Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Janeth ni mwanamke msomi na mwenye kipato kizuri tu. Licha ya umbile lake zuri na tabia njema, hajaolewa mpaka sasa licha ya kuwa ana umri wa miaka 37.

Kitu pekee kinachomliwaza Janeth ni mtoto aliyempata katika mahusiano akiwa chuo kikuu mwaka wa pili na suala la kuolewa limeshindikana kwake mpaka sasa na amechoshwa na upweke wa kukosa mume wa maisha.

Nadya amebahatika kuolewa mapema na mume mwenye upendo wa dhati kwake na anamtimizia mahitaji yote muhimu katika ndoa. Licha ya kuwa ndoa yao ina miaka minne, hawajabahatika kupata mtoto licha ya kupimwa hospitalini na kuambiwa wote hawana tatizo la kiafya.

Je, kati ya Janeth na Nadya nani ana faraja zaidi katika maisha?

 
Hapo faraja kwa Nadya naiona hamna kabisa yaani...ila kwa Janeth angalau
 
Bora usingle mama masimango ya ugumba [emoji15][emoji15]
 
Mawifi wenyewe wa siku hizi na wakwe uolewe tu usizae utajutaa kwa nini uliolewa...lakini ukiwa na watoto na pesa hata ww mwanamke unaoaa tu wanaume kibao wanapenda mseleleko
 
Mnataka kusema kwamba.. maisha ya sasa mtoto kwanza ndoa ni majaliwa?
Bala shaka ndio ukweli kiupande mwingine...
Maana ! Hata ndio isipopatikana sawa....lakni kukosa mtoto na umri unaenda si mchezo kwa sisi wanawake unaweza kuzaa na mtu hujategemea ili mradi upate mtoto tu.
 
Mawifi wenyewe wa siku hizi na wakwe uolewe tu usizae utajutaa kwa nini uliolewa...lakini ukiwa na watoto na pesa hata ww mwanamke unaoaa tu wanaume kibao wanapenda mseleleko
Umeona ee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…