Wakristo tujirekebishe katika hizi nyimbo za maombolezo

Wakristo tujirekebishe katika hizi nyimbo za maombolezo

Umezaliwa,kukulia na kujifunza teolojia ya kikatoliki halafu hujui kuchambua maudhui ya nyimbo za kikatoliki?🤔🤔🤔🙄🙄🙄
Maudhui? Ukipiga sauti inayoashiria kelele masikioni kwa mtu unataka mtu asikie kama muziki mororo?? What are you talking about? Wote wanaokwenda msibani wanajua fasihi?? Wanaweza kujua maudhui ya nyimbo? Ndio hili nalichukia kusomea upadri kanisa katoliki unasoma kwanza Falsafa ((Philosophy) kabla ya Teolojia (Theology) na mwisho wa yote ndiyo kuja kuleta hoja za hovyo kama hiyo yako.
 
Una matatizo kwenye kufikiri.Usiuchukulie wimbo kwa namna unavyowaza.Kila neno linalowekwa huwa lina maana zaidi ya unavyoliona na kulitafsiri.Jifunze kuhusu fasihi kwa ufasaha.Kama unataka kwenda makanisa ya walokole weye nenda.Usitafute vijisababu.
Duh..!
Mkuu inaelekea wewe ni katekista.
Mpe mwongozo wa hekima 'kondoo' wa Bwana ili abaki zizini....usimtandike mateke kiasi hicho
 
Song: Hapa We Msafiri​

Composer: Fr. G. F. Kayeta​

Category: Mazishi​

Choir: -​

Hapa We Msafiri Lyrics​

  1. Hapa we msafiri simama na tazama (simama na tazama)
    Nimekufa leo, kesho - ni zamu yako
    (ona) ona vema nilivyowekwa humu,
    Na nilivyoacha mali na jamaa
  2. Nilitoka uchi tumboni mwa mamangu
    Narudia uchi, kati-ka tumbo la nchi
    (Sanda) sanda moja hilo ni vazi langu,
    Wameninyang'anya hata senti moja.
  3. Nifunike vema na hilo jembe lako . . .
    Nalitangatanga, kati-ka ulimwengu
    (Basi) basi leo kiburi kimekwisha,
    Kumbe dunia hii ni mti mkavu.
  4. Nyumba yangu leo ni shimo udongoni
    Hakuna mlango, haku-na madirisha
    (Kita) kitanda changu na blanketi langu,
    Ni udongo mzito wanielemea
  5. Kifafanuacho wafu mbele ya Mungu . . .
    Si cheo kikubwa, si da-raja si sifa
    (Mate-) matendo mema saa ya kufa kwangu,
    Yatafungua mlango wa uwingu
  6. Ole wangu mimi nilifanya ujinga . . .
    Kwa kuambatana, na wa-tu wa dunia
    (Ona) ona wote leo wameniacha,
    Hasa watu wale niliowapenda.
  7. Unapojiona jiwazie mwenyewe . . .
    Kufa siku moja, kwa wo-te ni lazima
    (Japo) japo sultani japo ni mtumwa,
    Mungu atamwita ikiwa saa yake.
  8. Nimekufa leo nilipona salama . . .
    Nalijidhania, mwenye - afya mwilini
    (na ma-) na mara moja nikaanguka chini
    Labda huamini kwamba nali`mzima.
  9. Yesu msalabani kateswa vikali mno . . .
    Kwa kutukomboa, aka-mwaga damuye
    Wahurumie wote wa toharani,
    Mwanga wa milele uwaangazie.
  10. Kwaherini wote kwaherini wapenzi . . .
    Ninakwenda kwetu sita-rudi nyuma
    (Kwa he-) Kwaheri Baba kwaheri Mama yangu,
    Mungu akipenda kwake tukutane.
 
Dini inayomfanya mwanadamu mwenye akili timamu alisogelee sanamu alibusu na alisujudie na kuliomba kitu anachokitaka alafu anatoka kimya kimya eti asipige kelele sanamu litamsikia ,hii dini ni hatari
umenena vema. Nami niko kinyume sana na hili. Japo kanisa katoliki lenyewe ( na baadhi ya sehemu za maandiko ya biblia) inaonyesha kuwa na sanamu si dhambi ( aghalabu hata haya maandishi yangu unayoyasoma ni sanamu za sauti!) lakini kweli sanamu zinaabudiwa sasa. Ni vibaya sana na kanisa linapaswa kuliangalia hili upya.
 
Sisi ni wanadamu ni dhaifu lazima tuomboleze juu ya wapendwa wetu
Unapata faida gani unapoitupilia mbali imani yako ya kikristo na kujitupa pasipo matumaini? Faida ya maombolezo ya namna hiyo ni ipi?
 
Duh..!
Mkuu inaelekea wewe ni katekista.
Mpe mwongozo wa hekima 'kondoo' wa Bwana ili abaki zizini....usimtandike mateke kiasi hicho
Ni vizuri kama yeye ni Katekista. Mimi ni mwalimu wao so hopeffuly tutaelewana ili asije kuwa katekista jina na maswali makuu ya imani akashndwa kuyajibu vema kama walivyo makatekista wengine
 
Song: Hapa We Msafiri​

Composer: Fr. G. F. Kayeta​

Category: Mazishi​

Choir: -​

Hapa We Msafiri Lyrics​

  1. Hapa we msafiri simama na tazama (simama na tazama)
    Nimekufa leo, kesho - ni zamu yako
    (ona) ona vema nilivyowekwa humu,
    Na nilivyoacha mali na jamaa
  2. Nilitoka uchi tumboni mwa mamangu
    Narudia uchi, kati-ka tumbo la nchi
    (Sanda) sanda moja hilo ni vazi langu,
    Wameninyang'anya hata senti moja.
  3. Nifunike vema na hilo jembe lako . . .
    Nalitangatanga, kati-ka ulimwengu
    (Basi) basi leo kiburi kimekwisha,
    Kumbe dunia hii ni mti mkavu.
  4. Nyumba yangu leo ni shimo udongoni
    Hakuna mlango, haku-na madirisha
    (Kita) kitanda changu na blanketi langu,
    Ni udongo mzito wanielemea
  5. Kifafanuacho wafu mbele ya Mungu . . .
    Si cheo kikubwa, si da-raja si sifa
    (Mate-) matendo mema saa ya kufa kwangu,
    Yatafungua mlango wa uwingu
  6. Ole wangu mimi nilifanya ujinga . . .
    Kwa kuambatana, na wa-tu wa dunia
    (Ona) ona wote leo wameniacha,
    Hasa watu wale niliowapenda.
  7. Unapojiona jiwazie mwenyewe . . .
    Kufa siku moja, kwa wo-te ni lazima
    (Japo) japo sultani japo ni mtumwa,
    Mungu atamwita ikiwa saa yake.
  8. Nimekufa leo nilipona salama . . .
    Nalijidhania, mwenye - afya mwilini
    (na ma-) na mara moja nikaanguka chini
    Labda huamini kwamba nali`mzima.
  9. Yesu msalabani kateswa vikali mno . . .
    Kwa kutukomboa, aka-mwaga damuye
    Wahurumie wote wa toharani,
    Mwanga wa milele uwaangazie.
  10. Kwaherini wote kwaherini wapenzi . . .
    Ninakwenda kwetu sita-rudi nyuma
    (Kwa he-) Kwaheri Baba kwaheri Mama yangu,
    Mungu akipenda kwake tukutane.
Asante kwa msaada. Sikutaka kuhangaikia takwa lake maana sidhani humu kuna mtu ambaye hajahudhuria mazishi ya mkatoliki na huo wimbo huwa haukosekani.
 
Yanakuhimiza kunyenyekea na kuwa mwema ili adhabu za dhambi uziepuke.Siyo uzito wa udongo na giza.😂😂😂😂
Unaokolewa kwa kunyenyekea?? Seriously? Ni neema au unyenyekevu unaokuoa? Wakristo jamani! what went wrong with you??
 
Msiba ni msiba huzuni lazima iwepo, wanafunzi was Yesu ambao Leo ndio mgano wa kuigwa kwetu, Yesu alikuwa anawaaga walihuzunika hata yeye akawatia moyo ya kwamba msihuzunike sitawaacha yatima. Ndio ije kuwa sisi? Ndugu zake Razaro waliomboleza wanamwabia Yesu kama ungelikuwepo kaka yetu asingekufa, angalia wale wajane walivyomlilia Dorcus mpaka Mungu akamrejeshea uhai wake, achana na msiba na hata Mungu anajua ndio maana akasema farijianeni ninyi kwa ninyi
 
Song: Hapa We Msafiri​

Composer: Fr. G. F. Kayeta​

Category: Mazishi​

Choir: -​

Hapa We Msafiri Lyrics​

  1. Hapa we msafiri simama na tazama (simama na tazama)
    Nimekufa leo, kesho - ni zamu yako
    (ona) ona vema nilivyowekwa humu,
    Na nilivyoacha mali na jamaa
  2. Nilitoka uchi tumboni mwa mamangu
    Narudia uchi, kati-ka tumbo la nchi
    (Sanda) sanda moja hilo ni vazi langu,
    Wameninyang'anya hata senti moja.
  3. Nifunike vema na hilo jembe lako . . .
    Nalitangatanga, kati-ka ulimwengu
    (Basi) basi leo kiburi kimekwisha,
    Kumbe dunia hii ni mti mkavu.
  4. Nyumba yangu leo ni shimo udongoni
    Hakuna mlango, haku-na madirisha
    (Kita) kitanda changu na blanketi langu,
    Ni udongo mzito wanielemea
  5. Kifafanuacho wafu mbele ya Mungu . . .
    Si cheo kikubwa, si da-raja si sifa
    (Mate-) matendo mema saa ya kufa kwangu,
    Yatafungua mlango wa uwingu
  6. Ole wangu mimi nilifanya ujinga . . .
    Kwa kuambatana, na wa-tu wa dunia
    (Ona) ona wote leo wameniacha,
    Hasa watu wale niliowapenda.
  7. Unapojiona jiwazie mwenyewe . . .
    Kufa siku moja, kwa wo-te ni lazima
    (Japo) japo sultani japo ni mtumwa,
    Mungu atamwita ikiwa saa yake.
  8. Nimekufa leo nilipona salama . . .
    Nalijidhania, mwenye - afya mwilini
    (na ma-) na mara moja nikaanguka chini
    Labda huamini kwamba nali`mzima.
  9. Yesu msalabani kateswa vikali mno . . .
    Kwa kutukomboa, aka-mwaga damuye
    Wahurumie wote wa toharani,
    Mwanga wa milele uwaangazie.
  10. Kwaherini wote kwaherini wapenzi . . .
    Ninakwenda kwetu sita-rudi nyuma
    (Kwa he-) Kwaheri Baba kwaheri Mama yangu,
    Mungu akipenda kwake tukutane.
 
Msiba ni msiba huzuni lazima iwepo, wanafunzi was Yesu ambao Leo ndio mgano wa kuigwa kwetu, Yesu alikuwa anawaaga walihuzunika hata yeye akawatia moyo ya kwamba msihuzunike sitawaacha yatima. Ndio ije kuwa sisi? Ndugu zake Razaro waliomboleza wanamwabia Yesu kama ungelikuwepo kaka yetu asingekufa, angalia wale wajane walivyomlilia Dorcus mpaka Mungu akamrejeshea uhai wake, achana na msiba na hata Mungu anajua ndio maana akasema farijianeni ninyi kwa ninyi
Mbona unesema vema hata mtume Paulo anasema farijianeni, sasa kusema udongo mzito wanielemea au wanitesa (mfano tu wa nyimbo nyingi) ndio kuwafariji wafiwa????
 
Mbona unesema vema hata mtume Paulo anasema farijianeni, sasa kusema udongo mzito wanielemea au wanitesa (mfano tu wa nyimbo nyingi) ndio kuwafariji wafiwa????
Huo wimbo wa udongo mbona umeambiwa uuweke haujauweka, ili tusikie na maneno mengine tuone kweli kwenye huo wimbo hakuna maneno ya kufariji? Lakini ukumbuke pia msiba haupo kwa ajili ya aliyekufa Bali wanaobaki tukikumbushana kutengeneza maisha yetu, msiba unapotokea mwanadamu ndio huwa anakumbuka kuwa kumbe na yeye anafuata njia hiyo hiyo
 
Au anapoambiwa mkristo kuna mauti baada ya kuishi utasikia "pepo la mauti lishindwe,lishindwe ktk jina la yesu sasa najiuliza hivi hajui kama kufa ni lazima wakati ukifika,baba yetu adamu kafa itakuwa sie,Yesu ndie hakuinja kikombe hicho nae anasubiri arudi ili akionje,wakati mwingine naonelea kuwaacha tu wafu wazikane.
 
Back
Top Bottom