Mkuu, wewe shahada yako ya sheria umesoma wapi, mbona unashindwa kuelewa mambo rahisi ?
Nimesema tokea mwanzoni, kwamba kama tutatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa, basi tutatengeneza mwanya ambao utahatarisha msingi mzima wa kuheshimu mikataba ya kimataifa. Nchi ambazo zinaona zinabanwa na mikataba zingeweza kuvunja kila zinapotaka. Kwenye sheria za kimataifa za mikataba, kanuni ni hii, "Pacta-Sunt-Servanda"
Halafu IGA maana yake nini wewe jamaaa, ???
IGA ni jina tu kama majina mengine. Mkataba wa kimataifa unaweza ukaitwa, Intergovernmental Agreement (IGA), Concordant, Memorundum of Undestanding (MOU), Bilateral Investment Treaty (BIT), Pact, Protocol, Convention, Charter, The Constitutive Act, etc Muhimu ni maudhui yaliyopo ndani ya mkataba.
Nashanga ninyi mnavyotaka kuyafanya mambo yawe magumu, ilhali IGA inaweza ikawa inahusu ulinzi, uwekezaji, kodi na mengineyo. Kuna IGA nyingi sana baina ya Marekani na UAE zinazohusu kodi. Lakini, kule nchini Marekani, IGA huwa zinasainiwa baina ya majimbo. Jimbo la California linaweza kusaini IGA na jimbo la Newyork. Huu siyo mkataba wa kimataifa.
==================================================================
Kuhusu Kenya: Chanzo kikubwa cha mgogoro ni mikataba ya uwekezaji (Investment Treaties + Concessions). Sheria za uwekezaji ziko sawa dunia nzima, na zinasimamiwa na kanuni za pamoja za Customary International Law ambazo zinalenga kutengeneza kitu kiitwacho, Fair and Equitable Treatment (FET) for Investors. Sasa iwe ni IGA/BIT/MIT/Hybrid-Treaty kama zinahusu uwekezaji kanuni zitakuwa sawa tu.
NB: You can bank on this....