Wakinga wameamua kupambana, maneno yameanza kama ilivyo desturi ya Waswahili

Wakinga wameamua kupambana, maneno yameanza kama ilivyo desturi ya Waswahili

Dogo usikumbatie umaskini. Pambana utoke kwenye umaskini na kukariri majina ya watu ukidhani watakusaidia kila siku. Fanya kazi dogo umaskini si jambo la kujivunia na kujifariji.
Mimi ni mstaafu nina pensheni. Nilichaguaa kusoma na kuajiriwa. Sikukubali mauchawi ambayo Wakinga mnakwenda kwa Mwakipande kuwafanya mama zenu na baba zenu misukule ya kuwavutia hela.
 
Muulizie mwakipaande ingawa alifaruki ila alimrizisha mwanae ambae alikuwa akiishi mwanza wakati wa miaka ya 2000, sjui kwa sasa yuko wapi.
Huyo ndo alikuwa mtaalam wa makafara ya kujipatia pesa.
Nikiwa na muda nitawaletea hadithi ya ukweli ya mkinga aliyetaka kumtoa mkewe kafara, wakati huo huyo mkinga alikuja Dar kutoa gari mpya bandarini akamwambia mkewe amfuate dar ili warudi pamoja................kilichofuata anajua mkewe(ambae aliondoka kwenye ndoa baada ya tukio hilo) na dereva alokuwa amlete mke dar............
Wewe mshirikina Komeo Lachuma njoo usome hii hapa juu inakuhusu
 
Kwakweli mimi hili la kusemaga kabila fulani wamepata kwa kafara sijui uchawi wala halinikaagi kabisa kichwani.
Nachkaminini wakinga pesa zao wamezipata kwa kufanya sana kazi. Pia miti na kilimo kimewapa mitaji. Sisi wachagga pesa zetu tumezioata kwa kutumia sana nguvu. Hatuna ardhi. Na pia si kweli kwamba eti wachagga wameondoka kkoo ama wakinga wametuzidi ni uongo. Sisi ni kabila kubwa sana ukiacha udogo wa mkoa. Wachagga wamevuka na kuingia katika uzalishaji kabisa.

Kwa kuongezea jambo, wakinga wana nidhamu sana ya pesa. Hawaichezei. Wanaitunza mno na watafika mbali. Kwahiyo sitaweza wasakama kabisa katika hili. Ila ardhi yao sasa hivi tumeivamia na watanzania wengineo. Pambaneni wakinga umaskini unadhalilisha sana
Mkuu naungana na wewe. Watumike kama role model ya maendeleo.
 
Mimi siyo dogo. Naweza kuwa baba yako kwa kukuzaa. Hivi kule nyuma nilipokuambia nawafahamu Wakinga wa Mbeya wa miaka ya 1980s hukunielewa? Akina Nkwenzulu, Tweve na Chawe. Ningekuwa na huo umri unaoniita dogo nisingeandika haya ninayoandika. Matajiri Wakinga ni washirikina tu, period
Walikuwa wapi zamani kutamba kama siku hizi kwenye biashara?
MAANA WANATREND KAMA WASOMARI. WOTE KKOO WALIKUWA HAWANA INFLUENCE KAMA SASA. Na ukumbe kariakoo sehemj nyingi watu wamekaa kikabila na kimakundi waha, watu wa tanga watu wa mbeya, wasuku.a kwa nini hawa wanakuwa kwenye level za juu kuwapita wenzao. Kama ni uchawi wote ni wachawi tu.
 
Kweli kabisa uaminifu kwenye pesa kwetu sisi watz ni hakuna, nilikutana na mkenya mmoja akaniambia kwenye pesa hats wazazi wako wanakupiga, niliwahi kufungua mradi wa kilimo cha umwagiliaji nikamuomba Dada yangu na shemeji yangu wasimamie baada ya miezi sits nikaenda kuwatembelea nilipofika tu sikutaka hata kukaa Kitano nikaomba wanipeleke shambani kwanza kisha mambo mengine yataendelea, iliwachukua nusu SAA kufikia uamuzi wa kunipeleka site nilipofika huko hakukua na shamba wala chochote bad enough walipokua wananitumia video clips za progress ya kazi walichukua kutoka mashamba mazuri kabisa ya watu wengine yaliyostawi vizuri na kutunzwa vizuri hiyo ilinipa moyo nilituma pesa kila ilipohitajika na ziada niliwapa, hakika nilisamehe tu ili kuilinda ndoa ya Dada wajomba zangu wasijewakapata tabu, nilighafilika mno coz nilisave kwa kujinyima mno na niliplan mradi ungetik nilipanga kuacha kazi kwa kua mazingira ya kazi hayakua mazuri, niligeuka Sikh hiyohiyo nikarudi nilipotoka.
Aisee pole sana kwa yaliyokukuta
Nakuambia hivi sio hela hata plan zako wasijue, wawe ndugu wala nani
Binadamu sisi wabaya sana
Wengi wanaolizwa hulizwa na ndugu wa karibu sana

Kuna watu wengi wako nje ya nchi yaani wanashawishika kujenga na wanatuma hela za kiwanja
Ujenzi unaanza kwa kuwa husafori wewe unatumiwa picha za sites za watu tu kuanzia msingi
Hela zinapigwa siku ukienda utazungushwa kupelekwa site mpaka unajiongeza na kumwambia sema tu umenipiga


Ndugu hawafai wengi wao na usije kimbia ndugu ukaamini rafiki hao ndio balaa
 
Mimi ni mstaafu nina pensheni. Nilichaguaa kusoma na kuajiriwa. Sikukubali mauchawi ambayo Wakinga mnakwenda kwa Mwakipande kuwafanya mama zenu na baba zenu misukule ya kuwavutia hela.
Kusoma kila mtu anasoma . Kuelimika ndo changamoto Dogo. Ukielimika utagundua bidii ya biashara na miiko yake inatajirisha. Nyie endeleeni kuamini free mason na matakataka mengine. Msome muelimike dogo.
 
nimekua karibu na wakinga naeza kusema nawajua vizuri. zaman wakinga wengi walikuwa ni jamii maskini sana (ule umaskini mbwa mbwa kabisa) tu kama zilivyo jamii zetu nyingi. wengi walikuwa wanafanya kaz za kuhemea vibarua vidogo vidogo majumban na hasa mashamban yani kam una kikaz chako unamuita anakufanyia.

kilichowainua wakinga ni nidhamu ya juu sana ya kutafuta na kutunza pesa [jamaa sio watumiaji wa pesa]

mkinga anaweza kuwa na burungutu la ela lakini ukakuta anashindia vipande vya mihogo vya mia tano. wako ivo.

cha pili ni wachapakazi sana na wako focused kupita maelezo. anaweza kuwa na duka lakin lazima awe na mashamba yale makubwa uko kwao sio ajabu kukuta tajiri mkubwa tu apo town lakn ana heka 200, 300 au 400 za mazao uko porini.

ni watu wavumilivu na sio watu wa kuendekeza anasa au maisha ya show off kifupi sijapata kuona jamii kama iyo. wanafocus kwenye mambo yao zaidi sio watu wa kupenda kuongeaongea.

hayo mambo ya uchawi kuna jamii gani ya apa tz haina uchawi mbona awaupati uo utajiri? ingekuwa uchawi una maajabu wale watu wa songwe na wenzao wa sumbawanga si wangekuwa matajiri wakubwa sana?
Kweli kabisa, kwenye nidhamu ya pesa wako vizuri. Mtu anaingiza 10k, lakini anajinyima anatumia buku.

Masikini na wavivu wa kufikiri ndio wanaoleta hizo hoja za uchawi.
 
Kweli kabisa, kwenye nidhamu ya pesa wako vizuri. Mtu anaingiza 10k, lakini anajinyima anatumia buku.

Masikini na wavivu wa kufikiri ndio wanaoleta hizo hoja za uchawi.
Sasa unajuje mtu kaingiza kiasi fulani? Au kilamahesaba wanakujulisha kwamba leo nimeingiza 10k na nimetumia buku.
Kataa kubari ushirikina ni jadi yao.
 
Je kufanya biashara ni kipaji?” Ninafurahi kuwa yamekuwa makala yaliyowavutia wengi ambao hawakusita kunitumia mirejesho ya pongezi na maoni kupitia ujumbe wa simu, barua pepe na simu za miito. Msomaji mmoja amenitumia ujumbe ulionifurahisha kweli kweli; ninanukuu, “Makala yako ni nzuri na umechambua kitaalamu, lakini pia utajiri wa Wakinga asilimia 70 huwezi kuutenganisha na ushirikina. Vile vile Wachagga nao utajiri wao asilimia 30 ni ushirikina na 20% ni ujambazi. Na asilimia zilizobaki ndizo zinazoangukia kwenye uchambuzi wako,” mwisho wa kunukuu. Leo nitachambua kwa mara nyingine tena hili sekeseke la ushirikina kuhusishwa na biashara, si tu kwa Wakinga na Wachagga pekee, bali pia kwa wafanyabiashara wote bila kujali kabila wala eneo waliloko. Lakini kabla ya kuendelea na uchambuzi huu kwanza nina taarifa moja ya muhimu kwa wasomaji wetu.

Kwa muda sasa wasomaji wengi wamekuwa wakiniulizia ikiwa nimeshaandika kitabu. Na kila ninapowajulisha kuwa sijaandika kitabu chochote mpaka sasa, wengi wamekuwa wakiniomba kufanya hivyo. Ombi hilo nimekuwa nikilipokea kwa muda mrefu sasa, na hatimaye mwaka huu nimeamua kulitekeleza.



Tangu Februari, mwaka huu nimekuwa katika mradi wa kuandika kitabu kiitwacho ‘NI WAKATI WAKO WA KUNG’AA’. Ni kitabu kinachoeleza namna ya kuwa mshindi katika maeneo yote ya maisha. Kinaeleza namna ya kujitambua, jinsi ya kuwa mshindi kiuchumi, jinsi ya kung’aa kifamilia na kuwa mtu unayeona ladha halisi ya maisha.



Ninaamini kuwa kitabu hiki kitakuwa na matokeo makubwa kwa kila atakayebahatika kununua nakala yake. Kitabu hiki kimefikia hatua nzuri na ninatazamia kuwa kitaingia sokoni mwishoni mwa Novemba ama mwanzoni mwa Desemba, mwaka huu. Ni kitabu ambacho asilimia 90 ya mauzo yote nitazipeleka katika kusaidia huduma za afya za watoto barani Afrika.



Msomaji aliyenitumia ujumbe wa takwimu za ushirikina na ujambazi wa Wakinga na Wachagga hakuweza kunieleza ni wapi ametoa takwimu hizo. Wenye hekima wanatueleza kuwa pasipo kufanya utafiti huna haki ya kuzungumza. Suala la ushirikina lipo “kiroho” na “kihisia” kiasi kwamba watu wengi mitaani wanaongea na kuwataja wafanyabiashara washirikina pasipo kuwa na utafiti wa kitaalamu kuhusiana na hilo.



Kwa miaka mingi nchini Tanzania na duniani kumekuwapo na imani, hisia, visa na matukio yanayohusisha ushirikina na mafanikio ya mtu kibiashara. Katika uzoefu wangu wa kusoma na kusikiliza, sijakutana na utafiti ama maandishi yoyote rasmi yanayodhihirisha kiusawa (fair verification) nafasi ya ushirikina katika mafanikio ya mtu kibiashara.



Wataalamu wa masuala ya biashara, taasisi za maendeleo, wanadini na watu wa kada ya kawaida, mara zote wasimamapo katika hadhara husisitiza watu kutoamini mchango wa ushirikina katika mafanikio ya mtu katika biashara. Pamoja na hayo; Je, ni kweli kuwa ushirikina haupo? Je, mioyo ya watu inaamini nini kuhusu hili?



Ukweli ni kwamba watu wengi wanaamini uwepo wa imani hizi za kishirikina katika biashara mbalimbali. Ni wachache wanaokiri wazi iwapo wanatumia ushirikina, lakini siku kwa siku idadi ya wanaofika kwa waganga wa kienyeji kutaka ndumba za kuwatajirisha inaongezeka.



Huku Nyanda za Juu Kusini, kabila la Wakinga (kama nilivyoeleza katika makala ya wiki lililopita); ni maarufu sana kibiashara. Ni kawaida kusikia habari za wafanyabiashara hawa kuhusishwa na ushirikini. Ukweli na uhalisia wa Wakinga (na watu wengine popote) kutumia ushirikina ni jambo ambalo huwezi kulithibitisha wala kulikanusha kirahisi.



Nakiri kuwa licha ya kwamba ni vigumu kukanusha ama kuthibitisha uwepo wa ushirikina katika biashara; vipo visa, tetesi na stori nyingi kuhusu ushirikina kwenye biashara. Mathalani, hivi karibuni kumevuma habari za uwepo wa waganga wa jadi nchi jirani (Zambia, Malawi na DRC) ambao wanatoa “utajiri” kwa staili ya aina yake.



Inasemekana kuwa huko kuna kuku wa uganga ambapo “mteja” huchota punje za mahindi na kuzirusha chini; kisha kuku wa uganga huanza kuzidonoa. Idadi ya punje atakazodonoa ndiyo miaka utakayokuwa hai ukiwa na utajiri wa kupindukia.



Mbali na habari hii ya utajiri wa kudonoa (kama unavyojulikana kwa jina maarufu) vile vile tumekuwa tukisikia taarifa za watu kumiliki misukule ambayo inatumika kuwafanikisha kibiashara kwa kuiba fedha kutoka kwa wengine. Maeneo mengi imani hii ya misukule, majini ama ndumba, kuiba na kupeleka fedha inaitwa chuma ulete.



Pengine hii ni changamoto kwa sisi wataalamu wa masuala ya biashara. Haitakuwa busara kwa wataalamu na wadau wa biashara kukaa kimya, ama kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu na mawingu mazito namna hii.



Lazima tutafiti na kujiridhisha kuhusu suala hili. Je, kuna ukweli kiasi gani kuwa ushirikina unaweza kumfanikisha mtu kibiashara? Kama ushirikina hauna nafasi katika biashara, mbona kuna watu wanaoutumia na wanakiri kuwa wanafanikiwa?



Miaka kama minne hivi iliyopita nimepata kufanya utafiti mdogo kuhusu nguvu ya ushirikina katika biashara. Nilikutana na kuzungumza na waganga wa jadi takriban watatu hivi. Waganga wawili kati ya hao hawakuwa tayari kuzungumzia suala hili kwa uwazi.



Lakini mganga mmoja maarufu kutoka maeneo ya milima ya Livingstone niliyekutana naye mjini Makambako alikuwa tayari kunipa mawili matatu. Mganga huyu alikiri kuwa zipo dawa na utundu wa kijadi ambao humuwezesha mtu kufanikiwa kibiashara. Ingawa mganga huyu alisema wanatumia zaidi kanuni za kiakili (kisaikolojia) kuliko dawa.



Kwa mfano, mtu apewapo dawa hizi za utajiri hupewa masharti mbalimbali ya kiuganga. Baadhi ya masharti haya ni kama; “kutokula nyama” ambapo ulaji wa nyama huongeza bajeti na kupunguza faida.



Mara nyingine mganga anaweza kumpiga marufuku muombaji wa dawa hizi za biashara “Kutotembea nje ya ndoa”. Anachozuia mganga hapa ni utapanyaji wa mali kwa sababu ni vigumu mfanyabiashara uwe na kimada halafu usihonge, haiwezekani. Na sote tunafahamu kuwa kuhonga kunapoteza fedha na kupunguza mtaji.



Waganga wengi pia hupiga marufuku waombaji wa dawa hizi “Kutovaa nguo nzuri wala kulala mahali pazuri”. Hapa napo kuna janja! Kwa mujibu wa saikolojia ya walaji (consumer behaviours), ni kwamba mtu awapo na hela hujikuta anatamani kununua vitu vingi hata visivyo na umuhimu. Mganga anapomwambia mtu huyu kuwa asile wala kuvaa vizuri, ‘technically’ anakuwa akipambana na “consumer Behaviour” ya kupenda kutumia ovyo.



Waganga wengi wanafahamu kuwa pasipo kumdhibiti kisaikolojia mfanyabiashara huyu; anaweza kutumia ovyo hela ya mtaji na kujikuta biashara haikui. Ikiwa mtu hafanyi ‘shopping’ za gharama na ikiwa mtu hali vyakula vya anasa, ‘automatically’ ni kuwa fedha nyingi itabaki kwenye mzunguko na hivyo mtaji na biashara kwa ujumla kukua.



Kinachowasababisha watu wengi kuhangaika na kufuatilia ndumba katika biashara kunatokana na ukosefu wa elimu sahihi ya mambo ya kibiashara. Kanuni nyingi zinazotumiwa na waganga wa kienyeji zikitolewa kama masharti kwa wateja wao zipo katika sayansi ya biashara pia.



Kuna wakati waganga huwaambia wateja wao kuwa ili kuwapata wateja wengi katika biashara; waweke dawa katika milango ya kuingilia na kisha wahakikishe wanaongea vizuri na kila mteja anayeingia. Suala la kumjali mteja na kumchangamkia aingiapo katika biashara ndilo ambalo linazalisha wateja wazuri na wa kudumu. Hii ni kanuni katika sayansi ya biashara na kamwe dawa iliyotundikwa haina cha maana inachokifanya pale.



Kutokana na kuendekeza imani za kishirikina biashara nyingi zilizopo katika nchi yetu zinakuwa si za kudumu ama endelevu. Kwanza ni namna zinavyoendeshwa, na pili ni kukosa maono endelevu. Wafanyabiashara wengi wanaotumia ndumba katika biashara zao hawana mfumo wa uendeshaji (business management system).



Biashara ndiyo wao na wao ndiyo biashara. Kwa kuwa mganga alimwambia “dawa hii uweke katika droo ya mauzo na asishike mtu mwingine yeyote”, basi mfanyabiashara analazimika kuwapo eneo la biashara saa zote, ili kukwepa kukiuka masharti.



Wengi hawaajiri wafanyakazi na kuwaelekeza “A-Z” ya biashara zao kwa sababu ya masharti ya kipuuzi wanayopewa na waganga wa jadi. Wapo wafanyabiashara ambao hata wake zao hawajui namna biashara zao zinavyoendeshwa kwa sababu tu wameambiwa, “mke wako akishika fedha za mauzo akiwa kwenye siku zake za hedhi atakuwa amekiuka masharti na hivyo kufilisika.”



Tena mara nyingi mmiliki wa biashara anapofariki biashara zake humfuata nyuma (hufilisika). Utawasikia watu wakisema: Fulani alikuwa tajiri sana alipofariki, mke wake ama watoto wake walishindwa “kufuata masharti” ya mganga ndiyo maana wamefilisika.



Sehemu kubwa ya ukweli si kukiuka masharti ya mganga wa kienyeji, bali ni kushindwa kwa walioachiwa kuendesha biashara kwa sababu hawakushirikishwa katika uendeshaji wake wakati mmiliki alipokuwa hai.



Kuamini ushirikina imekuwa ni sumu mbaya kwa sababu watu wanabweteka wakiamini kuwa “ndumba” ni kila kitu. Kuna visa vingi tunashuhudia vya kufilisika kwa wafanyabiashara mbalimbali ambavyo huambatana na maneno kuwa huenda wamekosea masharti ya waganga wao.



Kumbe uhalisia ni kwamba huwa hawatambui kabisa biashara zina ukomo na bila kuzihuisha, kuziboresha na kubuni mpya; muda utafika nguvu ya soko itakulazimisha uondoke na kujikuta umefilisika.



Wengi hawana ushauri wa kitaalamu kuwajulisha: Je, biashara zao zinazalisha faida kiasi gani kwa mwaka. Je, hali ya masoko na ushindani ikoje na ina athari gani? Je, biashara zake zitakuwa na hali gani miaka mitano, kumi ama ishirini ijayo? Je, mikakati na mipango gani ifanyike kuhakikisha biashara zinadumu hadi kizazi cha wajukuu zake?



Wajasiriamali wanatakiwa kufundishwa elimu ya biashara ikiwemo namna ya kutafuta masoko ya bidhaa na huduma, namna ya kuendesha biashara katika mifumo rasmi, jinsi ya kushindana katika ulimwengu wa kistaarabu pamoja na utunzaji wa kumbukumbu za kimahesabu.



Kubwa kuliko yote ni namna wanavyoweza kufundishwa na kujizoeza kuwa wabunifu (creative and innovative) katika biashara zao.
 
Ungekuwa unamfahamu MWAKIPAANDE basi ungeweza kwa kiasi fulani kukubaliana na dhana ya wanaosema wakinga wanatumia uchawi ktk kufanikiwa kwao.

Sasa jitahidi sana umjue huyo mtu na historia yake
Mwakipande alishakufa siku nyingi!!
 
DOGO ENDELEA KUJIFARIJI KATIKA UMASKINI WAKO. WENZIO TUMESHATOBOA.
Dogo, mbona kama umetumia nguvu kubwa sana kubisha..unatumia nguvu kubwa sana kuwajibu watu,, inaleta ukakasi, mtu anaejua jambo la kweli na anafaham kua ni la kweli labda kwa namna moja ama nyingine hua hatumii nguvu kubwa sana kulidhibitisha.
 
Nadhani wewe unayeamini kwenye ushirikina ndo mshirikina dogo. Mimi naamini katika sayansi. Juhudi bidii na ufanisi pay. Nyie maskini washirikina sna.
We kumah tu. Kwanza unaita watu dogo huna adabu, na unajitapa una mafanikio..mafanikio gani wewe huku unalilia.mkeo apewe urithi ili wewe ufaidike, mara unaish kwa shemej yako mbwa wewe unaamka.asubuhi unaenda mezan kukimbilia chai iliyotafutwa na mme wa dadayako,,fala wewe usizarau watu mbwa wewe kmamakoh, ukinyooshea watu kidole angalia vitatu vinakuagalia stupid nikampoomp! [emoji867][emoji867]

 
Dogo, mbona kama umetumia nguvu kubwa sana kubisha..unatumia nguvu kubwa sana kuwajibu watu,, inaleta ukakasi, mtu anaejua jambo la kweli na anafaham kua ni la kweli labda kwa namna moja ama nyingine hua hatumii nguvu kubwa sana kulidhibitisha.
Dada sisi wanaume tunapambana nyie mnakaa kibarazani mnasema dawa wakati mkisukana.
 
Back
Top Bottom