Wako wapi mabodigadi na wapambe wa Makonda? Sasa anatembea peke yake vijijini. Je, ni laana ya Warioba? Vijana tuna la kujifunza

Wako wapi mabodigadi na wapambe wa Makonda? Sasa anatembea peke yake vijijini. Je, ni laana ya Warioba? Vijana tuna la kujifunza

Siku hizi watu wanachukua video wakati wa kuuwa?. Tatizo watanzania kutetea uovu tupo juu mpaka Marekani alipomuwekea ngumu ya kwenda kwenye nchi yake kwa sababu alizuia haki ya watu kuishi. Mpaka mgeni anaona wewe mwenyeji umeshupaza shingo.
Sababu iliyopelekea Makonda kuzuiwa kuinga Marekani “Ni kupambana na ushoga” sasa narudi kwako wewe, labda utuambie wewe ni shoga tujue moja.
 
Mnyenyekevu ni yule anayekubali kukosolewa na sio kujiona yupo sahihi. Kuhusu msamaha, Ni Magufuri ndio aliomba wasameheane pale Tanga na so vinginevyo, alikuwa na kiburi cha madaraka. Makonda alikuwa anadharau wengine hakuwa na roho ya Unyenyekevu ndio maana ameshuka mpaka kuwa raia wa kawaida. Alijiona mungu mtu kuwatukana watumishi wa umma hadharani mbele ya camera tena wengine wamemzidi umri.

Issue ya madawa ya kulevya ilikuwa siasa tu na kujifaisha tu. Wangapi walioitwaa kwenye listi yake wamehukumiwa jela?. Hakuna hata mmoja zaidi kaishia kuwatishia wahindi wampe hongo. Kiburi ndio kimemuangusha makonda mpaka chini.
Hapo tanga, Tanga Ruge Maskini
 
Makonda kawa kama chizi wapi?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Bavicha mna laana? Mtu kajikalia kimya anakula maisha nyie eti kawa kama chizi?

Mbona picha inaonesha kawa chizi. Tena chizi aliyekata tamaa ya Maisha.
 
Nawe wanakushughulikia kwa hilo neno pumbavu. Tuone umekaa kiumbeaumbea kama makonda mwenyewe utakuwa na matako makubwa sana.
Pole sana dogo, inaonekana kwa hasira zako hizi Makonda alikugonga na kitu chenye ncha kali
 
Le mobimba le mutus le commandant le field marshal
 
Hapo tanga, Tanga Ruge Maskini

Sijakuelewa. Tanga maana yake ilikuwa siku ya mkutano wa kutia saini mkataba wa Bomba la mafuta na mkutano huo ulifanyikia Tanga. Wakati Rais Magufuri akihutubia mkutano, ndipo alipowaita Ruge na Makonda wasameheane hadharani. Kweli walikuja mbele na wakapeana mikono Kama ishara ya msamaha.
 
Sio laana ya Mzee Warioba tu, bado wale aliowapora fedha zao na alioshiriki "kuhujumu maisha" yao
 
Sababu iliyopelekea Makonda kuzuiwa kuinga Marekani “Ni kupambana na ushoga” sasa narudi kwako wewe, labda utuambie wewe ni shoga tujue moja.

Wewe ndio shoga na familia yako. Acha mazoea ya kijinga. Ile statement uliisoma lakini?. Ilisema right to life, Yani haki ya kuishi. Alizuiliwaa kwa kosa la kuzuia wengine kuishi, maana kuua wengine. Ipo siku ukweli utakuwa wazi.
 
Nyie ndio mnaomuharibu Makonda. Baadala mkubali madhaifu yake na mumshauri ajirekebishe nyie mnatetea uongo. Nyie ndio mlikuwa mnamdnganya alipoangushwa kura za maoni na Ndungulile kuwa Rais atamrejesha?. Mshaurini huyo kijana ajirudi siku zingine asiongoze kwa dharau na kiburi, bali awe mnyenyekevu kwa wale anaowaongoza.

Makonda hakuwa na kujiamini chochote Bali Ni kiburi na dharau. Na hicho ndicho kilichomuangusha. Makonda aliambiwa na mkubwa wake ukigombea ubunge utakuwa umejifukuzisha. Kwa sababu ya kiburi akapuuza ushauri akaendelea kugombea ubunge na hatimaye kushindwa hadharani Kila mtu akiona.
Hivi kuna haja gani nifatilie maisha ya mtu, kinasaidia nini? Kila mtu anastili yake ya kuishi na kuongoza. Aliongoza kwa staili yake. Aliona inamfaa. Na pengine alikuwa na watu walio ona anafaa. Si wewe ukiona hafai basi na wengine wataona hivyo la hasha.
 
Maelezo yako hayo marefu lakini hakuna mahali ulipoeleza makosa hasa ya makonda aliyofanya!

Kukamata madawa ya kulevya na kutetea haki za wajane ndiyo huo mkono wa chuma unaodai alitawala?

Hakuna Rc baada ya Makonda aliyeiweza Dar kwa ubunifu na uibuaji wa miradi mbali mbali kama yeye.

Na kama basi hilo la Clouds ndiyo kutawala kwa mkono wa chuma, kumbuka hayo yalishazungumzwa wakayamaliza tena wakasameheana hadharani kila mtu analijua hilo.

Jambo lolote chini ya jua, likishaongelewa na kupatiwa ufumbuzi, kulirudisha tena mezani ndiyo majungu menyewe hayo!

Huwa kila siku najifikiri ni nini hasa cha mno alichowafanyia kibaya huyo mja huwa nakikosa.

Lakini sababu iliyomfanya Magufuli amlinde mpaka mwisho ni kule kuanzisha kwake vita pevu ya kumpiga vita shetani wa madawa ya kulevya.

Hiyo ndiyo sababu haswa iliyomfitinisha kwenye ndimi za watu mahasidi hadi leo kwa kugusa vyakula vyao haramu walivyozoea kuvila bila ya kufuta midomo!

Kiongozi yeyote wa umma anayepiga vita uharamia, ujambazi na dhulma zingine za mfano huo lazima tu atafutiwe visingizio vya kumvunja moyo na si ajabu sana kwa jamii hii iliyojaa roho za kifisadi na ubinafsi.
Ubaya huvuma kuliko wema
 
Baadhi ya watanzania hasa wa mitandaoni wanapenda viongozi legelege, na hawapendi mtu anaye jiamini. Hawapendi mtu anae wazibia maslahi yao yasi halali. Wamebaki kuongelea watu na umbea, usio wasaidia. Hata umuongelee vibaya huyo Makonda, utafaidika na nini, au utampunguzia nini? Alisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar. Alifanya kwa nafasi yake alofanya. Atabaki katika historia. Kwa sasa anamaisha yake hajaja kwako kukuomba fedha au kulialia. Anaenjoy maisha yake.
Ya Mungu mengi hujui kesho. Makonda bado ni kijana uenda akarudi tena madarakani. Tusiongee sana, tuwe na akiba ya maneno!
Kabisa mkuu hii ndio dunia
 
Back
Top Bottom