Ok, hebu twende sawa..
Hapa kuna point ya wazi kabisa ambayo nakuona una miss, unashindwa kutofautisha ni wakati gani zitumike sheria za kimataifa, na wakati gani zitumike sheria za ndani.
Mfano tukiangalia shauri lililotolewa hukumu leo mahakamani, wale wapeleka maombi walikuwa wanalalamika juu ya sheria za ndani zilizovunjwa wakati wa kuingia ule mkataba wa IGA, na kwa mantiki hii, kwangu kwao kuonesha hizo sheria kwa kutumia Law of Contract Act na nyinginezo ni sahihi kabisa, kwamba ndio zimevunjwa.
Hawakutakiwa kutumia sheria za nje wakati wale walikuwa wanailalamikia serikali yetu, ambapo kama wangeshinda ile kesi, na mahakama kutoa order ile IGA ni batili...
Sasa hapo serikali yetu ndio ingetakiwa kwenda kwenye hayo mabaraza ya nje ya usuluhishi, ambapo huko, hizo sheria za kimataifa kama Vienna Conventions na nyinginezo ndio hutumika, pale ambapo serikali yetu inakuwa ikitaka kuvunja ule mkataba wa hovyo dhidi ya waarabu wa Emirati..
Naamini unaielewa pointi yangu, ndio maana nikaona kama una under-estimate kwa namna fulani kazi nzuri iliyofanywa na wakina Adv. Mwabukusi na wenzake, kwa kutoielewa hiyo concept, kazi ambayo imesababisha jopo la majaji kutoa maelekezo kwa bunge nini wakafanye.
Kwangu ni hayo tu.