Wewe ndie unaejibu kwa jazba, huko kujuana wala usingeandika hilo linafamika.
Na nahisi kuna kitu wewe hunielewi, na sijui ni hoja gani hasa unazotaka.
Hakuna mahali nimesema watu wasihame, unahama kihalali??
Msingi wangu ndo upo hapo, sawa unahama je unahamaje sasa!? .
Hao waliouawa nchi zao zilikua na changamoto gani!? Walifuata taratibu ili kuingia huko?
Ingekua ni raia wa nchi moja ama kweli hao waliowapiga kweli wengelikua na roho ya kinyama, wanajua changamoto za nchini kwao halafu wanawadunda tena badala ya kuwapa afueni.
Lakini hao sasa ni kutoka nchi mbalimbali, wanaingia kiwizi tu. Na hapo wakiingia wala hawajipeleki serikalini kupata vibali ila wanaishi kiharamia tu.
Hakuna huruma, hujafata taratibu DUNDWA, urudi kwenu.
Mkuu mimi najua sana hali halisi ya ukimbizi
Nilikuwa vitani tena tatu
Ya mwisho ilikuwa uvamizi wa Iraq huko Kuwait
Nilikuwa Iraq ikabidi nikimbie niingie Jordan
Pindi vita inapotokea mahali huwa kuna immunity katika nchi husika
Tuliingia na magari yetu na kuelekezwa pa kwenda
Tulikaribishwa bila bughudha na wasiokuwa na passport zao waliambiwa wakaombe katika balozi zao kama huna balozi hapo kuna wawakilishi wa nchi
Nilikaa miezi miwili bila kuulizwa chochote natulipewa nyumba ya gorofa 16
Maisha yakikubana utaenda na kukimbilia popote utapopata uhifadhi Mkuu
Hapo nilipambana nikatoka na kuendelea na safari za kutafuta maisha
Huwezi kujua baada ya miaka kadhaa utakuwa wapi Kwa hiyo maisha hayana formula wala huwezi kupanga bali yanakuja tu
Sikutegemea kama ningemiliki uraia wa nchi nne
Ila leo nimazo mbili tu
Binadamu hawezi kuzuia mtu mwingine kufanya kitu
Mmoja atakataa uingie na mwingine anakupa shavu upande mwingine
Nimekuelewa sana unachoongea ya kuwa watu wafuate sheria waombe sheria za kuishi
Sasa mkimbizi utaomba viza ya Ulaya nani atakupa kwa kwenda ubalozini?
Ubalozi hautoi viza za wakimbizi Kwa hiyo watu wanaingia huko na kujilipua na baadae wanapewa sheria
Nchi za Ulaya western wanahitaji labour kila mwaka ndio maana wanawapokea ukiacha nchi njaa kama Greece