Kwa wakongwe hawa miamba kulikoni utajiri wao umeondoka kama upepo; Mabasi ya Meridian, Mabasi ya Matema Beach: Sarfina n.k.
Kuhusu uhusiano wa utajiri na sadaka ni imani ambayo ipo kila sehemu duniani. Kuna tunaomini kuwa ukiwapa masikini msaada wa mali au pesa kwa nia njema au ukitoa kwenye nyumba za ibana mungu wa mbinguni anakulipa zaidi. Lakini kuna wanoamini kuwa ukitoa sadaka inayohusiana na uhai wa mtu unayempenda zaidi, au ukiikatili nafsi yako mwenyewe, shetani atakupa utajiri. Imani ya sadaka ya uhai au kufanya kitu kitakochokuondolea furaha katika maisha yako yote haipo tu nchini, lakini ipo zaidi India, China, Marekani na East Europe.
Mimi nina mifano ya mambo yenye mwelekeo wa kuhusisha ushirikina na utajiri;
Kuna suala la matajiri wengi kuvaa pete kubwa au kufuga paka ambaye anakuwa sehemu ya Biashara na analindwa kuliko kitu chochote.
Kuna baadhi ya nyumba hasa Iringa na tanga, kuna chumba maalumu haruhusiwi kuingia mtu isipokuwa baba na mama. Sasa kuna siku binti mgeni akaona kwa nini nakatazwa kuingia hiki chumba, wakati ankoo anaingia kila jioni? akazama alichokiona kilimfanya aondoke hiyo nyumba bila kuaga;
Soko la Kariakoo na mwanjerwa yalipo ungua, kuna wafanyabiashara walitoka madukani na wanyama hatari kama kenge na nyoka;
Kuna kipindi nilienda Beach yenye vichaka Bagamoyo nikakaa hadi saa nne usiku, nikaona kuna watu waume kwa kike wanakuja na magari, then wanavua nguo zote wanaanza kuoga maji masafi waliyokuja nayo then wanaelekea bahari hadi wanapotea. jinsi nivyochomoka hiyo sehemu mungu tu anajua;
Kuna sehemu Dar kuna mzee tajiri alikuwa anaogopwa na majirani zake wote, sasa mimi nikiwa sijui chochocte kuhusu hiyo nyumba, nikakatisha huo mtaaa. Nikakuta kuna dada kama house girl analia kuwa mtoto kaingia kwenye hiyo nyumbana kwamba anaogopa kumfuata, nikazama ndani, nilichokikuta mungu anajua. Baada ya kutoka nje na mtoto watu wakaanza kunizunguka wakinihoji nilichoona, sikusema kitu kwani mwenye nyumba alisema funga mdomo;
Kuna nyumba mikocheni kwa osama, kila mpangaji akipanga baada ya usiku mmoja anaondoka mwenyewe, sababu ni kupigwa fimbo au kulazwa nje. Sasa kuna siku wakaingia wachina, mwenye nyumba ndio alikuja kuwaomba msamaha asubuhi na wachina hawakuhama.
Miongoni mwa maeneo masikini zaidi Tz ni Makete, Kigoma na Pemba. Lakini watu kutoka huko ndio matajiri Wakubwa nchini. Utajri wa baadhi yao kamwe huwa hausambai kwa ndugu wa karibu na koo zao. wakifa ndio basi.
Kuna baadhi ya vijana wamefika mjini hawana kitu, lakini baada ya miaka miwili anajenga jengo la floor 10 kariakoo lenye value ya 5B. Sasa kinadharia serving ya 5B kwa miaka miwili ni ngumu labda uokote kipande cha almasi au uuze ngada kwa mafanikio makubwa.