Dini gani inasema mtu akifa anakuwa mzimu?Hizi dini nimeachana nazo tangu 1999 baada ya kutumika kwa miaka mingi. We jiulize swali dogo tu, eti mtu akifariki wanamwita mzimu! Yaan leo baba yako akifariki ndio mwisho wa kumuita baba? Akili ni zako chagua mwenyewe ila najua mwisho wa siku wataumbuka baada ya waafrika kujitambua
We labda huelewi leo ukimfanyia sherehe au tambiko marehemu unaambiwa unaabudu mizimu pia ukienda kutambika Makaburini unaambiwa unaomba mizimuDini gani inasema mtu akifa anakuwa mzimu?
huenda uko sahihi lkn weka akilini kwamba dini hazitokani na Mungu, wala Mungu hatokani na dini, dini ni mawazo ya wanadamu juu ya Mungu, Mungu sio dini wala dini sio Mungu, wakoloni walitumia dini kuwa kinga ya kupanua himaya ya tawala zao, wakoloni hawa bila soni, walianza kupora mali za wa afrika wakatuachaa waafrika tukiwa hoi huku wakijigamba kuwa wao ni watumishi wa Mungu kumbe ni wachumia tumbo tu, hawakuishia hapo walienda mbali hata kuchoma moto nyaraka za historia ya waafrika kwa madai kuwa zilikuwa nyaraka za mashetani,Hii ni dalili ya kuchoka na maisha. Watanzania tumeanza kufa pole pole na chanzo cha kifo hicho hamtakijua kamwe. Mleta mada inaonekana anafikiri sana lkn khali mbaya ya maisha imemfikisha hapo alipo.
Mtoa mada as if u are reading my mind ,,binafsi nakiri umekomboleka na pia endelea kukomboa ,hoja yako nzito sana kwa jinsi ambavyo waafrika dini zilivowaingia inahiyaji nguvu ya ziada ,,umetema ukweli ""kwa wakristo wenzangu unabiwa FUNGU LA KUMI " hapo watu bora alale njaaa ili atoe fungu la kumi waliwaweza kwangu dini hainiendeshi
Wewe ulisema kwamba dini zinasema kwamba marehemu ni mizimu,maandiko yako haya hayaelezi ni kwa vipi dini zinasema marehemu ni mizimu kwakuwa kwanza hayo ni maneno ya wanadini siyo dini zenyewe kwa maana ya vitabu....We labda huelewi leo ukimfanyia sherehe au tambiko marehemu unaambiwa unaabudu mizimu pia ukienda kutambika Makaburini unaambiwa unaomba mizimu
Umeandika maelezo mengi lakini sijaona umuhimu wa maelezo yako haya kutokana na nilichokisema hapo mwanzo.....mkuu Eiyer kabla ya afrika kuvamiwa na wakoloni afrika chini ya uongozi wa Mafarao, lilikuwa bara linoongoza kwa tekenolojia na maendeleo duniani, miili ya mafarao waliokufa miaka 3,000 iliyopita ilipakwa dawa ikazikwa haijaoza mpaka leo, maarifa haya leo hayakupo duniani na afrika wakati huo ilikuwa ikiongoza kwa sayansi na utawala bora ikiwa na taasisi nyingi za utafiti wa kisayansi ambazo dini za kigeni mujibu wa dini za kigeni wanaziita Mungu, afrika imewahi kutawala dunia kwa miaka isiyopungua 18,000 au zaidi, tangu hapo afrika lilikuwa bara tulivu kutokana na asili ya watu wake kuwa waungwana na watulivu, (watu weusi)Tawala za afrika zilikuwa tawala za kidemokrasia waatu wake walikuwa na uhuru wa kutoa mawazo yao mradi havunji sheria za nchi, waaafrika wana asili ya utu wema, upole, ni waungwana, wakarimu, hawana asili ya ubaguzi, kama wangelikuwa ni watu wabaguzi, Yusufu wasingempa kazi ya uwaziri mkuu wa nchi yao.
Mambo yalianza kubadilika baada ya Warumi kuchukua dola kutoka mikononi mwa wagiriki waarumi walianzisha utawala wa sheria, mfumo uliowafanya wawe maarufu na kupendwa sana duniani, kwawa bahati mbaya,watawala hawa walijisahau, wakajiingiza katika starehe naufisadi hapo ndipo sayansi, utawala bora na democrasia vikatoweka, badala yake starehe na ufisadi ikawa ndio dira ya watawala, watanashati, wakaasisi siku kuu nyingi za mapumziko kitaifa, siku kuu hizo zilisherehekewa kwa ngono na ufisadi, Moja wapo ya siku kuu za aina hiyo ilikuwa siku ya tarehe 25 Desemba, siku kuu hizo, nyingine zilipigwa marufuku nyingine kubadilishwa kama ile ya Tarehe 25 December ambayo ilibadilishwa ikawa siku kuu ya Chrismas siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu,
kupitia dini walitukandamiza wa afrika wakapanua dola yao kwa kisingizio kuwa wametumwa na Mungu, wazungu walikuwa watu wa kwanza kufika afrika kuleta dini, walitumia ulaghai mwingi kulaghai watu kuzisadikisha dini zao, waarabu nao walipoleta dini, walitumia ulaghai ule ule uliotumiwa na wazungu kusadikisha dini zao, pamoja na kutumia ulaghai mwingi, pia waarabu walitumia mabavu kusadikisha dini yao, yaani jihad, walifanya mauaji ya kikatili ya hali ya juu, mfano mzuri ni pale walipovamia afrika kaskazini, walichinja watu kama watu wanavyochinja kuku, waliwaona watu weusi kuwa nimashetani makafri hawatokani na Mungu, wakidai kuwa wao wametumwa na Mungu kuleta dini, huu ni ushenzi wa hali ya juu waliotufanyia hawa watu na dini zao,
Wewe utakuwa mchawi aiseeee matambiko gani hayo mtu kashakufaWe labda huelewi leo ukimfanyia sherehe au tambiko marehemu unaambiwa unaabudu mizimu pia ukienda kutambika Makaburini unaambiwa unaomba mizimu
Ni sawa lkn utamaduni wenu unakuongoza kufanya maBnafsi dini imenisaidia sana malezi yao walivyonielekeza na kunielea kiutu na kimaadili ni mtu muhimu sana ktk position yangu kama mtumishi wa umma na mwanadamu kweli ninayejiheshimu n kuwaheshimu wenzangu
Umeandika maelezo mengi lakini sijaona umuhimu wa maelezo yako haya kutokana na nilichokisema hapo mwanzo.....
Kwanza nilikuambia kuwa Ukristo siyo dini ya wazungu..
Pia,Nilikuambia kwamba,hao wazungu wakati wanakuja huku Afrika hiyo karne ya 17 tayari huku Ukristo ulikuwepo,labda uniambie tu kwamba walipeleka Ukristo baadhi ya maeneo na siyo kwamba walileta Ukristo hapa Afrika....
Lakini zaidi nilikuambia kuwa Ukristo hajawahi kumfanya mtu akaacha mila zake,kama wazungu walikuja na ulaghai hilo ni suala lingine...
Hebu niambie dini hii inakandamizaje watu na kuwafanya waache mila zao na desturi zao na hatimaye kuwa watumwa wa desturi zingine?
Kwanini hatukusikia habari ya utumwa wakati akila Luka wanakwenda Libya?
Kwanini hatukusikia habari ya watumwa wakati akina Barnaba wanakwenda Ethiopia huko?
Unachokiongelea wewe hapa hakikusababishwa na Ukristo hivyo weka hoja yako kwa namna nyingine ili upate michango sahihi.Tatizo la Waafrika halijasababishwa na Ukristo bali mambo mengine tu....
Hebu tuanze na kueleza hapa kwetu Tanzania,hebu tufafanulieni ni vp kwamba tupo hivi tulivyo kwa sababu ya ukristo na uislamu. Hebu tupeni uchambuzi wa umasikini wa Tz ni vp dini hizi mbili zimehusika.
Mkuu mbona unaponda dini badala ya kueleza hatua kwa hatua jinsi dini zilivyofanya Tz ikawa masikini?Dini zina husika sana kwa umasikini afrika na Tz, zinafundisha vitu vingi ambayo vinamfanya mtu akili yake idumae, huwa nasema dini na wapiga ramsli ni kitu kimoja, wote hawa wanafanya biashara za kuuza pepo, wote hawa wanapandisha pepo, pepo linapowapagaa wana dini, dini hudai ni roho mtakatifu wa Mungu, ni pepo wazuri, lkn pepo wanaopandishwa nje ya dini za kigeni yaani wapiga ramli dini zinadau kuwa pepo hao hutokana na mashetani, hao wote wanadini na wapiga ramli asili yao ni ujinga kwa sababu wanaimarisha ujinga miongoni mwa binadamu, si wanadini wala wapiga ramli wanaruhusu binadamu kuhoji mambo yao, wanadai mambo yao wanoyafanya hayahojiwi, ukihoji wanadai unampinga Mungu na kujitafutia laana kwa kuhoji unamkufuru Mungu.
dini inawambia watu watamani vitu kutoka juu mbinguni wasitamani mali za dunia, hawa wana dini hawa kuishia hapo walihakikisha kuwa waafrika wanauona na kuuhesabu utajiri sawa na mavi, ukiacha hayo wanatufundisha kuwa watakatifu wote wataishi mbinguni kwa maisha ya umilele, umilele wa maisha haya hutofautiana kati ya dini na dini, mfano dhana wakikristo wasema, mbinguni hakuna kufa, hakuna kula wala kunywa ni kuabuda na kusifu tu, kwa waislamu wao wanadai kuwa maisha ya umilele mtu atapata thawabu ya kukaa katika bustani iliyo na majani mabichi yenye mito inotiririsha maji mengi, watahudumiwa kwa vinywaji vitamu, huduma itakayokuwa ikitolewa na wanawake warembowenye macho makubwa km vikombe, kwa ufupi dini na wapiga ramli wote ni kitu kimoja yaani dini ramsli, ramli ni dini
Kwanza mwaka 3020 A.D haujafika nadhani ulikuwa unamaanisha mwaka 320 au 302 labda...1. Ukristo sio dini ya wayahudi, ni dini ya wazungu, wkati warumi walipoutaifisha ukristo mwaka 3020 AD, wakaufanya ukristo kuwa itikadi ya Ulaya, Ukristo huo huo ulipoingia marekani ukawa biarasha.
Hapa umenisikitisha sana na inaonekana umeanzisha thread ambayo huna kabisa elimu ya kutosha kuhusu ulichokianzishia thread...2. Unapotaka kuwa Mkristo, ukristo unakulazimisha kuacha jina lako la asili na kuchukua jina la kizungu au kiyahudi
Duh!! Wewe ni noma...3. Utumwa ulikuwapo ndio maana Paulo ana sema hivi enyi watumwa watiini mabwana zenu,
Una hokiandika hapa nakijua pengine kuliko hata wewe na ndiyo maana nasema kwamba hii thread huna uelewa nayo kwa namna ipaswavyo....halafu unaposema matatizo ya waafrika hayakusababishwa na dini unajua historia vizuri? km unajua historia, katika karne ya 17 wa misionary waliagizwa wawafundisheje waafrika?
Mito hii imeandikwa hapo na hii inasababisha nisielewe mantiki ya swali lako,labda unataka kuniuliza hii mito ni ya eneo lipi,itakuwa vizuri kama ukiliweka swali lako vizuri....MWANZO sura 2. mstari wa 10, unasema hivi ukatoka mto mmoja ukamwagilia bustani ya edeni, kutoka hapo ukagawanyika katika viunga vinne, ambavyo ni Gishoni na Pishoni, Euphrates na Tigris hivi wajua mto huu ni mto gani?,
Nakuunga mkono kwa asilimia zote.
Dini ni moja ya alama ya utamaduni[Cultural element]
Ni kama ilivyo lugha, mtindo wa mavazi, mila na desturi n.k.
Sasa walipokuja wazungu, wakaanza ku-undervalue kila kilichokuwa cha mwaafrika,
Waka waambia waafrika lugha zao ndo bora zaidi, dini zao ndo bora zaidi maana zinatoka kwa Mungu tofauti na za waafrika zinazotoka kwa Shetani.
Hata majina ya waafrika yalidharaulika na kupewa yale ya waleta dini.
Dini hazikuwa na lengo la kufanya penetration ya ukoloni pekee bali kumtawala mwaafrika milele.
Dini ni aina ya utawala kama zililvyo tawala zingine.