Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Naam kaka naona umekolea 😂,wanashauri usitoe hukumu unafuraha sanaaa au hasira sanaaaa....

Enewei ila usingo hauletwi na upande mmoja pekeee
 
Kweli kabisa, single Mama are the best, wana mapenzi moto moto.
 

Maneno yako unanikumbusha mdogo wangu, miaka mingi nyuma, aliniletea habari anataka kuoa "single mother" nikamwambia hiyo ni hiyari yako, kabla hujaoa fikiria "unaweza kustahamili kula meza moja na ex wake mkeo siku anafanyiwa birthday party yake mtoto wenu?"

Akanambia hilo hajalifikiria lakini halimpi shida. Wakaowana.

Nikamtakia heri na mafanikio. Matokeo, baada ya miaka mingi ya ndoa kupita, kilichowaachanisha ni birthday party ya huyo mtoto (alikuwa wa kike).

Swali hilo linarudi kwako.
 
Labda litahira pekee ndilo linaweza kumuoa money monger woman.

Single maza wengi kukataa hawawezi, ukiomba namba ya simu wanakupa, mkichati kidogo tu kabla hamjafika muafaka wanaanza kukuita baby.

Acheni utapeli, yaani sms 3 tu ya 4 unaniita baby. Hatari zaidi mnaanza njaa zenu za gesi imeisha, nywele zimefumuka. Inamaana hiyo gesi ilinisubiri Mimi kuisha?

Mnajishushia heshima.

Watu tuna pesa zetu tunataka tuwasaidie mambo muhimu makubwa ya kimaendeleo lakini huo upumbavu wenu mtaishia kusakanyuliwa mpaka ilegee kisha kila unayempa harudii tena.
 
Jamii nyingi hii kitu ilikuwa ni laana
Bukoba uliweza kufunkuzwa kabisa nyumbani. jamiii zingine waliwaua kabisa waliozalia nyumbani
siku hizi mmeboresha kabisa na kuwapa jina la kizungu-single mothers
Kwetu tarime ukishazaa kabla ya kuolewa unakuwa ni sawa na scraper-chuma chakavu
unaweza kuolewa tu na mzee na sio kijana , yaani unatakiwa kuwa mke wa pili na kuendelea na mahari inashuka
Je kwenye jamii yenu hili jambo lipoje
 
Kwetu tarime ukishazaa kabla ya kuolewa unakuwa ni sawa na scraper-chuma chakavu
unaweza kuolewa tu na mzee na sio kijana , yaani unatakiwa kuwa mke wa pili na kuendelea na mahari inashuka
Je kwenye jamii yenu hili jambo lipoje

Hata kwenye jamii kijijini kwetu hili lilikuwepo, ila kwa sasa limepungua.

Tunaenda vizuri na utandawazi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…