Wakristo mjitafakari kwenye suala la mahari, mnawakosea sana binti zenu. Kilichotokea hivi karibuni kwa jamaa yangu kina funzo

Wakristo mjitafakari kwenye suala la mahari, mnawakosea sana binti zenu. Kilichotokea hivi karibuni kwa jamaa yangu kina funzo

Dhana nzima ya kuolewa ni ya tamaduni fulani.

Utaliona hili vizuri katika lugha.

Katika Kiswahili kuna anayeoa na kuolewa.

Katika Kiingereza, hakuna anayeoa wala kuolewa. Watu wanaoana. They get married.

Sasa wewe umejifunga katika utamaduni, utamaduni uliopitwa na wakati.
Nimejifunza katika Dini....

Wazungu si wapuuzi Tu....tangu lini mnaoana.....lazima kuna anaye oa na kuolewa
 
Nimejifunza katika Dini....

Wazungu si wapuuzi Tu....tangu lini mnaoana.....lazima kuna anaye oa na kuolewa
Kwani tukisema wanaona au anaoa inabadili nini kwamba hawa watu wanamahusiano ya ndoa?...Mimi naona mgongano wa tamaduni tu lakini mantiki inabaki pale pale
 
Sawa mkuu japo sijui kwa nini umeweka shaka kwamba sitakuelewa.
Hapo kwenye upelelezi sawa ila pia kama umeshafanya upelelezi ukajua wazazi lazima watataka pesa na unamhitaji Binti nini utafanya?
Mimi sichukulii mahari Kama mila mbaya miongoni mwa Mila zetu na sijui ni kwa nini tunainasibisha na kudhalilishwa kwa wanawake.
Kwani hakuna siku utajisikia kuwapelekea wakwe zako zawadi ? Kwa nini tusiichukulie kama zawadi japo baadhi ya wakwe nao wanataka kama wanakomoa.
Ulivyomalizia ndicho nikichotabiri kitatokea, na nakushangaa kwa nini unanishangaa niliposema hutanielewa, wakati umemalizia kwa kunionesha hujanielewa.

Jamii zilizoweza kuweka equity kati ya wanawake na wanaume zishaondoa mahari. Haya si mambo ya nadharia, ni mambo tunayoona dunia hii.

Mahari haina tofauti na kununua ng'ombe.

Ukisema zawadi, mbona mwanamme hatolewi zawadi ya mahari? Na kwa nini zawadi isitolewe bila kulazimishwa baada ya ndoa?

Mbona watu wanatoa zawadi kila mara kwa wazazi, bila kubagua mzazi wa mwanamke au wa mwanamme? Mbona wanatoa hata baada ya kutoa mahari?

Najua ni utamaduni na mmezoea na ni vigumu kueleweshana mara moja.

Lakini, ukweli ni kuwa mahari inamfanya mwanamke kuwa bidhaa ya kununuliwa.

Na huwezi kumfanya mwanamme asijione kamnunua mwanamke kama utabaki na mahari.
 
Kwani tukisema wanaona au anaoa inabadili nini kwamba hawa watu wanamahusiano ya ndoa?...Mimi naona mgongano wa tamaduni tu lakini mantiki inabaki pale pale
Tofauti IPO Sana labda kama hutaki kuiona....Nani anapropose kuoa? Nani anatoa mahari? Nani yupo responsible kt ndoa?
 
Ulivyomalizia ndicho nikichotabiri kitatokea, na nakushangaa kwa nini unanishangaa niliposema hutanielewa, wakati umemalizia kwa kunionesha hujanielewa.

Jamii zilizoweza kuweka equity kati ya wanawake na wanaume zishaondoa mahari. Haya si mambo ya nadharia, ni mambo tunayoona dunia hii.

Mahari haina tofauti na kununua ng'ombe.

Ukisema zawadi, mbona mwanamme hatolewi zawadi ya mahari? Na kwa nini zawadi isitolewe bila kulazimishwa baada ya ndoa?

Mbona watu wanatoa zawadi kila mara kwa wazazi, bila kubagua mzazi wa mwanamke au wa mwanamme? Mbona wanatoa hata baada ya kutoa mahari?

Najua ni utamaduni na mmezoea na ni vigumu kueleweshana mara moja.

Lakini, ukweli ni kuwa mahari inamfanya mwanamke kuwa bidhaa ya kununuliwa.

Na huwezi kumfanya mwanamme asijione kamnunua mwanamke kama utabaki na mahari.
Hujasema kwa nini unahisi kutoa mahari ni sawa na kununua ng'ombe.
Hii dhana nilidhani wewe muafrika ungeiona kwa jicho tofauti kabisa na mzungu aliyehadidhiwa sababu unajua fika maana ya mahari si kununua mwanamke.
Ni kwa nini unahisi mpaka mwanaume naye atolewe zawadi ndio itakuwa sahihi? Kuna mashindano gani hapa kama miaka n miaka mahari zinatolewa na hicho unachosema sicho kinachomaanishwa?
 
Tofauti IPO Sana labda kama hutaki kuiona....Nani anapropose kuoa? Nani anatoa mahari? Nani yupo responsible kt ndoa?
Ukisema nani napropose kuoa na yule atasema nani anapropose kuoana.
Kwangu Mimi hizo no lugha tu hakuna zaidi.
Mahari ndio issue iliyoko mezani hapa.
Nani yupo responsible kwenye nini? Na nani hayupo responsible kwenye duania ya leo.
 
Kama binti ni bikra na pesa ipo mimi naitoa kiroho safi. Ila kama ni Japanese used sitoi io hela
 
Kwanza karne hii ukiona mtu "amepandwa na kichaa " cha kutaka kuoa unapaswa kumpa mke haraka kabla kichaa hakija toweka, ili kichaa kiondoke tayari akiwa na mke ndani ndiyo akumbuke 'kumbe mimi fala hivi
daah huu msemo sie tusiokuwa na mpango wa kuoa unatupa moyo sana na usingle wetu
 
Yani binti ndo kamaliza form 4 mwamba mwenye watt watatu anaenda kumchakaza. Aaaaaaaghhhh
 
Rafiki yangu(37) ni single father with 3 kids, ana mchumba wake mganda ambaye naye ni single mother(37 yrs) with one kid. Alikuwa rafiki yake wakati wakisoma chuo, wakaja kukutana tena miaka kadhaa baada ya ku graduate, jamaa anaishi Dar, mrembo anaishi Kampala wakaanzisha uhusiano.

Muda wa kwenda kutoa mahari ulikuwa mwezi uliopita. Nilikuwa mmoja katika ujumbe uliyoongozana na rafiki yangu na matchmaker(mshenga) wake. Wakati wa kunegotiate mahari wazazi wakaanza na 15 million Ugandan ambayo ni kama milioni 9 ya Tanzania(walitaja idadi ya ng'ombe then ikawa converted to cash).

Tukakomaa wakashusha mpaka milioni kumi ya Uganda. Tutakomaa tana wakashusha mpaka milioni tano ya Uganda. Mwisho kabisa wakakomea shilingi milioni nne na point kadhaa ya Uganda ambayo ni sawa na milioni tatu ya Tanzania.

Hapo wakasema haipungui hata mia. Tukaomba tupewe muda tukatafakari kisha tutatoa taarifa ni lini tutarejea tena ukweni kukamilisha hiyo mahari. Kumbuka hapo tumefikia hotelini. Basi tulipoenda kujadiliana tukamuuliza muoaji kama bajeti yake ina mruhusu kulipa milioni tatu cash akasema no way out hawezi kulipa mahari yote hiyo.

Akasema alitegemea wangesema milioni moja halafu yeye angetoa laki tano au saba huku akitoa ahadi ya kumalizia mahari iliyo baki(waganda hakunaga kubakiza mahari). Wakati hapa Tz kutokumalizia mahari ni heshima kubwa sana kwa wakwe, kwasababu kwanza, inaonyesha kwamba bibi harusi sio bidhaa unayo weza kuinunua dukani na kwamba wazazi wa bibi harusi wamekutunuku binti yao ukaanzishe nae familia. Lakini pili Inaonyesha kwamba wewe muoaji unampenda sana mkeo kiasi kwamba haupo tayari kusubiri mpaka upate mahari kamili.

Mshenga akamuuliza bwana harusi. Hauna alternative mahali kwingine, yaani hauna mchumba mwingine?
Jamaa akajibu nina mchumba mwingine yupo Tanzania ila yeye ni muislamu na kwao wanataka tufunge ndoa ya kiislamu(mshenga akajibu nilitaka kushangaa unakosaje alternative?!).

Kisha akamuuliza. Upo tayari kufunga ndoa ya kiislamu? Jamaa akajibu yupo tayari. Mshenga akajibu tunasubiri nini? Mshenga akaenda kutoa taarifa ukweni kwamba tunarudi Dar kujipanga na tutarejea tutakapo kuwa tayari.

Jamaa karudi Dar ndani ya hizo wiki mbili kavuta jiko na harusi ikafanyika kwa gharama ya kawaida sana, na mtoto mwenyewe mbichi kabisa ndiyo kwanza kamaliza form four(anaweza kuwa bado hajawa dis flowered).

Baada ya kuoa jamaa kamjulisha mchumba wake wa uganda kwamba hayupo tena interested na ndoa kwa sababu hizo gharama haziwezi na kwamba ameamua kuoa sehemu nyingine. Mwanamke wa kiganda kachanganyikiwa sasa hivi anawalaumu wazazi wake tu.

Wakristo hizo zama za wanaume kutoa mahari za mamilioni hazipo tena. Jifunzeni kwa waislamu, mnawakosesha binti zenu ndoa kwa sababu ambazo hazina msingi. Kwanza karne hii ukiona mtu "amepandwa na kichaa " cha kutaka kuoa unapaswa kumpa mke haraka kabla kichaa hakija toweka, ili kichaa kiondoke tayari akiwa na mke ndani ndiyo akumbuke 'kumbe mimi fala hivi'.

NB: Kwa sababu ya complications zake, familia nyingi za kikristo huwa zina experience ndoa chache sana ikilinganishwa na familia za kiislamu. Dini ya kiislamu imerahisisha sana suala la ndoa. Matokeo yake familia nyingi za kikristo huwa hazifahamu saikolojia siasa za waoaji.

Ni hivi muoaji anapo kuja kwenye familia yako, usifikiri hajaona mwanamke mwingine au hana option nyingine. Most of the time muoaji anapofikia hatua ya kuja kujitambulisha nyumbani kwenu tayari anakuwa na option zingine kama mbili, tatu au hata nne.

Nikija kwenye familia yako kuchumbia, halafu ukaniletea complications ngumu, mimi nitakacho kifanya nita kuachia binti yako nitaenda kwenye familia ambayo haitaniwekea complications ngumu.

Ninapokuja kwenye familia yako usinichukulie kwanza kama mtu ambae ninataka kumuoa binti yako, nichukulie kama mtu ambae nimekuja kutazama kama familia yako ina complications au la!
samahani kusema maoni yangu, huyo rafiki yako hakuwa muoaji kabisa. Kwamba anasafiri kwenda Uganda akashindwa hata kutafiti Mila zao.!! Bora huyo binti hakuolewa na huyo kwa kweli. Unakwenda kuoa ukiwa na mbadala kweli!! Mbona ukristo hauko hivyoo. Ukristo kiuhalisia hauna talaka.
 
Ukisema nani napropose kuoa na yule atasema nani anapropose kuoana.
Kwangu Mimi hizo no lugha tu hakuna zaidi.
Mahari ndio issue iliyoko mezani hapa.
Nani yupo responsible kwenye nini? Na nani hayupo responsible kwenye duania ya leo.
Tuliache kama lilivyo mkuu.....kila mtu abakie na kile anachoona ni sahihi
 
Always unachaoamin maranying ndo kinatokea ukiamini utapata mwanaume 😂 shetani unapewa tu shetani lako kama mm nikipewa wew lazima nipate kichaa🤣🤣🤣
Wee unatapata raha bwana wala usijali na mtoto wetu wa kambo
 
Hujathibitisha Mungu yupo.
Nilikupa hoja zangu ukakimbia... Kwakuwa Una Uhai,ridhiki yako unapata na unaendesha Maisha unapata kiburi kuwa Mungu hayupo...Ila mungu hapa duniani awapa watu wote ridhiki Yao iwe wachawi,wasio amini mungu kama wewe,majambazi nakadhalika...

Ukifa mkuu jeuri yko itajilikana...let's wait kaka
 
Kutokudumu ni kuchagua kwako asiekufaa pia binadamu hatuwez kuwa sawa never watu mmekutana ukubwani kilamtu kalelewa kwao kumatch sio rahis Inahitaji uvumilivu mkishindwa kuvumiliana achaneni Kwa amani
Talaka ipo na japo ni Sheria ila haifurahishi ila Tulivoumbwa hatufanani na hatuendani 💯
Mie talaka siipendi
 
Back
Top Bottom