Wakristo tuisusie Azam TV, wanatutenga Krismasi

Tumechelewa Sana Ndugu Zangu
Tumeliwa Sana Ndugu Zangu
Tumelaliwa Sana Ndugu Zangu
Tumegongwa Sana Ndugu Zangu
 
Hongera
Ika jua tu azam kama hujaiangalia bas utainywa na kama hujainywa utaila Lama hujaila utaipanda na huko mbeleni wakianzisha mtandao wao wa siku basi utawasikiliza
 
Safi kwa kukitia moto hicho kisimbuzi..kitu kikikukera act fasta
 
Wewe sio Mkristo, hizo kiki za Kibinadamu na Ukristo hapa na wapi
 
Mwanaume kulalamikia vimaua ni ujinga,unakuwa ujinga plus unahamasisha kususia.
Mie ni mkristo tena sio mkristo jina ni mkristo wa kuzaliwa mara ya pili.
Ila madai yako naona unajidharirisha wew na wakristo,wkristo hatupo hivyo..
Wewe sijui mkristo daraja la ngapi sikuelewi..
Susia pia jf maana hawajaweka hvyo vimaua,susia maduka,susia hosptal susia vingi maana hakuja wekwa..hata kwako hujaweka susia mpka choo chenu.
 
Weka picha kuchoma moto king'amuzi chao kama sio wivu na roho ya "kaa" kwa mafanikio yao ⁉️ Mbadala wako ni kipi❓
 
Hongera wadini sana mi hata sijawah kinunua.
 
Dini yenu ni ya promo ndio maana mnalia....weka zile za upendo tv,agape na nyingine nyingi kwenye king'amuzi hicho hicho cha azam pale kwenye category ya religion chanel....utapata maukristo yako ya kriss mass.
 
Upo sahihi lakini tabia ya kulialia mambo madogo hivyo sio ya kwetu wakristu. Kuna mambo ya maana zaidi ya hayo..hatupo weak kihivyo.
 
Ukiristo haushurutishi, nawa mikono, kung'uta vumbi, aga, sepa, usigeuke nyuma, Songa mbele, kuwa na amani.
Mbona unageuka nyuma kuwaambia wengine?
 
Kuna baadhi ya mabasi ya mikoani safari nzima wanaweka nyimbo za injili ya kikristu na mengine nyimbo na mawaidha ya kiislamu na wao tuwazungumzie vipi.
Ifike mahala mtu achague anachotaka asichokitaka akiweke pembeni, ni uamuzi tu wa kuachana na king'amuzi cha azam ahamie kingine kitakachomfurahisha.
 
EATV JE mbona hawaweki mambo ya waislamu na star tv mbona hamlalamiki
 
Mimi sina shida na imani ya mzee Backhresa,minachotaka ni huduma bora.
Huijui ile familia vizuri kwenye mambo ya imani.
Waliotuletea izi dini wala awana muda mchafu wa kupoteza kwenye mambo ya dini,ila sisi waswahili viherehere ndo tunashupaa mishipa ya shingo.
Pole sana hii inaitwa ignorance!
Yani kisa umeikana imani yako basi unajiona umekuwa mkamilifu na hakuna lolote linalokuweza.

Walioleta hizi dini muda wanao tena mkubwa sana kuliko unavyofikiri tatizo ni hujishughulishi kujua.

Kanisa la Anglikana linapokea fedha nyingi tu kutoka kwa taasisi mbalimbali za kiingereza kwa kuwa England ndio muasisi wa hilo Kanisa na wanatoa hadi pesa kwa ajili ya vyuo vya kanisa.

AIC pia kutoka Finland.
Lutheran kutoka Ujerumani hawa hutoa pesa kwa ajili ya taasisi mbalimbali za Kanisa na vyuo vyake.

Catholic hapa ndio mwisho wa reli Kanisa linaendeshwa na Vatican kwa 100% na fedha za ujenzi wa mahekalu hutoka kwao plus mataasisi mengine makubwa makubwa ya kanisa.

Kwa upande wa uislamu ndio kabisa wanajenga waarabu kila siku miskiti huku alafu useme hawana muda.
Jaribu kumrudia Mungu wako huko kuikana imani yako iko siku utaukumbuka huu muda
 
Wacha ujinga usio na akili, nani alikuambia utizame Azam TV? Msipende kujipa ujinga kwa kujiaminisha upuuzi vichwani mwenu, nani aliyekuambia Yesu alizaliwa mwezi huu, soma upate kujuwa ukweli. Hizi dini ni usanii tu.
 
Kwaiyo bwashee mimi kukataa kuachana na king'amuzi cha Azam ndo iwe sababu ya mimi kuikana imani yangu?

Ao wanaotuma misaada uku kwetu ndo wenye dini zao,kwao awana time na dini.
Nchi za E.U ndo zinaongoza kuwapa uraia watu wanaotoka kwenye nchi za kiislam.
 
Mawazo finyu haya mkuu. Sio lazima wao kufanya hivyo, ni matakwa binafsi. Kama hupendezwi nao hama tu kimya kimya hakuna haja ya kushawishi wengine kuleta udini kwenye mambo yasiyo na msingi.
 
Hivi king'amuzi cha Azam chanel za kikristu na za kiislam zipi nyingi? Tuanzie hapo kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…