Wako wapi waliodai Tume ya Katiba haina weledi na wala si huru!??

Wako wapi waliodai Tume ya Katiba haina weledi na wala si huru!??

Duh, Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Kweli kuwa na akili za kibavicha ni hasara kwa taifaKwa mawazo yako, watu wanaotakiwa kuijadili rasimu kwa akili yako, unataka rasimu iwajadili wao.Bila aibu uko mbele kutoa ushauri kwa Nape Nnauye.
Masalia you know you cant be accepted back: why are you still paining about Bavicha move on and live your life
 
......(3) Muundo, madaraka na mambo mengine ya kiutendaji yahusuyoSerikali yaTanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yataainishwa
katika Katiba za Washirika wa Muungano.

Katiba ya Tanganyika itaanza kuandaliwa lini na itapitishwa na chombo kipi? Zanzibar tayari wana ya kwao Nape Nnauye

Kumuuliza Nape swali gumu namna hii ni kumuonea sana ! Hebu swali lako mpelekee Profesa SHIVJI .
 
Tatizo la Nape akishatoa pumba hapa hukimbia kujificha huku akisoma comments zetu kwa mbaali. Mengi yamenenwa na bila shaka mwenye masikio amesikia na mwenye macho amesoma
 
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!
Dah,Nape kwenye AVATAR yako nawaona waziri wa mali asili wa zamani,MH.Kinana,na wewe,mbona umewasahau Mh.malima na Mh. Mtutura, kwenye safari ya kuelekea ruaha game reserve?
 
Usizungumzie matukio ya mwaka huu, jikumbushe historia au kwa kukusaidia pitia kesi na hukumu ya Jaji Kahwa Rugakingira, na tume za (Nyalali na Kisanga) jinsi CCM ilivyoingilia kuzuia mgombea binafsi na mambo mengine.

Wewe kijana una akili mno , umeenda mbali kuliko macho ya Mwanadiwani yalipoishia !
 
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!

Bado mchakato ni mrefu na maamuzi magumu bado yanahitajika. Kuna vipengele vingi vya kurekebusha, watu wamekimbilia kushangilia sana sana kwa vipengele hivi, (i) Kurudi kwa Tanganyika (ii) Ukomo wa Mbunge na Mbunge kutokuwa Spika/Naibu, (iii) Kupunguza baraza la Mawaziri la Muungano.

Lakini bado kuna mambo mengi ya kuangalia wewe umekimbilia kutoa maelezo ya ushabiki zaidi.
(1) Suala la kuteua majaji bado ni kitendawili
(2) Suala la kupata wajumbe wa "Tume Huru" ya uchaguzi pia ni kitendawili kingine.
(3) nk nk nk.

Mkuu, ni bora kukaa kimya mpaka mchakato utakapokwisha, kwani nina Imani wananchi kupitia mabaraza ya katiba, wanaweza wakaja na mambo mengi wananayoyataka wao na ukabaki umeduwaa na tume ikayachukua vile vile.

Safari bado ni ndefu, though it is a good start!
 
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi
Mmoja wao huyu hapa...
"@ LE MUTUZ LIVE HARD STRAIGHT TALK!!:-

AT SOME POINT SERIKALI YA CCM NI LAZIMA IWAKUMBUSHE KAMATI YA KATIBA MPYA KWAMBA WAO WANACHOWEZA KUFANYA NI KUPENDEKEZA TU NA SIO KUAMUA UAMUZI WA MWISHO, NIMEISOMA RASIMU LAST NIGHT,
IMEJAA MADUDU MENGI SANA AMBAYO NI PURE NONSENSE!!, SERIKALI TATU KWA PESA GANI TULIZONAZO BONGO? NI NCHI GANI DUNIANI IMEENDELEA KWA HARAKA KUTOKANA NA KUWA NA SERIKALI TATU?

SERIKALI YA SASA INATUPA SHIDA ITAKUWA TATU? INA MAANA KILA SERIKALI KATI YA HIZO TATU LAZIMA IWE NA KATIBA YAKE NA WAAMUZI WAKE? WANANCHI MILLIONI 45 UNAWAWAKILISHAJE BUNGENI NA WABUNGE 75 TU? KAMA SIO INSANITY NI NINI HASA? SPIKA ASIWE MWANASIASA FOOLISH IDEA NI NCHI GANI DUNIANI ILIYOENDELA AMBAYO SPIKA WAKLE SIO MWANASIASA WA CHAMA CHOCHOTE PALE NCHINI?

SIKU MOJA NILIENDA KWENYE MKUTANO WA HIYO KAMATI NDIO NIKAAMUA SITARUDIA TENA,
IMEJAA VIONGOZI WENYE HASIRA YA KUKOSA MLO NA SERIKALI YA SASA, WEWE MTUMZIMA NA AKILI TIMAMU LEO MWAKA 2013 UNAWEZAJE KUSEMA SPIKA WA BUNGE ASIWE MWANASIASA KAMA SIO KUFILISIKA IDEAS?

- MIMI NINGEKUA RAIS JUZI NINGEIMALIZA ILE KAMATI YA KATIBA NA KUWAOMBA WAONDOKE HARAKA SANA, NINGECHAGUA WANASHERIA MAARUFU HAPA NCHINI KAMA 10 NA KUWAPA JUKUMU LA
KUUNDA KATIBA MPYA BILA MIKUTANO WALA HOUTBA ZA KILA SIKU ZA RASIMU, WHAT IS RASIMU YA KATIBA KAMA NONSENSE? 80% YA MAPENDEKEZO YA RASIMU YA KATIBA NI WASTE KWA TAIFA, SERIKALI UWAONDOE HAO KATIBA NOW KABLA HAWAJATULETEA MATATIZO NA MAPENDEKEZO YASIYO NA TIJA KWA TAIFA, HAKUNA TIJA KWA TAIFA KUWA NA WABUNGE 75 KUWAKILISHA WANANCHI MILLIONI 45 NI PURE NONSENSE!!, MUNGU AIB ARIKI TANZANIA!! - LE MUTUZ "
 
Wewe unayejifanya kuwa na busara wakati huna hata tone la busara zaidi ya matusi.

Kwa akili yako hii finyu, unafikiria watu wa kijijini ndiyo wanapenda majungu.

Hebu tuambie wewe wa mjini usiyependa majungu umeweka input gani katika rasimu.

MwanaDiwani una roho ngumu sana kumtetea Nape kwenye hili aisee !
 
NAPE ataacha lini kuharisha hapa jukwaani na kukimbia bila kujibu maswali yetu?
poor ccm!!
 
Naungana nawe Nape kwa sasa, hayo unayoyaona kuwa mapendekezo mazuri ya katiba tunayoitarajia yaendelee kuwa hiyo , wale wajumbe mliowapitisha kwa nguvu wa mabaraza ya katiba watakosoa sana, najua kwa ccm hawawezi kufurahia maoni hayo. Kawaida ya chama chako ni kufanya kile kisichopendwa na watu wengi
 
Me sio mwanasiasa lakini Nape kakangu sincerely unapenda umbea,yani mada imeka kidaku daku hivi
 
Nape Nnauye , Habari za siku mkubwa.

Kwanza hakuna aliyesema unnayoyasema hapa, ila malalamiko ni mabaraza ya katiba yaliingiliwa na makada wa CCM mmoja wapo ni mama yangu, dada yangu Asha rose Migiro na wewe. Mliwatengeneza watu wa kuingia kuyapigia kura haya maoni. Naomba utafute matamko ya wote waliopinga utajua wapi walipinga. Mpaka sasa tunapinga upatikanaji wa watu watakao jadili na kuyapitisha haya maoni. Je kweli watayakubali wakati wengi ni makada wa kuingizwa wa CCM?

Tutafurahi wengi kama mtawaelekeza makada wengi kuzingatia maoni ya watanzania.

Maoni yangu binafsi sikubaliani na uwakilishi wa wanaume na wanawake kwenye majimbo utaongeza gharama kubwa sana za kuendesha bunge. Kama nimeelewa vyema yaani kuwe na wawakilishi wa kike na kiume kwenye jimbo moja. No huu utakuwa ni mzigo kwa walipa kodi. yaani majimbo 239 yatoe wabunge 478??? come on haiwezekanai. ni wengi mno ukilingisha na uwezo wa nchi. Nilitegemea tume ingepunguza majimbo ya uchaguzi na kufikia walau 70 au 100. ya kudumu.

Nape tujadili hizi rasimu Tanzania ni yetu wote, wewe utapita, Jk atapita, Lowasaa atapita , Membe Atapita ila Tanzania bado tunayo sana, msifikiri ninyi viongozi wa sisasa mna maana sana zaidi ya maisha yetu la hasha ninyi mnatetea ajira tu hamna la maana mnalilifanya, hamtetei taifa, wananchi wala ustawi wa tanzania. hamna uchungu na uhalisia wa maisha magumu ya Mtanzania.

ndio maana hamjali kushuku kiwango cha elimu manapendekeza utumbo wa kuwaongezea wanafunzi alama. Tukishindwa kuwaandaa vijana wetu leo kwanini kesho tulalamike kuhusu huduma za afya, barabra, mahakama , waalimu wabovu?? Kama leo tunashindwa kuandaa wataalamu kwanini kesho tushangae ghorafa zikituangukia ?? Nape serikali yenu imeshindwa vibaya sana. Na ninaomba miradi yote ya viongozi walioshiriki kuuwa elimu ya nchi ife kwa ukosefu wa utaalamu labda mtajifunza. Nape leo mnafurahia kutibiwa nje na kuiuwa Muhimbili na hospitali zote za ndani, ila ukumbuke kesho mnastaafu uwezo wa kwenda nje kwa fedha za walipa kodi masikini mtakuwa hamna. Najua wote mnapigana vikumbo kutuibia ili kujaza mafedha ya kesho mkiwa nje ya siasa za kibazazi.

Ila Iko siku watanzania watadai fedha zao kwa nguvu.
kaka mchango wako ni mzuri ila hapo kwenye majimbo hujaipata tume vizuri,imepunguza majimbo kutoka 170 hadi 25 kwa hiyo kila jimbo likitoa ke na me jumla ni 50 ukiongeza 20 znz na 5 wa rais kutoka katika makundi ya walemavu jumla ni 75.punguza kwenye 300 na ushei wa sasa unaweza kuona kuwa hata mil 20 kwa mbunge tunaweza lipa bila wasiwasi.
lakini kwingine upo vizuri.
nape mpuuzeni kwa sababu amesahau ni mawaziri wa chama chake waliosema katiba ya sasa inatosha na wengine wakasema serikali haina hela lakini hao chadema wakakkza kamba mpaka kikatoka hiki tunachokiona lakini tunamwambia kazi baaado,tunataka kila kitu kiwe wazi pccb,dpp,majaji nk panyooshwe hapo na katiba.
na asisahau hata mchawi ukimshikia bango hawezi loga watoto wako na hicho ndicho chadema walichosimamia.
 
EH NAPE, YOU THINK VERY LOW, YOU TALK VERY LOW, Mungu akusaidie kama una watoto au utakapojaliwa wisishike akili zako, watawataabisha waalim darasani, sijui kama umekisoma kwanza ulichokiandika; kwanza kwani ndio katiba imekamilika hapo?! si ni rasimu tu hiyo! kha, style uliyoamua ni vijembe na mipasho kwa kwenda mbele? hujali tena kuwa kuna jamii inakusikiliza na kukutizama unchofanya na unachoongea? ifike mahali ujirekebishe, mbona unaonekana sio mdogo ki-hivyo?
 
Rais lazima hashitakiwe,wakuu wa mikoa hasiwachague.acha wapigiwe kura kama wakuu wa majimbo kwenye nchi zilizo nyingine.wanaitwa gavana.
 
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!
Nape Nnauye Mbona unaongea kishabiki sana, kuna maoni magapi ya chama chako yamezingatiwa? au ni maoni gani yamekukuna sana! Mimi naona kuna maoni mengi ya wapinzani yameonekana kuwa na maana kuliko ya ccm!
 
Last edited by a moderator:
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!

Jamani uwezo mdogo wa kifikra wa Nape mnaujua naombeni msibishane nae.
 
Hofu yangu msije kuchakachua kwenye mabaraza ya katiba. Hiyo ni rasimu tu na hayo ni mapendekezo ya Tume na wananchi. Sidhani kama nyie ccm mmefurahia maoni hayo. Tungoje Bunge la Katiba loikae lijadili hayo na tuone yakibaki kama yalivyopendekezwa na si kukurupuka kuanza kusema watu kimafumbo hapa, ndugu Nape.

Hivi huko kwenye mabaraza inaenda tena kufanya nini, si tayari Tume imejumuisha maoni ya watanzania, sasa nini tena cha zaidi?? Haya mabaraza ni wastage of time and resources, wataichakachua bure!!
 
Yani huyu jamaa huwa namshangaa huwa anaongea kama ye ndo chama pinzani mfano ajenda ya majimbo ya CDM ni mradi wa wakubwa maneno kama hayo yalitakiwa yatajwe na chama pinzani anaongea kana kwamba CDM wameshachukua nchi na kuanzsha mfumo huo.... huyu jamaa alipaswa kuwa baloz wa nyumba kumi sio katibu chama kikubwa kama CCM
 
Ninasubiri kwa hamu kubwa kuwasikia waliosema kwa sauti kubwa nahadharani kabisa kuwa Tume ya Mabadiliko ya katiba nchini haina watu wenye weledi kwa kazi hiyo tena wakaenda mbali kuwa haiko huru tume hiyo kufanya kazi wanayotakiwa kufanya. Sasa baada ya rasimu hii natamani kuwasikia tena wakisema nakurudia maneno yale na pengine kwa kuyapigia mstari mkubwa!!
Nape you are an idiot. Haya ni mapendekezo tuu. Mambo baado kabisa.
 
Back
Top Bottom