Wakristo mjitafakari kwenye suala la mahari, mnawakosea sana binti zenu. Kilichotokea hivi karibuni kwa jamaa yangu kina funzo

Kuna arusi za kiislam zishafanyika kubwa sana za wakiristo zinasubiri.

Arusi hufanyika hata siku saba
Singo, bomu, lunch, akdi, reception, chai, na siku ya kupeleka begi pia huwa kuna ngoma
Na mahari yao ndio usiseme, kuna mabint wametolewa mahari mpk 10M na utaskia kazawadiwa na seti ya dhahabu.
Inategemea family na family tu
 
Mimi bado naziheshimu ndoa za waislam very cheap and nzuri na mwanamke kama amekulia kwenye dini hutakuja kujuta sema misimamo yao ya tofauti za didi otherwise i still opting to muslam ladies
Hata kuachana ni cheap hivyo hivyo, in a blink of an eye.
 
usisingizie dini bali laumu umaskini wako,mwanamme kushindwa kulipa million tatu huyo ni hoehae
 
tena mahari ya million tatu mwanaume anaghairi mpaka kuoa?heshima iko wapi?miaka 37 huwezi kulipa mahari ya 3M?
 
Kwamba jamaa yako kabadilishwa dini na mbususu tena ya form four aiseee na unakuja kujisifia hapa. Si angebadili tu tangu mwanzo kuliko kutaka kujibebesha mganda asiyemuweza.
aibu nimeona mimi yaani ameiabisha nchi bora usingeleta ujinga wako hapa
 
Ukishataja mahali huzungumzii tena ukristo , umevuka hizo ni Mila na desturi za makabila
Ukristo na mahali wap na wap?
 
Moja ya vitu vinavyosingiziwa ukristo ni swala la mahari. Ukristo haupo specifically kuhusu insu ya mahari..ukristo ni mtu kumuacha Baba yake na Mama yake, swala mahari kiasi hiki ama kile ni tamaa za wakristo si ukristo.
Tatizo la Ukristo si haya uliyo yasema shida Ukristo hauna mafundisho au muongozo wa kiimani juu ya suala la Ndoa. Hapa ndipo tatizo lililopo.

Kusema ndoa ni kumuacha baba yake na mama yake, hata ambao hawapo kwenye ndoa wanavutana tu. Hii haitoshi na hiyo ni sehemu ndogo sana katika ndoa.

Hii ni kutokana na kutokuwa na muongozi juu ya jambo hilo kutoka kwa Yesu.
 
Na kuachana ni cheap sana kwenye uislamu

Ukristo expensive na kuachana hakupo
Hapa ndipo utaona shida ya ukristo kwani ni dini ambayo haiendani na umbile la mwanadamu. Kwanini msiachane kama mmeshindwana ? Hii sheria aliwafundisha Yesu ? Kwa ninavyo wajua mitume hawawezi kufundisha ujinga kama huu.

Asikwambie mtu ndoa ambazo zimefunwa kwa mahari ndogo ndiyo zina baraka.
 
Vizuri, ulichokiandika ndicho mleta mada alipaswa kukijua kabla hajaleta uzi wake.
Mapokeo yamewathiri wakristo especially insu ya mahari.
Hapa msitake kuwadanganya watu. Hayo mapokeo katika jamii lazima yarasimishwe na dini yaani hapo ilitakiwa Yesu awe amefundisha suala la Mahari na ndoa kwa ujumla.

Ndoa ni jambo la kiibada tena kongwe, kwahiyo ni muhali kwenye dini kutokuwa na mafundisho rasmi juu ya ibada hii adhwimu.
 
Ulitaka afundishe nini ambacho unahisi hakijafundishwa?. unakusudia kusema Yesu alipaswa afundishe kiwango cha mahari ama nini hasa?.
Unajua mjadala ni mahari na si Ndoa?.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣fala sana we jamaa
 
Ukisikia binti kutoka Kigoma, Kagera na hao wenye asili ya Uganda jiandae kujipiga kifua kwenye mahari.
 
Unataka kusema nini hasa?
 

Umekusudia kuutukana ukristo? Ona hoja zako mfu hapa ambazo zinaonyesha jinsi gani unaleta hadithi za kutunga zisizo na mashiko:

1. Rafiki yako single father watoto watatu. Mama wa watoto hao watatu yuko wapi?

2. Single mother mtoto mmoja, baba wa mtoto yuko wapi?

3. Walikuwa marafiki chuoni (wapenzi)? Wapi Ukristo unaruhusu uchafu huo?


4. Hilo suala la mahari ya waganda lina uhusiano gani na Ukristo? Ni wapi kuna maelekezo ya kudai kiwango fulani cha mahari? Hoja za kipuuzi kweli kweli.

5. Huyo muoaji alitakiwa kusikitikia bajeti yake, kwamba amevamia mila za watu bila mwongozo sahihi. Muache kukurupuka, mambo haya hufanywa kwa utaratibu.

Akasema alitegemea wangesema milioni moja halafu yeye angetoa laki tano au saba huku akitoa ahadi ya kumalizia mahari iliyo baki(waganda hakunaga kubakiza mahari).

6. Akasema alitegemea watasema.... Kwani mlikwenda kupeleka posa mpangiwe mahari au mlikwenda kuwaeleza kile mlichokuwa tayari kulipa? After all mahari ya MWANAMKE tena mwenye mtoto haiwezi kuwa hicho ulichosema, ni uongo dhahiri. Mengine tuwaachie waganda na mila zao, sasa Ukristo unaingiaje hapo ewe usiye ufahamu?


7. Nilitegemea utasema "WAKATI KATIKA UISLAMU KUTOMALIZA MAHARI NI HESHIMA KUBWA.... " Kumbe umejichanganya mwenyewe, unadai Tanzania ni heshima kutomaliza mahari, kwani Tanzania ni ya Waislamu na Uganda ni ya Wakristo? Una matatizo ya logic kwenye hoja zako.


8. Sasa huyo mtu wenu alikuwa muoaji kweli au ni mhuni tu? Pia ninyi wasindikizaji feki ni genge la malaya tu, eti mngeshangaa kama hana alternative!? You're fake!!

9. Ok, kwa akili yako ukaona ni wakati sahihi kutuingizia character wako muislamu kwenye utunzi wako. Eti kwao wanataka ndoa ya Kiislamu, hapa unamaanisha ndoa za Kiislamu hazina mahari?

Kisha akamuuliza. Upo tayari kufunga ndoa ya kiislamu? Jamaa akajibu yupo tayari. Mshenga akajibu tunasubiri nini? Mshenga akaenda kutoa taarifa ukweni kwamba tunarudi Dar kujipanga na tutarejea tutakapo kuwa tayari.

10. Mwanamume aliye tayari kwa ndoa, amekwisha kujichagulia mchumba hawezi kamwe kubadili gia angani sekunde moja baadaye kutaka mwanamke mwingine. Hii ni dhahiri huyu hakuwa muoaji, ama utunzi umepwaya.

Jamaa karudi Dar ndani ya hizo wiki mbili kavuta jiko na harusi ikafanyika kwa gharama ya kawaida sana, na mtoto mwenyewe mbichi kabisa ndiyo kwanza kamaliza form four(anaweza kuwa bado hajawa dis flowered).

11. Form four, anaweza kuwa bikira. Kamaliza shule gani huyo? Huyu jamaa yako alidai anaye mchumba mwingine, alimposa lini? Kwa hiyo alikuwa na wanawake wawili akisubiri mwenye unafuu wa mahari? Baada ya kufeli kwa mwanamke wa kwanza akahamia kwa wa pili, huyu jamaa hakuwa na mpango wa kuoa licha ya sifa feki ulizommwagia. Genge la wahuni tu.

Baada ya kuoa jamaa kamjulisha mchumba wake wa uganda kwamba hayupo tena interested na ndoa kwa sababu hizo gharama haziwezi na kwamba ameamua kuoa sehemu nyingine. Mwanamke wa kiganda kachanganyikiwa sasa hivi anawalaumu wazazi wake tu.

12. Mwanamke wa Kiganda ama wa kikristo aliyechanganyikiwa? Umeshutumu ukristo kwa mila za Kiganda?


12. Sasa hapo kwenye hitimisho la upuuzi huu unajazia "ukristo" wakati kwenye andiko lako umebainisha utofauti wa ndoa za Kiganda na za Kitanzania, hivi kichwa chako kinawaza sawa sawa? Hakuna hata sehemu moja umeonyesha uhusika wa viongozi wa kikristo kwenye mchakato wa mahari. Sasa ukristo ujifunze nini kwenye Uislamu?

13. Tofauti ya ndoa za kikristo na nyinginezo ni mchana na usiku. Kwa mfano ndoa nyinginezo (ikiwemo uislamu) ni mikataba ambayo yaweza kuvunjwa wakati wowote lakini ndoa za kikristo ni AGANO LA MAISHA. Hili huvunjika pale tu upande mmoja unapokufa.

14. Mahari ni utamaduni wa kibiblia ambao huashiria nia njema ya muoaji. Pia ni shukrani kwa mzazi kwa malezi bora kwa binti yake. Maandiko hayaweki kiwango cha mahari stahiki, hilo limeachwa kwa jamii husika. Kuutuhumu ukristo kisa mlishindwa kulipa mahari ya Kiganda ni upotofu wa fikra. Yakobo alitumika miaka 14 ili kumpata mkewe aliyempenda sana, sasa huyo jamaa yako safari moja tu ya Uganda imeanzisha mada 'JF. Badala ya kurudi na kupanga hoja ili mwishowe ampate yule ampendaye eti akaona aoe muislamu! Kizazi cha hovyo kweli kweli.


15. Ukusudia wanawake wengi wasio na ndoa duniani ni Wakristo? Kwa utafiti upi? Huu nao ni upuuzi mkubwa. Unataka kumaanisha hata wanaume wa kikristo hupendelea kuoa wanawake wa Kiislamu? Hello, jaribu tena. Wewe si mtunzi mzuri.

Ni hivi muoaji anapo kuja kwenye familia yako, usifikiri hajaona mwanamke mwingine au hana option nyingine. Most of the time muoaji anapofikia hatua ya kuja kujitambulisha nyumbani kwenu tayari anakuwa na option zingine kama mbili, tatu au hata nne.

Kama hujaoa nakushauri usithubutu kwani hujajua ndoa ni nini. Huo ushauri wako ni wa kijinga kabisa, kama sababu za binti kukubali kuolewa ndio hizi, basi hakuna haja ya kuolewa!! Mtu anayekuja akiwa na 'option' mbili au tatu sio mwoaji, ni malaya kama malaya wengine tu. Tofauti ni kwamba huyu ameamua kuhalalisha umalaya wake kwa kumweka ndani binti wa watu huku moyo wake ukitangatanga hovyo.


Mwanamume anapohangaika kumpata mke ni dalili ya upendo kwake na mara nyingi ndoa za aina hiyo hudumu. Kwa familia yenye maadili kuoa sio hisani kwamba unaisaidia familia. Wewe na huyo jamaa yako bado mna safari ndefu ya kujifunza maana na maisha ya ndoa. Pole sana.
 
Kwa hiyo huyo binti asingekuwa fundi nguo; ungetoa hicho kiasi?
Sina maana kuwa nimedharau fani yake ila dharau zilianza kwa walezi wake kudharau kiasi cha pesa nilicho nacho, utamaduni wengi wa wakristo hupanga mahari kubwa kutokana na kiwango cha elimu walicho msomesha binti yao,
Hufanya hivyo wakidhani wanaenda kukufaidisha.
 
Wewe siyo mkristo labda huwa unakwenda kuangalia mademu tu church.

Kabisa linahusika vipi na mahari? Mambo ya kifamilia kabisa linaingiaje?
Niambie unaweza kutoa posa bila kiongozi wa kanisa kuhusishwa harafu wachungaji au viongozi wa kanisa wakakuelewa, acha masihara ndugu,
Kama ni hivo basi mvulana na msichana wangekuwa wanaelewana tu harafu wanaenda kwa mchungaji awafungishe ndoa basi
 
Ulitaka afundishe nini ambacho unahisi hakijafundishwa?. unakusudia kusema Yesu alipaswa afundishe kiwango cha mahari ama nini hasa?.
Unajua mjadala ni mahari na si Ndoa?.
Atoe muongozo wa Mahari na aseme lipi ni bora katika mahari, kutaja kiwango si jambo la msingi, ila kanuni na muongozo juu ya mahari na ndoa ndiyo jambo la msingi zaidi. Kukosekana kwa mafundisho ya Ndoa kutoka kwa Yesu ni ishara ya kuwa Ukristo haujatoka kwa Yesu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…