Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Umeeleweka na umewatia moyo sana.
 
subiri baba wa mtoto awe anamtembelea 'mwanawe' ndipo utakapo tia akili
 
Kila laheri maana inawezekana nao hawakupenda kuwa singo maza labda kuna aliye andaliwa wewe kuwa mkombozi wake
 
Jf kipindi bado niko msomaji tu iliniharibia mahusiano yangu na mwanamke flani hivi aliyekuwa na mtoto. Nilisoma uzi mumoja tu na comment zake nikatoa na tamko la tuachane hapohapo. Mpaka leo kama najuta hivi maana hata hii brandy new niliyonayo ni pasua kichwa. Siwezi rudi nyuma na mbele hakuendeki bora tu nijute yaishe
 
Pole mkuu ukisoma comments humu changanya na zako, ukifuatisha mambo wanayosema humu hutokaa uishi maisha yako fanya kile kinachouridhisha moyo wako
 
Single mother na kiwanja chenye mgogoro hawajawai kuwa na utofauti
By the way andaa headex
 
Bora nioe binti wa miaka 18 kuliko kuoa aliyezalishwa na kuachwa.
Wanakuwaga na machungu mioyoni mwao
 
nimeanguka kwa single mother, nimejiandaa kukabiliana na changmaoto zote zinazosemwa humu. kwakuwa la kuambiwa changanya na akili yako, nimeamua kuendelea.....maneno yapo humu, vitendo mtaani. wengi humu, tena wengine ni wapostaji wa kila siku wa threads zinazoponda single mothers, wanadeal nao vizuri tu; ni eidha wake zao au wapenzi wao. nikiwa muislam, najua ndoa hainibani sana.....asipotia akili, sioni tabu kuivunja hata kesho.

nimemzidi kipato maana hana kazi wakati mimi ni muajiriwa. yeye amenizidi, kwa mbali tu, akili ya ujasiriamali....amenizidi sana. mipango yake inaonekana na ipo dhahiri (wakati yangu ninapoilinganisha kimyakimya ipo dhaifu kweli dhidi yake).....nataka kuvuna hiki kipaji, km sio mimi basi mtoto wangu (tukijaaliwa kuzaa), km ambavyo nae najua anataka kufaidika nami. aliolewa lkn mume ukicheche ulimsumbua baada ya kupata mtoto wao huyo....akamtelekeza na harakati za kudaiana talaka zikafanyika.

nimepeleka barua, wananijibu kuwa wanataka laki nne. PUMBAVU!!! nimewaambia wapunguze hadi nusu km hawataki basi. natoka na nipo maeneo ya pwani, huku ndoa ni ibada zaidi kuliko fursa....ukizingatia na umama wake, naona km nataka kupigwa. nimewapa hadi kesho kuamua hilo.

nilileta thread ya kukimbiwa na binti na kwenda kuolewa na tajiri flani,...ameolewa kwa laki mbili na nusu tu!

karibuni.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…