Mazishi ya Kikristo yanavyokuwa.
Wakristo wote tunafahamu kuwa muongozo wetu ni Biblia,Hivyo kila tunalolifanya linatakiwa kuongozwa na Biblia neno la Mungu,Imani yetu imejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii naye Kristo ni jiwe kuu la Pembeni (Efeso 2;20). Hivyo tunajifunza kutoka kwao Maandiko hayatufundishi popote kuwa Walipokufa mitume walikamuliwa kama wafanyavyo waislamu mfano Ibrahimu alipokufa hatusomi kuwa alikamuliwa(Mwanzo 25;7),Isaka na yakobo pia walikufa na kuzikwa bila kukamuliwa (Mwanzo 49;32,50;1-6). Ni muhimu waislamu kutuambia kuwa maswala ya kukamuana wanajifunza kwa nani? Maana quran imeagiza wajifunze kutoka kwa Wakristo na wayahudi kama wana shaka katika jambo lolote {Surat Yunusi (Yona) 10;94)}
Kwa nini Wakristo tunazika na Sanduku?
Swala la kuzika na sanduku limekuwa likiwakera sana na kuwachanganya waislamu wamekuwa wakihoji kuwa wakristo wamejifunza wapi Tabia ya kuzika na sanduku?wakati mwingine wanafikiri tunaigiza utamaduni wa kizungu,kwa kawaida Wakristo hatufanyi mambo kinyume na maandiko yanavyo tufundisha soma (Mwanzo 50;24).
“..Yusufu akawaambia nduguze,Mimi nitakufa,Mungu atawajia ninyi bila shaka atawapandisha kutoka nchi hii mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu;na Isaka na Yakobo,Yusufu akawaapisha wana wa Israel akasema bila shaka Mungu atawajia ninyi nanyi mtapandisha huko mifupa yangu.Basi Yusufu akafa,mwenye miaka mia na kumi,WAKAMPAKA DAWA WAKAMTIA KATIKA SANDUKU HUKO MISRI.”