Wakina mama hujisikia vibaya watoto wao wa kiume wasiposhughulika na wanawake

Wakina mama hujisikia vibaya watoto wao wa kiume wasiposhughulika na wanawake

Siku moja mama aliniita alikuwa amekaa na baba ukumbini. Kilikuwa kama kikao cha dharura hivi. Mama akafunguka maswali yafuatayo.

Hivi mwanangu mbona sijawahi kuona, wala kusikia hata kidogo kama una mwanamke? Una tatizo gani mwanangu?

Mwenzako fulani analetewa hadi kesi kwa kutembea na watoto wa watu, wewe mbona sisikii lolote?

Na jambo kama hili lilitokea kwa ndugu yangu mwingine mtoto wa mama mdogo. Na rafiki yangu mwingine aliwekewa kikao kama hiki.

Mara ya mwisho rafiki yangu mwingine licha ya hao niliowataja alinihadithia tukio hili,
"mama yake alikuwa anatazama majina katika phonebook ya huyo rafiki yangu. Hakuona jina la kike hata moja. Mama yake hakujisikia vizuri akamuuliza. Mwanangu mbona sioni jina la kike hata moja? Una matatizo gani?

Kwa maelezo hayo nikagundua ya kuwa, wamama wanajisikia vibaya sana watoto wao wa kiume kutokuwa na mademu, tofauti na wababa. Na hii sijajua ni kwa nini. Kwa maana kwa upande wangu, baba hakuwa na wasiwasi ila ni mama. Na hao wote niliowataja wana baba ila wasiwasi ulikuwa ni kwa mama zao.

Hivi wadau hii imekaaje jamani?
Mrejesho
 
Ulikuwa na umri gani? Kama ulikuwa umemeliza masomo na una miaka kuanzia 20 mama yako kukuambia hivyo sio ajabu

Ila kama ndio ulikuwa shule ya msingi ama sekondar kisha mama anakushinikiza ukatafute wanawake, huyo mama yako alikuwa ni shangingi, stori kama hizo mnaongea na watu wa rika lako sio mama yako
Halafu atakutoleaje mfano wa rafiki yako kufunguliwa kesi kisa wanawake? anataka umuige? mbona ameoza sana kimaadili?
sorry kwa kum judge
🙏
 
Back
Top Bottom