Wakili Serikali Mulwambo: Mantiki sahihi ni kuingalia IGA dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo sheria za Tanzania

Wakili Serikali Mulwambo: Mantiki sahihi ni kuingalia IGA dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo sheria za Tanzania

Serikali ianaenda hatua ya HGA/CONCESSION na LEASE; XMASS tutakuwa na DP WORLD TANZANIA; 65% DP WORLD na 35% WATANZANIA. Mkuu jiandae kununua hisa
Bado niko kwenye IGA, huko HGA ukifika wasalimie.
 
Kumlaumu Mwabukusi ni kumuonea huwezi kujieleza vizuri wakati unapisha makombora He is being dogging bullets and you expect him to perform comfortably??!! His being living in fear and threat this is not a fair way of getting justice We salute his efforts and hopefully 🙏🏿 justice will prevail someday in Tanzania
Mkuu si anasema yeye haogopi chochote
 
Tanzania ina BIT 21 mpaka sasa. UAE na Tanzania hatuna BIT ndiyo maana tumesaini IGA ambayo imetohoa vipengele vingi kwenye sheria ya uwekezaji. Naamini BIT itakuwa nzuri zaidi kwasababu haitakuwa ni mkataba wa upande mmoja tu, (Duty to Tanzania, Rights to Dubai). Despite their pitfall, BITs are mutual and reciprocal to say the least.

Mwarabu amefanya hivi maksudi akifahamu kabisa endapo atasaini BIT na Tanzania, basi wananchi wa Tanzania watakuwa na haki kubwa sana kwenda kuwekeza sehemu yoyote ndani ya UAE ikiwemo Dubai. Hii ndiyo tunaita akili kumkichwa.
Mbowe mbona ana nyumba Dubai na huwa anaenda huko?
 
Mimi kwenye mantiki ya maisha ya kawaida siyo sheria ninaona Mulwambo yuko sawa. Unajua katika maisha ya kawaida na kuheshimiana rais anapokelewa na rais, mzee wa mji anapokelewa na mzee mwenzake. Kwa uelewa wang mdogo wa sheria na sheria za kimataifa pia nadhani yuko sahihi kwa sababu ukitumia sheria za ndani utakuwa unajenga mazingira ya kuonekana kutotenda haki
kwani katiba ni sheria ya nje, ndio maana tunawambia nyie makuwadi ya warabu kama kina kitenge na zembwela ni wapumbavu, nenxeni shule muelimike kama hujui ni kwamba kwenye dhana ya sheria za kimataifa(international law) kuna sheria za ndani(municipal laws) katika hili constitution inclusive ila wajinga mmebaki kupayuka eti lazima bandari iwekezwe kisa kumbe hongo ndio inatumika.
 
Mkuu, Mahakama imekubaliana na hoja za Mulwambo pamoja na masahihisho uliyofanya kwamba sheria katiba na sheria sheria (Municipal laws hazina) bearing yoyote kwenye IGA
Hukumu uk. 56 wanasema:
Overall, we are settled in our view that, since the parties were competent and with capacity to enter into trade and investment cooperation agreement, the signing of the IGA was not shrouded in any irregularity whichwould render it invalid or illegal. We are also settled in our minds that IGA is an international agreement whose oversight framework is not the LCA. We conclude that, to the extent this is not a normal contract, section 25 of the LCA is, in the circumstances of this case, immaterial.
hukumu za majaji wa kupigiwa sim nani anaweza kuzizungumzia.
 
Hata hili nalo lina walakini mkubwa. Hata katiba ya nchi nayo ni sheria kama sheria nyingine, sema tu ni sheria mama (The Mother-Law). Kiutaratibu, mikataba ya kimataifa huwa haivunjwi kupitia mahakama za ndani, kama ingakuwa inafanyika hivyo basi, mikataba mingi sana ya kimataifa ingekuwa inavunjwa kwa hila au ujanja pale ambapo nchi inahisi kubanwa.

Chini ya sheria za kimataifa za mikataba, kuna kanuni kongwe sana iitwayo "Pacta-Sunt-Servanda", ambayo hutaka nchi ziheshimu makubaliano iliyoyaingia bila ujanja-ujanja mwingine. Tukisema tunatumia mahakama za ndani kuvunja mikataba ya kimataifa basi tutakuwa tunaweka mwanya wa nchi kuvunja hii kanuni ya "Pacta-Sunt-Servanda"

Upande mwingine, Customary International Law, inasema dhahiri kwamba, suala zima la kusaini mikataba liko chini ya mamlaka ya serikali. AU, signing international treaties, falls within the prerogative of the executive. Hivyo bunge linapewa mamlaka ya kuridhia tu (Endorsing), kama mbinu ya ushirikishwaji wa wananchi, ila utiaji sahihi wa mikataba ni suala la serikali (The Executive). Ukishafahamu hili, utatambua kwamba mahakama haina uwezo wa kuvunja mikataba ya kimataifa kwasababu mamlaka yake ni ndani ya nchi tu.

Kesi za kikatiba za Rev. Christopher Mtikila, za miaka ya 90's ziliweka hizi kanuni wazi kabisa, kwamba kuna baadhi ya mambo siyo ya mahakama bali mihimili mingine. Hivyo mahakama inachoweza kufanya ni kutangaza haki na wajibu wa wahusika (Declaration of Rights) na kulishauri bunge lifanya mabadiliko muhimu. Hili niliongea majuzi na ndugu yangu Kalamu lakini nadhani hatukuelewana vizuri.

=============================================================
Sasa nirudi kwenye kesi na makosa niliyoyaona mwanzoni kabisa katika hoja tano ambazo mawakili wetu wasomi hawakuziangalia vizuri. Hata binafsi, nilishangaa kwanini mawakili wa serikali nao hawakuzizingatia vizuri hasahasa, Pre-Trail Conference (PTC):

Mosi, hoja ya kwamba Dubai siyo nchi hivyo haiwezi kusaini mikataba ya kimataifa. Wakili Mwabukusi alitumia mkataba wa kimataifa uitwao, The Monte-Video Convention, 1933 ambao unatoa vigezo vya sehemu kuitwa nchi. Hili ukiliangalia katika upande mmoja unaweza ukahisi ni sahihi, lakini katika mapana yake, lina walakini mkubwa.

Prof Hersch Lauterpatch aliandika mwaka 1958 kwenye chapisho la The International Law Commission (ILC), Commentary on International Treaties, kwamba "Treaties signed and entered by composition states/composite states, are treaties in the ordinary meaning of treaties entered by states"

Ukizingatia, State-Practice, hili linafanyika sana hapa duniani. Madola madogo (Composite States) ndani ya muungano au shirikisho huruhusiwa kusaini mikataba ya kimataifa chini ya udhamini wa dola kubwa. Mfano, Katiba ya Shirikisho la Ujerumani, chini ya Ibara ya 32 (3) inasema hivi "In so far as the Lander have power to legislate, they may, with the consent of the Federal Government, conclude treaties with foreign states"

Hichi kipengele ndicho kililipa ruhusa jimbo la Bavaria la Ujerumani Magharibi, kuingia makubaliano ya kimataifa mwaka 1960 na nchi kama Austria na Switzerland kwenye utunzaji wa ziwa Constance dhidi ya uchafuzi. Hivyo hili linawezekana vizuri tu. Lakini kubwa na muhimu ni kwamba siku hizi hatutumii, The Monte-Video Convention 1933, peke yake kupima uwezo wa eneo linalojitawala kuwa dola, bali tunatumia, The Badinter Principles ambazo ziliandialiwa na European Union kwenye kuzitambua nchi huru zilizojitoa kwenye shirikisho la Yugoslavia.

Pili, kutumia sheria ya mikataba "The Law of Contract Act" kupinga mkataba wa kimataifa. Haya ni makosa makubwa mno. Mikataba yote ya kimataifa hutafasiriwa na kusomwa chini ya The Vienna Convention on the Law of Treaties, 1969. Bahati mbaya kwenye ile kesi, hii sheria haikutumika, wala mawakili wa serikali hawakuitumia na sifahamu kama hata Jaji Ndunguru naye kaitumia. Kama hajautumia huu mkataba kwenye kuhukumu hii kesi, basi binafsi nasema, Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Bagosha (In Magu's Voice).

The Law of Contract Act, ingetumika endapo tu kama Tanzania/TPA ingekuwa imeshasaini HGA na DP-World. Maana, HGA ndiyo mkataba (A Contract/Concession/International Commercial Contract), bali IGA ni mkataba wa kimataifa (A Treaty). Japo, hata hapa kuna mianya mingi tu, ambayo mawakili wangeweza kupenya endapo wangepewa muda zaidi wa kujipanga.

Tatu, Jaji Ndunguru, Mawakili wa Serikali na Mawakili wetu kuna kitu muhimu kimewapita ambacho kama wangesoma vizuri, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, wangeweza kuutupilia mbali kabisa huu mkataba wa DP-World. Nchi jirani ya Kenya mwaka 2000-2001 waliweza kutupilia mbali kabisa mkataba wa kimataifa ambao ulizua taharuki kama hapa kwetu. Nadhani hili likifanyika na hapa kwetu, sijui serikali itaweka wapi uso wake.

Anyway,
Mambo ni mengi, na huyo wakili wako unayemsifia hapa naye kapuyanga vibaya. Wakina Mwabukusi walikuwa na baadhi ya hoja nzuri sana, sema tu hawakuziwakilisha vizuri mbele ya mahakama.
I love u nyanga nyanga,
 
Ok, hebu twende sawa..

Hapa kuna point ya wazi kabisa ambayo nakuona una miss, unashindwa kutofautisha ni wakati gani zitumike sheria za kimataifa, na wakati gani zitumike sheria za ndani.

Mfano tukiangalia shauri lililotolewa hukumu leo mahakamani, wale wapeleka maombi walikuwa wanalalamika juu ya sheria za ndani zilizovunjwa wakati wa kuingia ule mkataba wa IGA, na kwa mantiki hii, kwangu kwao kuonesha hizo sheria kwa kutumia Law of Contract Act na nyinginezo ni sahihi kabisa, kwamba ndio zimevunjwa.

Hawakutakiwa kutumia sheria za nje wakati wale walikuwa wanailalamikia serikali yetu, ambapo kama wangeshinda ile kesi, na mahakama kutoa order ile IGA ni batili...

Sasa hapo serikali yetu ndio ingetakiwa kwenda kwenye hayo mabaraza ya nje ya usuluhishi, ambapo huko, hizo sheria za kimataifa kama Vienna Conventions na nyinginezo ndio hutumika, pale ambapo serikali yetu inakuwa ikitaka kuvunja ule mkataba wa hovyo dhidi ya waarabu wa Emirati..

Naamini unaielewa pointi yangu, ndio maana nikaona kama una under-estimate kwa namna fulani kazi nzuri iliyofanywa na wakina Adv. Mwabukusi na wenzake, kwa kutoielewa hiyo concept, kazi ambayo imesababisha jopo la majaji kutoa maelekezo kwa bunge nini wakafanye.

Kwangu ni hayo tu.
Mkuu Denoo J,

Mosi, kwenye nchi ambazo zinafuata mfumo wa LEGAL DUALISM, bunge likishapitisha mkataba wa kimataifa (Ratification) mkataba unakuwa halali na unaanza kufanya kazi. Hili ni lazima ulifahamu kabisa, na ulikubali maana ndiyo sheria yenyewe.

Pili, pia hata kama utatumia sheria za ndani, utazitumia chini ya mwamvuli wa The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ili kuthibitisha kwamba kulikuwa na uvunjwaji wa sheria za nchi husika wakati wa kusaini huo mkataba (Non-Compliance with laws of the host state/State Party).

Tatu, ila jambo kubwa ambalo linashangaza zaidi ni kwamba hata, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ni mkataba ambao ulisainiwa na serikali ya Tanzania mwaka 1976 na kutungiwa sheria ya bunge. Hii sheria ndiyo inatumika kutafasiri mikataba ya kimataifa. Hivyo mkataba wa Vienna ni muhimu kutumika mahakamani kwetu kwasababu imekuwa Ratified.
 
Mkuu Denoo J,

Mosi, kwenye nchi ambazo zinafuata mfumo wa LEGAL DUALISM, bunge likishapitisha mkataba wa kimataifa (Ratification) mkataba unakuwa halali na unaanza kufanya kazi. Hili ni lazima ulifahamu kabisa, na ulikubali maana ndiyo sheria yenyewe.

Pili, pia hata kama utatumia sheria za ndani, utazitumia chini ya mwamvuli wa The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ili kuthibitisha kwamba kulikuwa na uvunjwaji wa sheria za nchi husika wakati wa kusaini huo mkataba (Non-Compliance with laws of the host state/State Party).

Tatu, ila jambo kubwa ambalo linashangaza zaidi ni kwamba hata, The Vienna Convention on the Law of Treaties 1969, ni mkataba ambao ulisainiwa na serikali ya Tanzania mwaka 1976 na kutungiwa sheria ya bunge. Hii sheria ndiyo inatumika kutafasiri mikataba ya kimataifa. Hivyo mkataba wa Vienna ni muhimu kutumika mahakamani kwetu kwasababu imekuwa Ratified.
Nakuelewa, lakini pia bado naendelea kuwa na maswali kwako..

Hivi ni lazima panapokuwa na kesi mahakamani, wapeleka maombi sharti watumie sheria zote zinazohusu kesi husika? kwamba wakisahau kutumia sheria fulani, lakini bado walizonazo zikafikisha malalamiko yao, kuna ubaya wowote?

Nionavyo, matumizi ya sheria mahakamani kwenye kusikiliza kesi, hayana tofauti na matumizi ya wachezaji uwanjani, wanapocheza mpira..

Mchezaji anaweza kuwa substituted, akaingia mwingine akacheza vizuri kwenye namba ya yule aliyebadilishwa, na hata mahakamani, kama unakubali Vienna Convention imekuwa ratified hapa kwetu, na kutumika kutafasiri sheria, lakini wapeleka maombi wakaamua kutumia sheria nyingine kufikisha malalamiko yao, hiyo kwangu pia ni sawa na substitution ya wachezaji uwanjani, ambayo licha ya kufanyika, bado huleta ushindi kwa timu husika, pakiwepo na fairness kwenye maamuzi.

Naamini unaielewa concept yangu, kwasababu jinsi unavyowalaumu wapeleka maombi kutotumia Vienna Convention, ni kama vile unamaanisha kuna sheria kwenye ile kesi iliyowalazimu kufanya hivyo, jambo ambalo siliamini, ndio maana mwishoni umetumia maneno mkataba wa Vienna ni "muhimu" kutumika, hujasema ni lazima.
 
Mkuu Comte, nitasema mara ya mwisho kabisa,

Mkataba wetu wa uwekezaji wa DP-World unatokana na IGA baina ya Tanzania na Dubai. Kitaalamu hii IGA is a sectoral investment agreement. Kama huu mkataba siyo halali hata utekelezaji hauwezi kuwa halali. Kanuni ambazo zinatumika kuvunja mkataba wa uwekezaji mkubwa (IGA) na mdogo (HGA) ziko sawa endapo uwekezaji huo umefanya ukiukwaji wa sheria.

Kukusaidia tu, kapitie The ICSID Convention, LCIA Rules, UNICITRAL Rules, Vienna Convention, na World Bank Guidelines on Treatment of Foreign Direct Investment, kote utaona kwamba kanuni zinazovunja mkataba mkubwa wa uwekezaji (BIT/MIT) ndizo hizo-hizo zinavunja mkataba wa utekelezaji (Concession/HGA/Contract).

Binafsi, nimeshatoa mchango wangu wa kile ninachokifahamu. Kama Mkristo naamini nimeshatimiza wajibu wangu, hivyo nanawa mikono kama Pilato. Mkiamua kuwa makini na kufuata weledi, itakuwa vyema, mkikataa pia, hewalaaaa mimi sipungukiwi na chochote.

Uwe na siku njema mkuu.


The Wonder Boy, elimu uliyotupa ni kubwa sana katika thread hii.

Imenifanya kuweza kusoma kurasa zote tisini na moja (91) za hukumu ya kesi ya kikatiba ya bandari na kuweza kupata mwanga kuhusu hoja za upande ukiowakilisha wananchi petitioner na upande wa serikali bila kusahau hoja za jopo la majaji.

Maana kuna legal jargons ( legal language) bila ya ufafanuzi wa The Wonder Boy ingekuwa ngumu kuelewa mabishano ya hoja baina ya pande mbili wananchi vs serikali na pia msimamo wa mahakama ya kikatiba wapi mamlaka yao inaishia.

Kesi hii imefungua ukurasa mpya hongera kwa wakili kiongozi Boniface Mwabukusi na timu yake wa mawakili wasomi pia raia waliofungua kesi hii ya kihistoria.

Imetoa mwanga katika maeneo mengi kinga ya Bunge, upeo Mahakama na pia elimu kwa mawakili.

Nina matumaini mambo yayabadilika na kuwa bora zaidi katika maeneo mengi yanayohusu mikataba ya kimataifa.

Natamani magazeti yetu na media kama vituo vya televisheni na radio wangepata watu wa sheria kama The Wonder Boy kuandika kwa kina kuhusu hukumu na mwenedo ulivyokuwa wa kesi hii ya kihistoria.

Hapo ndipo tunapoona umuhimu wa kuwepo waandishi wa habari / waendesha vipindi nguli wa sheria ambao wangeandika habari hii na pia kuendesha interview kuhusu kilichojiri na maana yake pana ya hukumu nzima ya kesi hii.


Pia kongole kwa JamiiForums kuwa na forums hizi zenye majukwaa yanayoelimisha masuala mengi mbalimbali kwa kina kuliko media Houses na mitandao ya kijamii yote Tanzania
 
12 August 2023

Wakili msomi - "Majaji wasema katika hukumu ya bandari kulikuwa na nafasi ya kuandaa mkataba mzuri zaidi ya huu"



Wakili wa kujitegemea na mbobezi wa sheria za mikataba Godwin Ngwilimi amechambua kwa kina hukumu ya kesi ya Bandari baada ya Wakili TV kufanya nae mahojiano kwa njia ya zoom.

Akichambua kurasa zote za hukumu kuanzia ukurasa wa 1 hadi wa 91 anaelezea maana na ujumbe halisi wa maneno katika hukumu hiyo ya kihistoria.
Source : Wakili TV
 
Wakili wa serikali Mulwambo ametoa somo kwa wanasheria na watu wengine kuwa kwa vile IGA ni makubaliano ya kimataifa kiitifaki inapaswa kuangaliwa dhidi ya katiba ya Tanzania na siyo kupitia sheria za Tanzania

He implored the Court to place the IGA on one hand and the Constitution on the other, as opposed to placing the IGA on one hand and laws and processes on the other hand. Learned counsel urged the Court to exercise restraint in deciding whether the IGA conflicts with the laws. At the end of the day, he argued, the expected word from the Court is whether the IGA contravenes the provisions of the Constitution
Kwani bangi zimeanza lini kuvutuwa makubaliano? Msingi wa sheria ni nini kama sik katiba?!
 
Back
Top Bottom