Wakoloni walituletea dini kama kinga kwao ili watutawale

Mkuu ukiulizwa A unajibu C.

Sijaona maana ya kujakueleza tafsri yako ya neno imani,jamaa una majibu mepesi kwenye maswali magumu.
sina hakika km tunaweza kuelewana aiseee yaani dini imekuingia sana tatizo ndio sababu tunashindwa kuelewana
nishakwambia mara kadhaa dini sio Mungu,
 
watu hali mbaya mpaka wanaanza kukufuru, Muombe Mungu japo huna imani hiyo akusaidie , daaaaa ugumu wa maisha ni kipimo cha akili
mkuu kufuru ndio nini? na nanni anayekufuriwa kwenye huu uzi?
hivi ndivyo wakoloni walivyowaagiza wa missionary wawaambie kuwa msihoji jambo lolote linahusu dini, mkihoji mnakufuru, ujinga wa hali ya juu huu
 

mkuu hebu nisaidie na wewe maana kuna watu hapo juu hawataki kunielewa sijui ni kwa makusudi au la, dini ndio chanzo cha umasikini huo ndo ukweli, kwa sababu zinawafundisha watu kuwa wasihangaike na vya duniani bali wahangaike na vilivyo juu, kutothamini mali zilizo chini ya ardhi yaani madini na vingine na kuwa utajiri wote uliopo duniani hauhusiani na Mungu, tena mafundisho haya huwa yanakaziwa kweli kuthamini mali au utajiri ulioko duniani ni chukizo kwa Mungu. (lkn wao wana magari ya kifahari, nyumba, maisha mazuri, watoto wao wanasoma nje, wana ndege nk)

mafundisho ya aina hii ndio yameharibu watu, wengine wao ni wavivu wa kujishughulisha wakisubir siku wakifa wataenda kuishi maisha ya milele ambako huko ni kusifu na kuabudu tu, wengine hawataki kusoma wanadai dunia imeisha YESU yuko karibu kurudi kwa hiyo hataki kujisumbua kwa neno lolote, isipokuwa anataka kusali na kuomba tu akimsubiri YESU (ndo hao wanolala makanisani hawafanyi kazi)

binadamu anatakiwa elewe na kuamini moyoni mwake kuwa Mungu yupo, roho yake ni mali ya Mungu, isipokuwa mwili ni mavumbi ya ardhi, watoke wafanye kazi, waache kulala makanisani na misikitini Mungu hatumikiwi hivyo, watafute pesa wawasaidie wanohitaji msaada pale wanapojiweza, wahakikishe wanatenda mema maishani mwao, watende haki na waitetee haki, ahakikishe ana chukia na kuachana na mabaya yote, awapende binadamu wote bila ya kuwabagua nk, huko ndiko kumtumikia Mungu.
 
nadhani hujamuelewa huyo ndugu, ni kweli kuwa dini na Mungu ni vitu viwili tofauti ila dini ni njia ambayo wanadamu tumejiwekea ya kumfikia huyo Mungu ingawa sio lazima sana kwani kuna watu wanawasiliana na Mungu moja kwa moja bila kupitia dini
Nimemuuliza ni ujumbe gani ambao hao akina Musa Yesu na Muhammad walikuja nao? hajanitajia huo ujumbe.

Wala hajanitajia ni kipi cha kututhibitishia kuwa huo ujumbe ni kutoka kwa mungu,ajabu bado mnaendelea kuniambia kuwa kuna bado wanaendelea kupokea au kuwasiliana na mungu.

Ukiangalia dini zinaelekeza mfumo gani wa kuishi hapa duniani vile ambavyo mungu ameelekeza tuishi hivyo na huo ujumbe wa mungu unapitia njia hiyo, sasa mnachotaka kukieleza nyie mnashindwa kukiweka katika kuendana na uhalisia ili kilete maana.
 

Mkuu,

Tusaidie kidogo,
Tukitaja Afrika tunamaanisha nini na waafrika ni watu gani?
 
sina hakika km tunaweza kuelewana aiseee yaani dini imekuingia sana tatizo ndio sababu tunashindwa kuelewana
nishakwambia mara kadhaa dini sio Mungu,
Na nyie wengi mna tatizo la kuona mnaelewa sana,na huwa mnashindwa kuwaelewesha kuelewa hicho mnachoelwa matokeo yake mnaona watu sio waelewa kumbe tatizo ni nyie mnashindwa kuelewesha.

Kwa maelezo gani ya kina uliyoyaeleza ambao ulitaka mie nifikie kukubaliana na unachokieleza? au wewe unataka nikubali tu unachokieleza bila kukuhoji ili nielewe?
 
fact[emoji106]
 
hachana na hawa waliokuja jana au juzi,,sisi tunazungumzia wale waliokuja enzi za ukoloni na kuleta dini iliyowafanya babu zetu kuwa inferior/wanyonge mbele yao ili wawatawale na kuwanyonya kiraisi,,,kamwa huwezi nibadilisha mawazo kama"THE TRUE AND GENUINE WAY OF WORSHIP GOD IS ONLY THE TRADITIONAL WAY OF OUR ANCESTORS" ila hizi zingine zimeletwa na wapigaji tuu!!!
 
Musa, Yesu na Mohamed ni watu, ni binadamu km ulivyo wewe, kila mmoja aliwakilisha mtazamo wa Mungu km anavyoufikiria yeye, ndio maana kunatofauti sana kati ya hawa watu,
uKRISTO unasema Yesu ndiye mwanzo na mwisho
Uisilamu unasema Msujudie Mungu na Mtume wake (Mohamed)
Musa msimamo wake ni wa Mungu mmoja na wala si Miungu mitatu,
mitazamo hii ya kibidamu si ya Ki Mungu

Mfumo wa maisha ya mwanadamu wa ki Mungu ni kupitia Sayansi, maana Science hushughulika na maendeleo ya watu walio hai, isipokuwa dini inahangaika na watu walio wafu,

katika kazi zote za ki sayansi, wana sayansi huwa wanaafikia na kuwa na msimamo mmoja katika mambo yao yote, lkn wana dini hawajawahi kukubaliana na wala haitakuja kutoa kukubalia ktk jambo lolote lile wanalodai kuwa ni la ki Mungu
 
Mkuu,

Tusaidie kidogo,
Tukitaja Afrika tunamaanisha nini na waafrika ni watu gani?
Afrika ni neno la Kilatini, lenye maana ya mtu alyeungua MWEUSI, hivyo inapotamkwa/kutajwa Waafrika ina maanisha ni mtu/watu weusi
 
Duh! haya twende hivyo hivyo.

Ulisema mwenyewe kuwa akina Musa Yesu na Muhammad walikuwa wanaleta ujumbe kutoka kwa mungu na walipewa karma na ukawataja hadi akina Nyerere. Sasa ndiyo maana nikauliza huo ujumbe ni upi waliyokuja nao kutoka kwa mungu? Unakataa tena kwa kusema waliyokuwa wakiyafundisha ni mitizamo yao haikuwa ya mungu,ina maana Musa Yesu na Muhammad hawakuwa na ujumbe kutoka kwa mungu.

Mkuu kwa contradictions hizi bado tu naonekana mie ndiyo sio muelewa?
 
Wale walishakuwa addicted na dini.
Hawaoni wala kusikia lolote pindi dini inapozungumzwa.
Dini ni kama opium vile.

Such kind of people might have been through hell n the church could have been their only support and so they decide to stand firm even if under manipulation
 
habari ya hapa,

Ni lini mtu mweusi alipata kiongozi anayeitwa faraoh?
Farao kilikuwa ni cheo cha watawala wa Afrika na Afrika imepata kutawaliwa na watawala wengi (Mafarao)
wewe wamtaka Farao gani? maana Mafarao wote walikuwa ni watu weusi
 
Mawazo ya kutenda Mema hutokana na Mungu, kupitia Ubongo wa Binadamu, kwa maana hiyo mtenda mema yeyote hutokana na Mungu Si Nyerere, Yesu, Muhamed, Musa nk, wako wengi tu
 
 
Mawazo ya kutenda Mema hutokana na Mungu, kupitia Ubongo wa Binadamu, kwa maana hiyo mtenda mema yeyote hutokana na Mungu Si Nyerere, Yesu, Muhamed, Musa nk, wako wengi tu
Musa Yesu na Muhammad ujumbe wao kutoka kwa mungu ulikuwa ni upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…