Tuseme tu ukweli.
CHADEMA ya Lissu na Heche walikuwa mbele sana ya wakati kudai Reforms kabla ya Uchaguzi.
Wakati kina Stephen Wassira, Amos Makalla, Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria, Jenista Muhagama, Hamza Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Baba yao anayepanga nani awe nani Tanzania Jakaya Kikwete wakijinasibu kuwa Reforms zimefanyika hakutakuwa na kuondoa Wagombea na Upinzania Lissu na Heche walitusanua Wananchi mapema sana kuwa ule ulikuwa ni mchezo wa danganya toto maana hautaondolewa moja kwa moja na Tume bali kupitia mapingamizi mengine.
MUNGU si Athumani wala Mzee Mgaya, mangalizo na maonyo waliyatoa Chadema hasa Lissu na Heche yamekuja kutimia ndani ya miezi minne tu.
Leo Luhaga Mpina mgombea wa Urais kwa ticketi ya ACT Wazalendo amekatwa na kuenguliwa kwa njia ile ile waliyosema Chadema itatumika.
MUNGU awabariki sana Chadema. Hiki chama kweli kinafanya kazi ya Mungu nchini Tanzania.
No Reforms No Election ✊️✌️