Wakili Serikali Mulwambo: Mantiki sahihi ni kuingalia IGA dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo sheria za Tanzania

Serikali ianaenda hatua ya HGA/CONCESSION na LEASE; XMASS tutakuwa na DP WORLD TANZANIA; 65% DP WORLD na 35% WATANZANIA. Mkuu jiandae kununua hisa
Bado niko kwenye IGA, huko HGA ukifika wasalimie.
 
Mkuu si anasema yeye haogopi chochote
 
Mbowe mbona ana nyumba Dubai na huwa anaenda huko?
 
kwani katiba ni sheria ya nje, ndio maana tunawambia nyie makuwadi ya warabu kama kina kitenge na zembwela ni wapumbavu, nenxeni shule muelimike kama hujui ni kwamba kwenye dhana ya sheria za kimataifa(international law) kuna sheria za ndani(municipal laws) katika hili constitution inclusive ila wajinga mmebaki kupayuka eti lazima bandari iwekezwe kisa kumbe hongo ndio inatumika.
 
hukumu za majaji wa kupigiwa sim nani anaweza kuzizungumzia.
 
I love u nyanga nyanga,
 
Mkuu Denoo J,

Mosi, kwenye nchi ambazo zinafuata mfumo wa LEGAL DUALISM, bunge likishapitisha mkataba wa kimataifa (Ratification) mkataba unakuwa halali na unaanza kufanya kazi. Hili ni lazima ulifahamu kabisa, na ulikubali maana ndiyo sheria yenyewe.

Pili, pia hata kama utatumia sheria za ndani, utazitumia chini ya mwamvuli wa The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ili kuthibitisha kwamba kulikuwa na uvunjwaji wa sheria za nchi husika wakati wa kusaini huo mkataba (Non-Compliance with laws of the host state/State Party).

Tatu, ila jambo kubwa ambalo linashangaza zaidi ni kwamba hata, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ni mkataba ambao ulisainiwa na serikali ya Tanzania mwaka 1976 na kutungiwa sheria ya bunge. Hii sheria ndiyo inatumika kutafasiri mikataba ya kimataifa. Hivyo mkataba wa Vienna ni muhimu kutumika mahakamani kwetu kwasababu imekuwa Ratified.
 
Nakuelewa, lakini pia bado naendelea kuwa na maswali kwako..

Hivi ni lazima panapokuwa na kesi mahakamani, wapeleka maombi sharti watumie sheria zote zinazohusu kesi husika? kwamba wakisahau kutumia sheria fulani, lakini bado walizonazo zikafikisha malalamiko yao, kuna ubaya wowote?

Nionavyo, matumizi ya sheria mahakamani kwenye kusikiliza kesi, hayana tofauti na matumizi ya wachezaji uwanjani, wanapocheza mpira..

Mchezaji anaweza kuwa substituted, akaingia mwingine akacheza vizuri kwenye namba ya yule aliyebadilishwa, na hata mahakamani, kama unakubali Vienna Convention imekuwa ratified hapa kwetu, na kutumika kutafasiri sheria, lakini wapeleka maombi wakaamua kutumia sheria nyingine kufikisha malalamiko yao, hiyo kwangu pia ni sawa na substitution ya wachezaji uwanjani, ambayo licha ya kufanyika, bado huleta ushindi kwa timu husika, pakiwepo na fairness kwenye maamuzi.

Naamini unaielewa concept yangu, kwasababu jinsi unavyowalaumu wapeleka maombi kutotumia Vienna Convention, ni kama vile unamaanisha kuna sheria kwenye ile kesi iliyowalazimu kufanya hivyo, jambo ambalo siliamini, ndio maana mwishoni umetumia maneno mkataba wa Vienna ni "muhimu" kutumika, hujasema ni lazima.
 

The Wonder Boy, elimu uliyotupa ni kubwa sana katika thread hii.

Imenifanya kuweza kusoma kurasa zote tisini na moja (91) za hukumu ya kesi ya kikatiba ya bandari na kuweza kupata mwanga kuhusu hoja za upande ukiowakilisha wananchi petitioner na upande wa serikali bila kusahau hoja za jopo la majaji.

Maana kuna legal jargons ( legal language) bila ya ufafanuzi wa The Wonder Boy ingekuwa ngumu kuelewa mabishano ya hoja baina ya pande mbili wananchi vs serikali na pia msimamo wa mahakama ya kikatiba wapi mamlaka yao inaishia.

Kesi hii imefungua ukurasa mpya hongera kwa wakili kiongozi Boniface Mwabukusi na timu yake wa mawakili wasomi pia raia waliofungua kesi hii ya kihistoria.

Imetoa mwanga katika maeneo mengi kinga ya Bunge, upeo Mahakama na pia elimu kwa mawakili.

Nina matumaini mambo yayabadilika na kuwa bora zaidi katika maeneo mengi yanayohusu mikataba ya kimataifa.

Natamani magazeti yetu na media kama vituo vya televisheni na radio wangepata watu wa sheria kama The Wonder Boy kuandika kwa kina kuhusu hukumu na mwenedo ulivyokuwa wa kesi hii ya kihistoria.

Hapo ndipo tunapoona umuhimu wa kuwepo waandishi wa habari / waendesha vipindi nguli wa sheria ambao wangeandika habari hii na pia kuendesha interview kuhusu kilichojiri na maana yake pana ya hukumu nzima ya kesi hii.


Pia kongole kwa JamiiForums kuwa na forums hizi zenye majukwaa yanayoelimisha masuala mengi mbalimbali kwa kina kuliko media Houses na mitandao ya kijamii yote Tanzania
 
12 August 2023

Wakili msomi - "Majaji wasema katika hukumu ya bandari kulikuwa na nafasi ya kuandaa mkataba mzuri zaidi ya huu"


Wakili wa kujitegemea na mbobezi wa sheria za mikataba Godwin Ngwilimi amechambua kwa kina hukumu ya kesi ya Bandari baada ya Wakili TV kufanya nae mahojiano kwa njia ya zoom.

Akichambua kurasa zote za hukumu kuanzia ukurasa wa 1 hadi wa 91 anaelezea maana na ujumbe halisi wa maneno katika hukumu hiyo ya kihistoria.
Source : Wakili TV
 
Kwani bangi zimeanza lini kuvutuwa makubaliano? Msingi wa sheria ni nini kama sik katiba?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…