Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Ni Kama umefungiwa kwenye box la dini hivi, je huwezi kuwazq zaidi Kwa manufaa ya watanzania wote? Mimi Nina dini yangu ninayoiamini, lakini ninawaza Kwa ajili ya JMT. Na sipendi mtu apofanya Jambo Kwa maslahi ya watu wa dini yake tu. Ukiangalia Sana wenye dini sisi ndio tunaoliharibu taifa. Kuna wakati naona ni heri wote tungekuwa hatuna dini labda umoja wa kitaifa ungekuwa imara zaidi. Dini za kigeni wazungu, waarabu, wabudha na nyinginezo zinatugawa na kuharibu umoja wa taifa. KAMA ningekuwa na mamlaka ningeanzisha dini ya WATANZANIA KAMA ilivyo Kwa lugha ya Kiswahili. Uwe na amani ndugu nilitaka kukupa chalenji tu. Ubarikiwe Sana. Mimi na wewe ni marafiki Wala si vinginevyo
Dini ndio inayoweza kumfanya mtu akawa mwanadamu, mtu hawi mwanadamu kwa sheria za kidunia au kwa mtutu wa bunduki, never ever. Bila dini mtu ni zaidi ya mnyama kwani akili yake inampa superiority ya kufanya chchote kama akili hiyo hiyo haitawekewa mipaka, je ni mipaka gani hiyo??, jibu, ndio maana Mungu akatuma manabii na kuwapa dini tujifunze kwa hao manabii ili tuwe na mipaka ya utu wetu na hivyo tuwe binadamu, vinginevyo mtu ni mnyama mbaya na hatari kuliko wanyama wote, Mungu aliyetuumba ndiye anajua jinsi ya kutuwekea mipaka na mipaka ya aina gani, wewe, mimi au yule hatuwezi kazi hii ya kujiwekea mipaka.