JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakili Salum Nduruma ambaye anamuwakilisha mchezaji Feisal Salum katika mgogoro wake wa kimkataba dhidi ya Yanga amesema wamepokea nakala ya maamuzi ya Kamati na mteja wake hana mpango wa kurejea Yanga kuendelea kuichezea timu hiyo.
“Feisal Salumu mpaka sasa hivi hana mpango wa kurudi na kuichezea Yanga na msimamo wake ni uleule kwamba anataka kuendelea kupinga hayo maamuzi kwa sababu anaona hayakumtendea haki… njia iko nyeupe kwenda CAS,” amesema na kuongeza:
“Hukumu tuliyopewa haina tofauti na kile kilichotolewa wiki iliyopita na Kamati. Tunataka kuwaandikia FIFA kuwaelezea mazingira yote yalivyokuwa ili kama inawezekana wakati Fei anaendelea na rufaa aweze kusajiliwa katika dirisha moja."