumu, ilhali IGA inaweza ikawa inahusu ulinzi, uwekezaji, kodi na mengineyo. Kuna IGA nyingi sana baina ya Marekani na UAE zinazohusu kodi. Lakini, kule nchini Marekani, IGA huwa zinasainiwa baina ya majimbo. Jimbo la California linaweza kusaini IGA na jimbo la Newyork. Huu siyo mkataba wa kimataifa.

==================================================================

Kuhusu Kenya: Chanzo kikubwa cha mgogoro ni mikataba ya uwekezaji (Investment Treaties + Concessions). Sheria za uwekezaji ziko sawa dunia nzima, na zinasimamiwa na kanuni za pamoja za Customary International Law ambazo zinalenga kutengeneza kitu kiitwacho, Fair and Equitable Treatment (FET) for Investors. Sasa iwe ni IGA/BIT/MIT/Hybrid-Treaty kama zinahusu uwekezaji kanuni zitakuwa sawa tu.

NB: You can bank on this....
Mkuu kwa kesi yetu concession contract au investment contract hazijafikiwa bado- kwa hiyo reference ya Kenya naiona kama ni irrelevant
 
Hata hili nalo lina walakini mkubwa. Hata katiba ya nchi nayo ni sheria kama sheria nyingine, sema tu ni sheria mama (The Mother-Law). Kiutaratibu, mikataba ya kimataifa huwa haivunjwi kupitia mahakama za ndani, kama ingakuwa inafanyika hivyo basi, mikataba mingi sana ya kimataifa ingekuwa inavunjwa kwa hila au ujanja pale ambapo nchi inahisi kubanwa.

Chini ya sheria za kimataifa za mikataba, kuna kanuni kongwe sana iitwayo "Pacta-Sunt-Servanda", ambayo hutaka nchi ziheshimu makubaliano iliyoyaingia bila ujanja-ujanja mwingine. Tukisema tunatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa basi tutakuwa tunaweka mwanya wa nchi kuvunja hii kanuni ya "Pacta-Sunt-Servanda"

Upande mwingine, Customary International Law, inasema dhahiri kwamba, suala zima la kusaini mikataba liko chini ya mamlaka ya serikali. AU, signing international treaties, falls within the prerogative of the executive. Hivyo bunge linapewa mamlaka ya kuridhia tu (Endorsing), kama mbinu ya ushirikishwaji wa wananchi, ila utiaji sahihi wa mikataba ni suala la serikali (The Executive). Ukishafahamu hili, utatambua kwamba mahakama haina uwezo wa kuvunja mikataba ya kimataifa kwasababu mamlaka yake ni ndani ya nchi tu.

Kesi za kikatiba za Rev. Christopher Mtikila, za miaka ya 90's ziliweka hizi kanuni wazi kabisa, kwamba kuna baadhi ya mambo siyo ya mahakama bali mihimili mingine. Hivyo mahakama inachoweza kufanya ni kutangaza haki na wajibu wa wahusika (Declaration of Rights) na kulishauri bunge lifanya mabadiliko muhimu. Hili niliongea majuzi na ndugu yangu Kalamu lakini nadhani hatukuelewana vizuri.

=============================================================
Sasa nirudi kwenye kesi na makosa niliyoyaona mwanzoni kabisa katika hoja tano ambazo mawakili wetu wasomi hawakuziangalia vizuri. Hata binafsi, nilishangaa kwanini mawakili wa serikali nao hawakuzizingatia vizuri hasahasa, Pre-Trail Conference (PTC):

Mosi, hoja ya kwamba Dubai siyo nchi hivyo haiwezi kusaini mikataba ya kimataifa. Wakili Mwabukusi alitumia mkataba wa kimataifa uitwao, The Monte-Video Convention, 1933 ambao unatoa vigezo vya sehemu kuitwa nchi. Hili ukiliangalia katika upande mmoja unaweza ukahisi ni sahihi, lakini katika mapana yake, lina walakini mkubwa.

Prof Hersch Lauterpatch aliandika mwaka 1958 kwenye chapisho la The International Law Commission (ILC), Commentary on International Treaties, kwamba "Treaties signed and entered by composition states/composite states, are treaties in the ordinary meaning of treaties entered by states"

Ukizingatia, State-Practice, hili linafanyika sana hapa duniani. Madola madogo (Composite States) ndani ya muungano au shirikisho huruhusiwa kusaini mikataba ya kimataifa chini ya udhamini wa dola kubwa. Mfano, Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, chini ya Ibara ya 32 (3) inasema hivi "In so far as the Lander have power to legislate, they may, with the consent of the Federal Government, conclude treaties with foreign states"

Hichi kipengele ndicho kililipa ruhusa jimbo la Bavaria la Ujerumani Magharibi, kuingia makubaliano ya kimataifa mwaka 1960 na nchi kama Austria na Switzerland kwenye utunzaji wa ziwa Constance dhidi ya uchafuzi. Hivyo hili linawezekana vizuri tu. Lakini kubwa na muhimu ni kwamba siku hizi hatutumii, The Monte-Video Convention 1933, peke yake kupima uwezo wa eneo linalojitawala kuwa dola, bali tunatumia, The Badinter Principles ambazo ziliandialiwa na European Union kwenye kuzitambua nchi huru zilizojitoa kwenye shirikisho la Yugoslavia.

Pili, kutumia sheria ya mikataba "The Law of Contract Act" kupinga mkataba wa kimataifa. Haya ni makosa makubwa mno. Mikataba yote ya kimataifa hutafasiriwa na kusomwa chini ya The Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969. Bahati mbaya kwenye ile kesi, hii sheria haikutumika, wala mawakili wa serikali hawakuitumia na sifahamu kama hata Jaji Ndunguru naye kaitumia. Kama hajautumia huu mkataba kwenye kuhukumu hii kesi, basi binafsi nasema, Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Bagosha (In Magu's Voice).

The Law of Contract Act, ingetumika endapo tu kama Tanzania/TPA ingekuwa imeshasaini HGA na DP-World. Maana, HGA ndiyo mkataba (A Contract/Concession/International Commercial Contract), bali IGA ni mkataba wa kimataifa (A Treaty). Japo, hata hapa kuna mianya mingi tu, ambayo mawakili wangeweza kupenya endapo wangepewa muda zaidi wa kujipanga.

Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.

Anyway,
Mambo ni mengi, na huyo wakili wako unayemsifia hapa naye kapuyanga vibaya. Wakina Mwabukusi walikuwa na baadhi ya hoja nzuri sana, sema tu hawakuziwakilisha vizuri mbele ya mahakama.
Unaandika vipi mawakili kuna hoja hawakuziwasilisha vizuri, wakati jaji kwenye hukumu yake amekiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba na vinatakiwa kufanyiwa marekebisho?

Kama wasingewasilisha hoja zao vizuri, jaji angeweza kuwaelewa vipi mpaka akiri kuna makosa kwenye vipengele vya ule mkataba wa hovyo wa bandari?

Usidharau kazi waliyofanya kina Adv. Mwabukusi, watanganyika tumeiona kazi yao na kuielewa.
 
Mkuu, wewe shahada yako ya sheria umesoma wapi, mbona unashindwa kuelewa mambo rahisi ?

Nimesema tokea mwanzoni, kwamba kama tutatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa, basi tutatengeneza mwanya ambao utahatarisha msingi mzima wa kuheshimu mikataba ya kimataifa. Nchi ambazo zinaona zinabanwa na mikataba zingeweza kuvunja kila zinapotaka. Kwenye sheria za kimataifa za mikataba, kanuni ni hii, "Pacta-Sunt-Servanda"

Halafu IGA maana yake nini wewe jamaaa, ???
IGA ni jina tu kama majina mengine. Mkataba wa kimataifa unaweza ukaitwa, Intergovernmental Agreement (IGA), Concordant, Memorundum of Undestanding (MOU), Bilateral Investment Treaty (BIT), Pact, Protocol, Convention, Charter, The Constitutive Act, etc Muhimu ni maudhui yaliyopo ndani ya mkataba.

Nashanga ninyi mnavyotaka kuyafanya mambo yawe magumu, ilhali IGA inaweza ikawa inahusu ulinzi, uwekezaji, kodi na mengineyo. Kuna IGA nyingi sana baina ya Marekani na UAE zinazohusu kodi. Lakini, kule nchini Marekani, IGA huwa zinasainiwa baina ya majimbo. Jimbo la California linaweza kusaini IGA na jimbo la Newyork. Huu siyo mkataba wa kimataifa.

==================================================================

Kuhusu Kenya: Chanzo kikubwa cha mgogoro ni mikataba ya uwekezaji (Investment Treaties + Concessions). Sheria za uwekezaji ziko sawa dunia nzima, na zinasimamiwa na kanuni za pamoja za Customary International Law ambazo zinalenga kutengeneza kitu kiitwacho, Fair and Equitable Treatment (FET) for Investors. Sasa iwe ni IGA/BIT/MIT/Hybrid-Treaty kama zinahusu uwekezaji kanuni zitakuwa sawa tu.

NB: You can bank on this....
Huyu mbongo haeleweki alinisumbua sana kumpa elimu nikaona shida yake sio elimu either ametumwa au ni mjinga asieelimika asante kwa kutoa elimu kuna wajinga wajuaji wengi Tanzania
 
Back
Top Bottom