Habari za Jumapili Wadau.
Joshua Christopher Mwakasege ni Mtoto wa Mwalimu wa Neno la Mungu, C. Mwakasege.
Ninawafahamu wote wawili na familia yao kwa ujumla vizuri tangu nikiwa mtoto mdogo.
Sijaagizwa kuyasema nitakayoyasema ILA nitakwenda kuandika yafuatayo kwakuwa pia Mwl. Mwakasege ni Mtu MUWAZI sana katika kitu / mambo yanayofundisha wengine. Amekuwa akitoa mifano mingi hata kuhusu alivyoanza uhusiano na mkewe wa sasa Diana.
Kijana wake alifariki ghafla October mwaka Jana, sasa ana mwaka kaburini.
SABABU YA KIFO CHAKE: Mengi yanasemwa, na mengine hayafahamiki na hata Mwl. Mwakasege alisema tu kuwa Mwanae amefariki ghafla. Ila kwakuwa kuna cha kujifunza nitaeleza kifupi sababu ya kifo chake.
Msomi Joshua Mwakasege alikuwa na Uhusiano na mwanamke mzuri, aliyekuwa na Mtoto. Mwanamke huyu (sitamtaja jina) aliwahi kuwa miss wa wilaya mojawapo hapa DSM. Walipendana sana na Joshua mpaka ikafikia mahali pa Joshua kumtambulisha rasmi kwa wazazi wake.
Mwl. Mwakasege hakuwahi kumkatalia Mwanae kumuoa binti mwenye mtoto hata siku moja, ila alimuuliza swali
''Unamfahamu vizuri binti unayetaka kumuoa'' ?
'' Unamfahamu aliyezaa nae'' ?
Mara zote majibu yalikuwa ndio na hakukuonekana na tatizo lolote.
Mwishoni Mzee mwakasege alimwambia kijana wake kuwa unapaswa kumwomba Mungu sana kuhusu mke wa kumuoa na tutaomba pamoja LAKINI, mwisho wa yote wewe ndiye unayemfahamu zaidi binti utakayemuoa, na hatuwezi kukuchagulia Mke.
Joshua Mwakasege alimpenda sana yule Mwanamke na walikuwa na malengo, alimpenda yule mtoto kama wakwake na kuamua kumsomesha, kumlisha na kumvisha na alikuwa anamwita ni Mwanae wa kwanza, wengine watafuata.
Pamoja na yote hayo, na baada ya kupita muda flani wa mahusiano, bila kutegemea yule mwanamke alisafiri kutoka DSM na kuja Arusha, kisha siku moja Joshua akiwa kazini alipata ujumbe kutoka kwa Mke wake (Ninasema hivyo kwakuwa walikwishaoana) ujumbe ulimwomba msamaha sana na mkewe akimwambia kuwa ameamua kurudiana na Baba wa mtoto wake.
Hii inamaana walikuwa katika mawasiliano na mahusiano bado.
Kilichomuua Joshua Mwakasege bila shaka ni Msongo wa mawazo ulipitiliza, Depression ingawa iliitwa shinikizo la damu.
USHAURI : Vijana wote wa kiume na wa kike, tuwe makini sana na watu tunaoanzisha nao mahusiano ya kuelekea kwenye Ndoa. Ni vizuri sana kuchunguza ikiwa wana uhusiano wa awali na wapenzi wao haswa waliochangia damu kuzaa mtoto/watoto.
Hata Mabinti pia mnapaswa kuwa makini sana katika hili.
Jumapili Njema.