Wako wapi mabodigadi na wapambe wa Makonda? Sasa anatembea peke yake vijijini. Je, ni laana ya Warioba? Vijana tuna la kujifunza

Mbona hayuko peke yake? Hapo ni nyumbani kwa mganga wake, mguse kama haukunata.
 
Maelezo yako hayo marefu lakini hakuna mahali ulipoeleza makosa hasa ya makonda aliyofanya!

Kukamata madawa ya kulevya na kutetea haki za wajane ndiyo huo mkono wa chuma unaodai alitawala?

Hakuna Rc baada ya Makonda aliyeiweza Dar kwa ubunifu na uibuaji wa miradi mbali mbali kama yeye.

Na kama basi hilo la Clouds ndiyo kutawala kwa mkono wa chuma, kumbuka hayo yalishazungumzwa wakayamaliza tena wakasameheana hadharani kila mtu analijua hilo.

Jambo lolote chini ya jua, likishaongelewa na kupatiwa ufumbuzi, kulirudisha tena mezani ndiyo majungu menyewe hayo!

Huwa kila siku najifikiri ni nini hasa cha mno alichowafanyia kibaya huyo mja huwa nakikosa.

Lakini sababu iliyomfanya Magufuli amlinde mpaka mwisho ni kule kuanzisha kwake vita pevu ya kumpiga vita shetani wa madawa ya kulevya.

Hiyo ndiyo sababu haswa iliyomfitinisha kwenye ndimi za watu mahasidi hadi leo kwa kugusa vyakula vyao haramu walivyozoea kuvila bila ya kufuta midomo!

Kiongozi yeyote wa umma anayepiga vita uharamia, ujambazi na dhulma zingine za mfano huo lazima tu atafutiwe visingizio vya kumvunja moyo na si ajabu sana kwa jamii hii iliyojaa roho za kifisadi na ubinafsi.
 
Nahisi anatafuta kura za wajumbe labda anataka kurudi bungeni naona kabisa huko kwao wanamuonaga kama Mungu wao wasukuma wajingawajinga sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…