Lovelovie
JF-Expert Member
- Oct 2, 2021
- 12,582
- 26,053
View attachment 2427340
Mavazi ya kusitiri hayana Dini, Iwe na ukristo ama Uislamu yamewekewa msisitizo lakini inaonekana wazi kabisa wakristo wanapuuza maandiko kwa kuendelea kuyapa thamani mavazi yasiyositiri.
View attachment 2427341
Mimi binafsi ni mkristo nashukuru navyozaliwa haya mambo ya utandawazi wa mavazi yalikuwa bado hayajaathiri wanawake wa kikristo, tangu nizaliwe sijawai kuona mama Yangu katoka nje kavaa suruali (vazi la mwanaume) inayomchresha mapaja, Makalio na hips .... SIJAWAI !!! Ni jambo la kujivunia kwakweli, Hebu vuta picha Mama yako anatok nje vazi limemchora mpododo, steki, mapaja, hips, n.k.
View attachment 2427343
Shida inakuja siku hizi, Suruali, vimini na magauni marefu anayobana yenye mpasuko yamekuwa kama vazi rasmi,, ni kawaida sana hata mtoto kujua ukubwa wa makalio ya mama yake, hips zake, mapaja, n.k. Hii ni aibu sana.
View attachment 2427344View attachment 2427345
Biblia ilishakataza kuvaa mavazi ya wanaume hizi suruali, kila mtu kapewa free will a kutaka kufanya atakacho lakini ni muhimu kuangalia impact, Binti kavaa jeans imembana imemchora kilakitu, Haya ni majaribu ya wazi wazi kwa wanaume walioumbwa kuyatamani maungo hayo, Na ndio maana hata mwanaume akigeuka ni vile alivyoumbwa luyatamani mango hayo.
View attachment 2427346
Biblia ilishaweka wazi wanawake waae mavazi yanayositiri lakini kinachoendelea ni kinyume, sketi zinazovaliwa zinaishia magotini kuyafanya mapaja yaonekane mwanamke akikaa. Kuna sketi hizi ndefu kama za harusini lakini zimembana sana mwanamke hazina tena heshima maana zinaachia hips wazi wazi bila kusitiri.
View attachment 2427347
Mavazi hayo yanavaliwa na wote sio waislamu sio wakristu.
Ushawai kutana na mtu kavaa dera na ushungi alafu huko ndani ako chukuchuku yalaaaa yalaaaa.
"Hyo picha namba mbili ya slimthickmary ifute mzazi mwenzie akiiona atambutua tu bure"