Wakristo mjitafakari kwenye suala la mahari, mnawakosea sana binti zenu. Kilichotokea hivi karibuni kwa jamaa yangu kina funzo

Maongezi yako yote mie Nina jicho moja kuwa una nia ya ku impart fear kwa watu hao uliowaongelea.

Yaani fear ndio inayo tufanya tuishi maisha yetu na Wala sio lingine huwa tunachagua the safest way and not unfamiliar way to pass through.


So don't impart fear mkuu
 
Kwanza karne hii ukiona mtu "amepandwa na kichaa " cha kutaka kuoa unapaswa kumpa mke haraka kabla kichaa hakija toweka, ili kichaa kiondoke tayari akiwa na mke ndani ndiyo akumbuke 'kumbe mimi fala hivi'.
Nakaziaa hapa mkuu naona km palikua pamelegea hivi 🤫
 
Ninapokuja kwenye familia yako usinichukulie kwanza kama mtu ambae ninataka kumuoa binti yako, nichukulie kama mtu ambae nimekuja kutazama kama familia yako ina complications au la!
Nakazia mkuu 😊
 
Mkuu mfano wewe umeenda kuoa wazazi wa Binti wakataja mahari utafanya nini?
Utaanza kuwapiga darasa au ili wasikutoze sababu ni iumdunisha mwanamke?
Issue ya mahari ipo kitamaduni zaidi sidhani kama inahusiana na kuuzwa au kudunishwa kwa mwanamke.
Mimi siendi kuoa kwa wajima.

Mahari inaondoa utu wa mwanamke na kumfanya awe bidhaa inayonunuliwa kwa bei fulani.
 
Mimi siendi kuoa kwa wajima.
Wajima tena mkuu?
Nilidhani utajibu hata kwa imagination kwamba umefika kwa wakwe wanataka mpunga ungefanyeje? Jibu usaidie hata watakaokutwa na kadhia za hao wajima.
 
Ni mtazamo tu

Hamuoni kama humu watu mna double standards. Kwa mfano; kuna watu mnalalamikia dini ya Kikristo kuhusu mambo ya mahari, au eti ukristo una mambo mengi...ok sawa. Lakini ni ukristo (neno la Mungu) unaosema mwanamke amtii mumewe...mwanamke asipotii kutwa mnafoka hakuna mfano kwamba haheshimu maandiko. Hamuoni mnakuwa mna double standard??

Afu ukute hata kupenda mlikoagizwa hampendi..tena ni biblia hiyohiyo ilioagiza wanaume kumpa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu ili kuomba kusizuiliwe haya haya hamyatimizi lakini mnashadadiaga utii utii utii na mengine hamyashiki. Kama vipi tushike yote...ni Kristo aliekataza uzinzi kwaiyo michepuko ni kuzini tu vilevile. Wewe unazini afu mke asipomutii au kukuheshimu unasimamia maandiko kiaje yani??
 
Wajima tena mkuu?
Nilidhani utajibu hata kwa imagination kwamba umefika kwa wakwe wanataka mpunga ungefanyeje? Jibu usaidie hata watakaokutwa na kadhia za hao wajima.
Mtu anayeshindwa kulipa mahari, au anayelalamika kupangiwa mahari kubwa baada ya kufika kwa wazazi ni mjinga.

Kwa sababu, hizi habari zote alitakiwa kuweza kuzipata kabla ya kwenda huko, kwa upelelezi wake.

Na mimi nakwambia, kabla ya kwenda huko nitajua kama wataweza kuelewa msimamo wangu wa kupinga mahari ama vipi.

Kama wanaendekeza tamaduni za kijima zinazomdhalilisha mwanamke kama mahari, hata hiyo ndoa haiwezi kufana na kudumu.

Kwa sababu ndoa itaunganisha familia, na mimi sitaki kuendeleza ujima kwenye familia yangu.

Ndiyo maana nikakwambia siwezi kuoa kijima.

Lakini watu tupo tofauti sana, inawezekana kabisa usinielewe.

Nikawa kama ngamia ninayemuandikia samaki habari za jangwa lisilo na maji, samaki akasoma akawa haelewi inawezekana vipi kukawa na sehemu haina maji kabisa.
 
😂😂😂Ilo ndo uliloliona pekee Uzi wote huu 😂
 
Hivi wakristo mahali wanapanga wazazi au anaeolewa ndo anataja mahari??
 
😂😂😂Ilo ndo uliloliona pekee Uzi wote huu 😂
Wee kiwa nanbackup plan ndugu yangu, hawa wanaume ni mashetani kama mlivyo mashetani nyie wanawake. Unabwagwa siku yoyote🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuna wengine mtadai tamaduni ok fine. Tamaduni za kiafrica labda zinaruhusu wanawake wengi. Lakini tamaduni zinataka wanawake watolewe mahari hakuna kuolewa bure. Kama unaenda na tamaduni all the way fanya kama zinavyodai. Kama una a lot of wives wahudumie sawa.

Huku ukitoa gari na huku toa gari. Huku wakila kuku na huku wale kuku. Mnasema tamaduni na hata wengne hamzijui. Tamaduni na mila za Africa zinakutaka ukalime wake watulie ndani wapendeze si wanakulelea watoto bwana.

Tamaduni hazitaki mtoto wa kike asome we kwanini unawasomesha?? Why waste your money. Ukishikilia jambo lielewe ili ulishike kwelikweli.

Ni mtazamo tu
 
Na kuachana ni cheap sana kwenye uislamu

Ukristo expensive na kuachana hakupo
Wanaachana sana tu na sikuhiz wanaoa km kawaida na nishahudia watu wamefunga ndoa kanisani zaidi ya maramoja na Bado wenzawao wapo hai
 
Zee lote hilo linashindwa mil.3? 😬😬
 
Kirahisi hakidumu
Kutokudumu ni kuchagua kwako asiekufaa pia binadamu hatuwez kuwa sawa never watu mmekutana ukubwani kilamtu kalelewa kwao kumatch sio rahis Inahitaji uvumilivu mkishindwa kuvumiliana achaneni Kwa amani
Talaka ipo na japo ni Sheria ila haifurahishi ila Tulivoumbwa hatufanani na hatuendani 💯
 
Wee kiwa nanbackup plan ndugu yangu, hawa wanaume ni mashetani kama mlivyo mashetani nyie wanawake. Unabwagwa siku yoyote🤣🤣🤣🤣🤣
Always unachaoamin maranying ndo kinatokea ukiamini utapata mwanaume 😂 shetani unapewa tu shetani lako kama mm nikipewa wew lazima nipate kichaa🤣🤣🤣
 
Sawa mkuu japo sijui kwa nini umeweka shaka kwamba sitakuelewa.
Hapo kwenye upelelezi sawa ila pia kama umeshafanya upelelezi ukajua wazazi lazima watataka pesa na unamhitaji Binti nini utafanya?
Mimi sichukulii mahari Kama mila mbaya miongoni mwa Mila zetu na sijui ni kwa nini tunainasibisha na kudhalilishwa kwa wanawake.
Kwani hakuna siku utajisikia kuwapelekea wakwe zako zawadi ? Kwa nini tusiichukulie kama zawadi japo baadhi ya wakwe nao wanataka kama wanakomoa.
 
Anayeolewa ni Nani?
Dhana nzima ya kuolewa ni ya tamaduni fulani.

Utaliona hili vizuri katika lugha.

Katika Kiswahili kuna anayeoa na kuolewa.

Katika Kiingereza, hakuna anayeoa wala kuolewa. Watu wanaoana. They get married.

Sasa wewe umejifunga katika utamaduni, utamaduni uliopitwa na wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…