Habari ya mda huu wanajanvi!
Kama mada inavyojieleza hapo juu:
Hebu leo tujadiliane kwa pamoja juu ya swala hili linalo onekana kumea kwa kasi katika maisha ya sasa.
Je? Ni sababu zipi zinapelekea jambo hili lionekane ni "common" katika maisha ya
Sasa.
Binafsi naweza kulizungumzia swala la kuongezeka ma "single mother"
Kwa kulinganisha na sababu zifuatazo:-
Mtego wa mimba:
Asilimia kubwa ya mabinti/wanawake ambao hawajaolewa hivi sasa wamejenga tabia ya kujilaisisha kwa wanaume amabao wanaona kuwa wana vipato/ajira.
Jambo hili lime pelekea wengi wao(mabinti/wanawake) ambao wanatafuta uolewaji kudhani kuwa hiyo itakuwa sababu ya mwanaume huyo kumuowa na hatapia kubeba majukumu ya malezi kwa mtoto kama mzazi.
Malezi na Makuzi:
Hii pia ni sababu inayo changia kwa kiasi kikubwa.
Kutokana na mabinti wengi kukuwa na kulelewa katika familia zisizo fuata misingi ya maadili, imepelekea mabinti wengi kujiingiza katika vitendo vya uasherati.
View attachment 1680364
Hebu tujadiliane mbali na saba tajwa hapo juu, ni sababu zipi nyingine zinazo pelekeà kuongezeka kwa ma"single mother ".
Nakalibisha maoni yenu.